Ushauri ili CHADEMA ivunje ngome ya CCM Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri ili CHADEMA ivunje ngome ya CCM Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlangaja, Apr 12, 2012.

 1. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Tatizo kuu la wakazi wa Dodoma ni shirila la CDA. CDA kazi yake hapa dodoma ni kuendeleza makao makuu ya nchi. Kwa sababu hiyo shirika hili linasimamia upimaji na ugawaji wa viwanja. Hata hivyo shirika hili kwa mda mrefu sasa, limepotoka katika malengo yake na badala yake limekuwa ni shirka la kupima viwanja kwa ajili ya washikaji wa wafanyakazi wa CDA.

  Mwaka juzi nilikereka sana. CDA walitangaza viwanja 500 vya kuuza kwa wakazi wa Dodoma na sehemu mbali mbali za Tanzania. Lakini baada ya kuona watu waliojitokeza ni wengi sana na washikaji wao watakosa viwanja walianzisha vurugu ili kusitisha zoezi.

  Siku hiyo mke wangu alikuwa ni moja ya watu waliokuwa wamepanga mustari kwa ajili ya kununua kiwanja kwani mimi nilikuwa safarini. Cha ajabu baada ya fujo kuongezeka mke wangu alikoswa na bomu la majozi. Hii ina maana kwamba, CDA walituita kutuuzia viwanja na badala yake wakatupiga mabomu.

  CDA ni tatizo kubwa sana hapa Dodoma, kwani wanauza viwanja vya watu au kubadilisha viwanja bila ridhaa ya wamiliki. Wanachukua mashamba ya watu wa pembezoni mwa mji na kugawa kama wapendavyo. Hii imewafanya wakazi wengi ambao ni wazaliwa wa pembezoni mwa Dodoma kufilisika kabisa na kuwa masikini wa kutupwa. Mifano ni wakazi wengi wa Swaswa, Njedengwa, Chang' ombe, mji mpya, ntyuka na Msalato.

  Wengi wao wamepokonywa maeneo yao ambayo ndiyo ilikuwa rasilima yao na badala yake kuwa mali ya CDA na wao kubaki mikoni mitupu.

  Hebu fikiri mtu mwenye shamba la ekari kumi anapimiwa kiwanja kimoja cha m 25 kwa 18m. Je mtu huyu atatokaje tena? Atalima wapi, atalisha wanyama wake wapi?

  Pia palitokea uchunguzi fulani mwaka juzi na baadhi ya wakurugenzi walipatikana na viwanja 216 katika manispaa ya Dodoma tu! Hii ni ajabu kweli. Hata hivyo CCM hawana kabisa nia ya kuangalia tatizo hili.

  Kwa sababu hiyo basi, CHADEMA ili mkubalike hapa Dodoma, CDA pangeni sera za namna ya kumaliza matatizo ya viwanja hapa Dodoma. Masikini wengi watawakubalini sana, kwani wanataabika sana. Watu wanaishi karibu na mabwawa ya maji taka kule Swaswa, watu wanaishi sehemu zisizo na miundo mbinu kama Kwamwatano, Ntyuka na kwingineko.

  Hawa wote wanahitaji watu watakao waongoza katika ukombozi wa mateso haya makuu ya kuishi kama wakimbizi. CHADEMA angalieni hili na lifanyieni kazi.

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA
   
 2. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sawa. Ila CCM hawana ngome Dodoma, tatizo kule ni ujinga umaskini na uoga.
  Makamanda wakizunguka kutoa elimu na kuwatoa uoga, Dom mbona inakombolewa tu.
   
 3. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  CCM haina ngome Dodoma, ujinga na umasikini wa fikra ndio tatizo la Dodoma, binafsi nimekaa Dodoma miaka miwili nawajua vizuri ndugu zetu Wagogo, mtaji wa CCM ni kuwapotosha Watanzania na kuwazamisha katika lindi zito la umaskini, kwa Dom ni rahisi taking in consideration hizo sifa mbili. Iwapo mbunge wao (Mtera) ni Lusinde je unategemea nini kwa mwananch wa kawaida? Hiyo marufuku ya mikutano ya kisiasa ni hatua ya kuhakikisha DOdoma inaendelea kuwa ngome kuu ya umaskini na ukosefu wa elimu. Wito wangu Dom hakuna wa kuwaletea mabadiliko isipokuwa nyie wenyewe. Msikubali kunyamazishwa na madhalimu CCM la sivyo mtakuwa hohehahe milele. Tulianza mikoa ya pembezoni sasa tumedhamiria kuwakomboa
   
 4. M

  Makyomwango JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  m4c itaondoa ujinga na uoga wa watu wa Dodoma, viongozi wa Chadema wajipange vema katika mpango huu wa m4c.
   
Loading...