Ahsante boss, kweli wanawake wana purchase sana haswa uremboHiyo namba moja hakuna wanunuzi ama wateja wazuri kama wanawake...
hawa ni regular customer....ilimradi uwawekee vitu vinavyokwenda na wakati
ahsante boss kwa mchanganuo wakao, nisaidie una maanisha nini kusema kwenye mzunguko itakwama kwenye mali?Hiyo namba 4 kwa hela yako ni ndogo sana labda ufanye hiyo ma 3 na 2 kidogo mzunguko wa hela utakuwepo ila ukiingia hiyo namba 5 na 1 hutofika mahali maana kwenye mzunguko itakwama kwenye mali.
Labda uingize hela yako kwenye aluminium na glass na mapazia ya kisasa ndio biashara inayokimbiza kwa sasa.
shukrani kwa mawazo hayo mkuu..Biashara ya kwanza na ya 5 unaweza kuunganisha location moja.
Fanya hivo.
ahsante kwa hizo ideas,6.Spare za pikipiki na bajaj. Weka mafundi iwe gereji.
7. Biashara ya vitu vya jumla kama chumvi,mafuta ya kula, viberiti,unga,mchele,soda,maji,juisi,sabuni za unga, sabuni za kipande, stiliwaya,sigara,condom n.k
Fanya utafiti ukiangalia eneo ulipo,wingi wa watu ,hali ya kipato cha watu katika eneo lako, wingi wa maduka katika eneo lako na umbali toka barabara ya lami.
NB: kwenye mpesa na tigopesa kuwa makini sana wafanyakazi wanaiba balaaa, sikutishi ila ndio ukweli.
thank you bossUtakaa dukani wewe au utatafuta mtu akuuzie duka? Pia wewe binafsi una ujuzi na nini? Naona kuna cosmetics (no. 1), hardware (2,3, & 4), na finance services (no. 5). Ni vizuri kuanza na biashara ambayo una ujuzi nayo.
ahsante boss.cheza na namba moja au 4
NB: komaa mwenyewe kwenye biashara ukiwa na wasaidizi wako
usijifanye boss mapema
ahsante boss kwa upeo wako, hili nalo nitaliangalia kwa ukaribu zaidi..kwa sababu ni fursa nzuriBinafsi yangu mm naona ufanye biashara ya vyakula hakika itoka na kilipa kwa sababu kula ndio kunamfanya binadamu aendeleee kuishi, unaweza ukafungua duka la kuuza vitu vichache kama sukari,sembe, mafuta ya kula,ngano,mchele maharagwe,njugu mawe,choroko, mbaazi na kunde tafuta duka zuli linalouza vitu bei ya rahisi kama mafuta ya kula, unaweza fuata mahindi Shamba na ukayaleta ukatafuta MASHINE ukasaga sembe kisha ukapeleka kuuza dukani kwako, biashara ya vyakula ni nzuli
Sent using Jamii Forums mobile app