Ushauri bunge la vijana Kiteto watekelezwa

Ushauri bunge la vijana Kiteto watekelezwa

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Na Mohamed Hamad

Katika kile kilichoelezwa kuwa ni wazo lenye tija na ambalo halitasahaulika, Serikali ya Kijiji cha Dosidosi Wilayani Kiteto Manyara, imetekeleza wazo lililoibuliwa na Bunge la vijana.

Wazo hilo ni kuhusu ujenzi wa Kituo cha Afya ambapo kipindi chote wananchi wanalazimika kutembea umbali mrefu na gharama kusaka huduma hiyo.

Akiwa katika moja ya vikao vya Kijiji Hamzangia mmoja wa wananchi na mkt wa Bunge la vijana wilaya alishauri Serikali ya Kijiji kutenga fungu la fedha kwaajili ya kuanza ujenzi wa Kituo cha Afya.

Wazo hili liliungwa mkono na wananchi kisha shughuli za ujenzi kuanza ambapo sasa wako hatua ya msingi kujenga word 2 za thamani ya mil 160

Baadhi ya wananchi wameonyesha kufurahishwa na mchango huo wakisema Bunge hilo la vijana litakuwa mwarubaini wa matatizo kijijini hapo.
 
Back
Top Bottom