Ushauri: Biashara ya duka la pembejeo za kilimo

Ushauri: Biashara ya duka la pembejeo za kilimo

ijoz

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
731
Reaction score
718
Wadau,naomba kwa wenye ujuzi/wazoefu wa biashara ya pembejeo za kilimo na mifugo (kama vile madawa,mashudu n.k) anijuze taratibu za kufuata ili kuanzisha duka ikiwa na vigezo vya kitaalamu kama vipo.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Wana JF sijasomea kilimo basically lakini nimepata wazo la kuanzisha biashara ya pembejeo na kilimo pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu wa kilimo in general. Napenda kuwa nasafiri nje kufanya shughuli zinazousiana na kilimo kama Hongkong na China.

Ushauri wadau kwa wazoefu wa mambo haya
 
Let me declear interest firs, mm nmesomea kilimo (general agriculture).

Pamoja na hayo na japo sina uzoefu na biashara hiyo lakini naweza kukushauri mambo mawili matatu kwanza hilo wazo ulilonalo ni moja kati ya mawazo mazuri pia kwa sababu kwa hali ya sasa ni vigumu kwa wakulima na wafugaji kulima au kufuga bila kutumia pembejeo za kilimo hivyo idea ya kufungua duka la pembejeo ni inalipa tu ila cha kuangalia kua unalifungulia wap ilikurahisisha upatikanaji wa wateja katika eneo husika, na pia wakati unafikiria experties wa kufanya kaz kwenye hiyo biashara yako ndugu yako hapa nipo unaweza ukaniajiri mana bado sijaajiriwa tangu nimalize chuo mwakajana 2013.
 
Let me declear interest firs, mm nmesomea kilimo (general agriculture). Pamoja na hayo na japo sina uzoefu na biashara hiyo lakini naweza kukushauri mambo mawili matatu kwanza hilo wazo ulilonalo ni moja kati ya mawazo mazuri pia kwa sababu kwa hali ya sasa ni vigumu kwa wakulima na wafugaji kulima au kufuga bila kutumia pembejeo za kilimo hivyo idea ya kufungua duka la pembejeo ni inalipa tu ila cha kuangalia kua unalifungulia wap ilikurahisisha upatikanaji wa wateja katika eneo husika, na pia wakati unafikiria experties wa kufanya kaz kwenye hiyo biashara yako ndugu yako hapa nipo unaweza ukaniajiri mana bado sijaajiriwa tangu nimalize chuo mwakajana 2013.
Sawa nashukuru sana mdau kwa angalizo ila biashara nataka kufungua Morogoro vipi unaweza kunipa updates zaidi,ntakachofanya nkiwa successful ntakuita kwa ushauri wa kawaida na wakitaalamu sina pesa za kuajiri kwa sasa ila waweza kuni pm contacts zako tutawasiliana,niko Morogoro mjini
 
Hbr wanajamvi .
Nina mpango wa kufungua Agrovet ndogo ya 3mlns ili niizungushe hiyo pesa nitengeneze ya zaidi.

Nafanya Kazi maeneo ya kijijini na pana soko siku ya j5, kwa tathmini ya haraka nionavyo wakulima hawapati kabisa huduma za pembejeo za Kilimo hivyo nikianzisha basi nitakuwa nimewasogezea krb.

Wadau wenye uzoefu na hii biashara naombeni ushauri please kabla sijaanza. Yaani Biashara ina faida gani na changamoto zake kubwa ni nini.

Pia natarajia kununua mashine ya kumwagilia ili nianze kununua bustani kadri nitakavyoweza.
Je , Mbegu gani nzuri ya nyanya na vitunguu hybrid ni nzuri kwa Kilimo( outdoor) Sio greenhouse. Na bei ipoje.? Nipo Simiyu. Krbn
 
Hbr wanajamvi
Nina mpango wa kufungua Agrovet ndogo ya 3mlns ili niizungushe hiyo pesa nitengeneze ya zaidi.
Nafanya Kazi maeneo ya kijijini na pana soko siku ya j5, kwa tathmini ya haraka nionavyo wakulima hawapati kabisa huduma za pembejeo za Kilimo hivyo nikianzisha basi nitakuwa nimewasogezea krb.
Wadau wenye uzoefu na hii biashara naombeni ushauri please kabla sijaanza
Yaani Biashara ina faida gani na changamoto zake kubwa ni nini.

Pia natarajia kununua mashine ya kumwagilia ili nianze kununua bustani kadri nitakavyoweza.
Je , Mbegu gani nzuri ya nyanya na vitunguu hybrid ni nzuri kwa Kilimo( outdoor) Sio greenhouse. Na bei ipoje.? Nipo Simiyu. Krbn
Mkuu upo gangabilili?
 
Uko Sawa
Kwa mbegu vitunguu tumia red bombay kwa nyanya angalia annaF1,Kipato au assila ila kama ndo unaanza tumia nyanya mwanga
 
Wadau habari zenu.
Niko Arusha, nataka kufanya biashara ya viwatilifu/pembejeo za kilimo. Naomba msaada kwa anayejua Suppliers na mbinu za hii biashara. Mtaji ni mdogo kwa hiyo sio biashara kubwa kivilee.
 
Waone (TFA) Tanganyika Farmers association hapo Arusha watakupa msaada
 
Salaam wakuu,

Naombeni kwa wanaojua utaratibu wa kufuata ili kuanzisha duka la pembejeo za kilimo. Ni hatua gani zinatakiwa zifuatwe, vigezo na masharti yake, changamoto n.k. Niyafurahi sana kama nitapata ambae ana uzoefu katika hili anitoe tongotongo machoni kwani hakuna ninalolijua katika hii biashara. Shukrani sana
 
Nakushauri, Nenda ofisi ya kilimo na mifugo wilaya watakupa muongozo kuhusu maswala ya kuanxisha maduka viwatilifu
 
waungwana nafikiria kufungua duka la pembejeo za kilimo na mifugo maeneo ya wilaya ya kisarawe mkoa wa pwani....

naomba mchango wa mawazo mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuanza...maana kwa utafiti mdogo nilioufanya wilaya nzima kuna duka moja tuu lililopo maeneo ya kisarawe mjini...

na maeneo ya vijijini kuna wafugaji na wakulima ambao uwalazimu kufuata mbejeo kati ya mlandizi ,kisarawe na dar... nataka kutumia hiyo fursa....

kwa kutumia jukwa hili naomba ushauri wenu....
 
Poa poa mkuu.
Jirizishe na watumiaji ipasavyo kabla ya kujilipua na uchague eneo ambalo ni rahisi watu kulifikia kwa ajili ya hayo mahitaji
 
Habari ndugu zangu wa JF,

Samahani nilikua naomba ushauri ninataka kuanzisha duka dogo tu la pembejeo za kilimo, je niandae mtaji wa kiasi cha shillingi ngapi, duka dogo tu la kuanzia.
 
Habar Kuna jambo la TPRI, linanichanganya kidogo Hasa kwa watu walio hitimu vyuo vya kilimo na mifugo. Mtu kakaa darasani 2, 3 or 5yrs alafu akitaka kufungua duka la pembejeo eti had akapate mafunzo maalum ya siku tatu kwa malipo ya tshs 320000 TPRI, 450000 vet, 300000 mamlaka ya Mbolea 300000+ tosc.

Je waliwafikilia vijana wanao maliza vyuo vya kilimo na mifugo ambao mitaji tu ni Shida wanaweza kulipa Ada hizo.? Ikiwa wanashindwaje kumuamin mtaalam alie soma chuo wamuamini mtu tu walie mpa mafunzo kwa malipo hayo.?

Lengo ni kutoa elimu au kukusanya pesa tuu.? Kwa kua wengi wao hasa vijijni hawajapata hayo mafunzo maalum inabid wafunge viduka vyao je wakulima wataweza kufuata huduma za viuatrifu mijini kwa walio pata mafunzo maalum.?

kwa mabwana shamba ambao ndo wanakaa na wakulima na kuwapa ushauri wa matumizi ya pembejeo Inamaana nao hawafai sasa kwa kua hawajapewa mafunzo maalum .? Kwa sasa mtu wa darasa la Saba alie pata mafunzo maalum ya siku tatu anaonekana ni bora zaid kuliko mtaalam alie soma chuo.

Duu ikaeje hii.
 
Back
Top Bottom