Ushauri: Anataka kuwa na mimi muda wote wakati ameniacha

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
378
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 26.

Nilikuwa na mpenzi tuliyedumu naye kwa takribani miaka miwili na miezi kadhaa sasa. Ni wiki iliyopita tu alitoka kuniambia kuwa mimi na yeye mapenzi yetu yameishia hapo. Nikimuuliza kitu gani nilichokosea, anajibu kuwa hakuna kibaya nilichofanya na ataendelea kuwa msaada kwangu muda wowote nitakapomuhitaji.

Kikubwa ni yeye anataka kujenga maisha yake.Binafsi sioni kama kweli kujenga maisha kunaweza kumsababishia yeye kuniacha. Nilikubali kuwa naye kwa hali yoyote aliyokuwa nayo. Sikuwahi kumbugudhi aninunulie chochote cha gharama ama kunipa pesa ya matumizi. Nilijua mfuko wake vema.

Nikakubali aondoke kishingo upande ingawa nilijaribu kuomba msamaha na kuahidi nitajirekebisha pale anapoona nakosea alikataa kata kata kuwa nami.Kitu cha ajabu kinachonishangaza, ni ile tabia yake ya kutaka kuwa nami muda wote pamoja na kuwa ameshaniacha.

Sielewi wana JamiiForum. Sijui ana malengo ya kuumiza moyo wangu tu ama bado ananipenda?
 
Kichaaa...sio kila anaevaa nguo fyuzi ziko connected.
Ipo siku atakuona kama kuku akakuchinja maana hayupo sawa kichwan
 
Mapenzi utundu, anaweza achwa yoyote.

Pole sana, Fanya mambo yako sasa
 
Huyo anakutumia kwa muda tu then akiona mwingine anakutema inaonesha alikuwa naye wamebwagana sasa karudi na kama ukikubali afunue kifuniko chako cha asali Loading........................error!
 
anakupima uvumilivu wako uyooo embu mwambie anachokitaka umekikubali uone atasemajeeeee!!!
 
inatakiwa uruhusu akili yako isonge mbele, usikae unawaza kitu kimoja utadumaa, futa huo ukaribu mlio nao ukiweza mwambie umepata mtu hivyo mkate mawasiliano, samtyme inabidi uwe na maamuzi yako usikubali kuyumbishwa, sasa wewe jifanye unajua kupenda kama julieth au jack uone ya walimwengu
 
Back
Top Bottom