Ushambuliwa padri ambrose- si dogo, lakini ‘dal-sek-ned’!

Baraghash

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2012
Posts
2,713
Reaction score
1,790
KUSHAMBULIWA PADRI AMBROSE- SI DOGO, LAKINI ‘DAL-SEK-NED'!

Written by SHAMUHUNA // 28/12/2012 // Makala/Tahariri // Mzalendo.net

Enzi zile Zanzibar kuna Taarab, kikundi kimoja kiliwahi kuimba wimbo uitwao ‘Watende wao'. Katika wimbo huo mwimbaji anasema, ‘Watende wao kina mwafulani. Kitendo wenzao, kutwa midomoni'. Kisha mwimbaji anaendelea kwa kusema, ‘ajabu ya watu hao, ajabu yakini, ajabu yakini, ajabu ya hao, yao hawaoni'. Mwisho wa kunukuu.

Nalazimika kunukuu vipande hivi vya wimbo, baada ya tukio la kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya, padre Ambrose Mkenda jioni ya siku ya Krismasi, huko nyumbani kwake Tomondo.Nanukuu si kwa maana ya kuhalalisha kitendo alichofanyiwa padre kwani, si kitendo cha kiungwana wala cha kibinadamu. Na kwa hili naungana na watu wote kulaani kitendo hicho cha kinyama dhidi ya padri Mkenda.
Kama kuna msomaji anafuatilia makala zetu nyingi hapa katika mzalendo, ataona kuwa mara nyingi tunapigania usawa na haki ya Mzanzibari katika Muungano.Ya kwamba, Muungano uwepo au usiwepo, kwa nguvu moja tunasema haumtendei haki Mzanzibar, na hasa akiwa muislamu. Kwamba kosa lolote lenye udogo mithili ya mdudu chungu, ilhali amelifanya Mzanzibar-muislamu, hilo huwa ‘mwao'. Huwa m'boga, ukatambaa, usifike mwisho. Dogo hukuzwa, na kusemwa na wakubwa na wanene wa nchi.Likawa jambo likatuojea.

Ni kweli kabisa, kitendo cha kujeruhiwa vibaya kwa padre Mkenda, si cha kiungwana. Na bila shaka kinastahiki uchunguzi haraka wa Polisi. Na kwa sasa polisi ya Zanzibar, imeshafunguwa upelelezi kabambe juu ya tukio hilo. Naamini kwa jinsi tukio lilivyotokea, polisi Zanzibar inatosha kufuatilia na kuweza kutambua ukweli na undani wa tukio hilo. Hii ni kwa sababu tunaliamini jeshi la polisi juu ya upelelezi, na ufanisi wa kesi kama hizi.

Tumeona jinsi sayansi na teknolijia ilivyotumika kuwatia nguvuni wahusika wa vurugu za bubu zilizopelekea kuuwawa kwa askari polisi. Pilisi, ilifanya upelelzi wake, na tuliyaona waliyoyagundua. Na kwa hili pia hatuna shaka wanaliweza.
Cha ajabu, licha ya kuwa tukio lenyewe ni kubwa sana, sioni haja ya kuletwa tena makachero ‘waliobobea' kutoka bora, kwa kile kinachoitwa ‘kuongeza nguvu' juu ya tukio hili. Suali la kuletwa makachero wa bara, wakati hapa kwetu tuna kitengo maalum, chenye ujuzi na uzoefu wa upelelezi, kunanipa shaka nyingi sana kuliko imani ya utendaji wenyewe unaolengwa kuongeza ‘nguvu' na ufanisi unaodaiwa.
Hofu yangu ya kwanza ni kwamba kwanini kitengo cha polisi cha upelelezi cha Zanzibar kiongezewe nguvu kutoka bara? Kwani kiliomba kusaidiwa, baada ya kuzidiwa na hali? Na upande wa pili ni pale ukijadili dhana ya kuongeza nguvu inapohitajika. Kiuozoefu tunaongezea nguvu pahala palipoonesha kuzidiwa na hali iliyopo. Jee hili lishajitokeza kuwa Jeshi la polisi limeshazidiwa na ufuatiliaji wa upelelezi wa kesi hii? Nahisi bado mapema kuomba msaada wa aina hii bado.
Upande mwengine, unaposema unaliongezea nguvu jeshi, tena kwa kuleta makachero ‘waliobobea' kutoka bara, unamaanisha kuwa makachero waliopo hapa Zanzibar ni ‘vibwengo, vichamba umande, au vimasantula' tu, visivyo na uzoefu. Na kama hivi ndivyo, nalazimika kuleta tena shaka nyengine ya kwanini nguvu hii iongezwe kwa kujeruhiwa padre Mkenda tu?
Alikamatwa Sheikh Farid, lakini kwa bahati mbaya si jeshi la polisi Zanzibar wala bara lilianza upelelezi wowote. Suali la Farid liliachwa kama alietekwa ni paka au mbuzi tu, na hata baada ya kuonekana aliishia kutiwa hatiani na kufungiwa rumande badala ya kuwatafuta waliomteka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Kisa, ni Mzanzibari na muislamu.
Karibuni hivi alimwagiwa tindikali Sheikh Fadhili Soraga. Kwa sadfa ya tukio hili utaona Sheikh Soraga ni ‘mwenzao'. Kwa ufupi na lilipotokea la Soraga, kila kiongozi alipania kumuona kumjulia hali Sheikh. Kwa upande wa jeshi la polisi Zanzibar, waliapa kuanzisha upelelezi mkali dhidi ya kadhia hii. Kwa bahati mbaya tena, hatukuwasikia makachero wowote kutoka bara walioletwa kuja kupelelza kadhia ya soraga, na mpaka hii leo hatujui kesi hii ilipokomea.Au hili halikuhitaji kuongezewa nguvu?
Sambamba na haya, kuna matokeo chekea ya uhalifu nchini hapa ambayo yalipuuzwa kufuatiliwa na wala hayakuchukuliwa hatua zozote za kufaa. Cha ajabu, akijeruhiwa mtu wa kanisa hata kama alikuwa na ugomvi na watu wengine, kwa bahati mbaya au kwa maswali yao ya mipango binafsi basi hilo hufanywa kubwa. Na kuanzia hapo tunaanza kulipa ukubwa na kulizidisha mada na shadda, tukianzia na ni sisi Wazanzibari wenyewe.
Kwa mfano, mara tu baada ya tukio, taarifa ya awali ya polisi ilihusisha tukio hilo la ujambazi na uwezekano wa padre huyo kuwa na pesa alizozipata katika michango ya waumini siku hio ya krismasi. Kauli hii aliekimbilia kuitoa, inaonekana haikuwaridhisha wakubwa, na wakoloni wetu kwani haikutegemewa isukwe hivyo. Taarifa kama hii ilikuwa isukwe, kwa kuhusishwa waislamu na jumuiya ya uamsho. Hapo wenzetu na viongozi wetu wangeridhika, japo kuwa sio kweli.
Pia Balozi Seif Idd, alikuwa kiongozi wa kwanza wa Zanzibar kulikozesha tukio hili. Na ni kwa sababu ya kauli yake yeye ndie makachero ‘waliobobea' wakaletwa. Na kwa wale wajuzi wa lugha wajue kuwa hii ‘kubobea' hapa ni kuwa na ujuzi uliopindukia wa kuchonga, kuumba-umba na kuzua mambo yaliyokuwa ndiyo na yasiyokuayo. Ya kweli na ya uongo. Huo ndio ubobevu wenyewe.
Hofu yangu, kwanini iwe hivi, tena kwa matukio yawahusuyo watu Fulani tu kuwa yaonekane ndio wenye haki zaidi mbele ya sheria na akina Fulani wawe si chochote si lolote? Nakumbusha tena kuwa silioni dogo tukio la Padri Mkenda, lakini kwanini iwe kwa akina hawa tu? Nionavyo, kuna kijambo kinatafutwa hapa. Sio bure maana kama ni la upelelezi tu, hakukuwa na haja ya kulikozesha na kulitia madda na shadda kiasi hiki. Tutende haki, tukiamini watu wote wana haki sawa mbele ya sheria.

Natoa hoja
 
Kwanza kabisa napenda ujue kuwa tukio la padre mkenda halikulenga kumjeruhi tu lililenga kumtoa uhai, ashukuriwe Yesu Kristu anayejidhihirisha kupitia neno lake kuwa wafuasi wake watalishwa vitu vya kuwafisha ila hawatakufa.
Pili, tukio hilo lilitokea baada ya kuwepo kwa vipeperushi vyenye vitisho kwa wakristu wakati wa Xmass,
Tatu, tukio hilo limetokea miezi michache baada ya uchomaji wa makanisa na miundo mbinu ya wakristu
Nne, hakuna hata mtu mmoja aliyetiwa mbaroni kwa tukio hilo.
Kwa hiyo kwa mtu yeyote anayethamini uhai wa binadamu mwingine lazima ataona kuna haja ya kuongeza nguvu kujua hawa al shaabab ni akina nani na wanafadhiliwa na nani!
 
Kwanza kabisa napenda ujue kuwa tukio la padre mkenda halikulenga kumjeruhi tu lililenga kumtoa uhai, ashukuriwe Yesu Kristu anayejidhihirisha kupitia neno lake kuwa wafuasi wake watalishwa vitu vya kuwafisha ila hawatakufa.
Pili, tukio hilo lilitokea baada ya kuwepo kwa vipeperushi vyenye vitisho kwa wakristu wakati wa Xmass,
Tatu, tukio hilo limetokea miezi michache baada ya uchomaji wa makanisa na miundo mbinu ya wakristu
Nne, hakuna hata mtu mmoja aliyetiwa mbaroni kwa matukio yote hayo.
Kwa hiyo kwa mtu yeyote anayethamini uhai wa binadamu mwingine lazima ataona kuna haja ya kuongeza nguvu kujua hawa al shaabab ni akina nani na wanafadhiliwa na nani!
 
hapa yapo mambo yamejificha tuliona sheikh alivyolipukiwa na bomu kule arusha sombetini hakuna taarifa yenye kufafanua bomu lile ni la aina gani na limetengenezwa wapi ,na yanapatikana wapi ,tunasoma habari masista kuvamiwa na majambazi kule dar hakuna ripoti yenye muelekeo ,makanisa yamechomwa moto ,polisi ripoti hakuna kutuliza hasira za wananchi na kutoa tumaini jema ,tukiwa bado tuna pigwa na butwaa padri apigwe risasi tukio limeambatana kwa karibu na maaskofu wanalaani ukimya wa serikali juu ya matukio haya siku iliyofuata padri ashambuliwa ,jeshi la polisi wameona maganda ya risasi pale ,hawajatoa tamko ,risasi ile ni ya wapi ,risasi ile inapatikana wapi na watu gani huruhusiwa kuwa na silaha za aina ile na zinatumika kwenye bunduki ya aina gani. Kwa ujumla hali ilivyo wnajamii wana kiu ya kupata majibu mengi ambayo majibu yake hayako kwa wanajamii bali yapo kwenye taasisi za serikali hasa jeshi la polisi .jeshi liamke sasa lilete matumaini kwamba lipo kazini na si kusubiri tukio na watoto wa mjini wanasema kupotezea .
 
i see!

Kama kuna msomaji anafuatilia makala zetu nyingi hapa katika mzalendo, ataona kuwa mara nyingi tunapigania usawa na haki ya Mzanzibari katika Muungano.Ya kwamba, Muungano uwepo au usiwepo, kwa nguvu moja tunasema haumtendei haki Mzanzibar, na hasa akiwa muislamu. Kwamba kosa lolote lenye udogo mithili ya mdudu chungu, ilhali amelifanya Mzanzibar-muislamu, hilo huwa ‘mwao’. Huwa m’boga, ukatambaa, usifike mwisho. Dogo hukuzwa, na kusemwa na wakubwa na wanene wa nchi.Likawa jambo likatuojea
 
KUSHAMBULIWA PADRI AMBROSE- SI DOGO, LAKINI ‘DAL-SEK-NED'!

Written by SHAMUHUNA // 28/12/2012 // Makala/Tahariri // Mzalendo.net

Enzi zile Zanzibar kuna Taarab, kikundi kimoja kiliwahi kuimba wimbo uitwao ‘Watende wao'. Katika wimbo huo mwimbaji anasema, ‘Watende wao kina mwafulani. Kitendo wenzao, kutwa midomoni'. Kisha mwimbaji anaendelea kwa kusema, ‘ajabu ya watu hao, ajabu yakini, ajabu yakini, ajabu ya hao, yao hawaoni'. Mwisho wa kunukuu.

Nalazimika kunukuu vipande hivi vya wimbo, baada ya tukio la kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya, padre Ambrose Mkenda jioni ya siku ya Krismasi, huko nyumbani kwake Tomondo.Nanukuu si kwa maana ya kuhalalisha kitendo alichofanyiwa padre kwani, si kitendo cha kiungwana wala cha kibinadamu. Na kwa hili naungana na watu wote kulaani kitendo hicho cha kinyama dhidi ya padri Mkenda.
Kama kuna msomaji anafuatilia makala zetu nyingi hapa katika mzalendo, ataona kuwa mara nyingi tunapigania usawa na haki ya Mzanzibari katika Muungano.Ya kwamba, Muungano uwepo au usiwepo, kwa nguvu moja tunasema haumtendei haki Mzanzibar, na hasa akiwa muislamu. Kwamba kosa lolote lenye udogo mithili ya mdudu chungu, ilhali amelifanya Mzanzibar-muislamu, hilo huwa ‘mwao'. Huwa m'boga, ukatambaa, usifike mwisho. Dogo hukuzwa, na kusemwa na wakubwa na wanene wa nchi.Likawa jambo likatuojea.

Ni kweli kabisa, kitendo cha kujeruhiwa vibaya kwa padre Mkenda, si cha kiungwana. Na bila shaka kinastahiki uchunguzi haraka wa Polisi. Na kwa sasa polisi ya Zanzibar, imeshafunguwa upelelezi kabambe juu ya tukio hilo. Naamini kwa jinsi tukio lilivyotokea, polisi Zanzibar inatosha kufuatilia na kuweza kutambua ukweli na undani wa tukio hilo. Hii ni kwa sababu tunaliamini jeshi la polisi juu ya upelelezi, na ufanisi wa kesi kama hizi.

Tumeona jinsi sayansi na teknolijia ilivyotumika kuwatia nguvuni wahusika wa vurugu za bubu zilizopelekea kuuwawa kwa askari polisi. Pilisi, ilifanya upelelzi wake, na tuliyaona waliyoyagundua. Na kwa hili pia hatuna shaka wanaliweza.
Cha ajabu, licha ya kuwa tukio lenyewe ni kubwa sana, sioni haja ya kuletwa tena makachero ‘waliobobea' kutoka bora, kwa kile kinachoitwa ‘kuongeza nguvu' juu ya tukio hili. Suali la kuletwa makachero wa bara, wakati hapa kwetu tuna kitengo maalum, chenye ujuzi na uzoefu wa upelelezi, kunanipa shaka nyingi sana kuliko imani ya utendaji wenyewe unaolengwa kuongeza ‘nguvu' na ufanisi unaodaiwa.
Hofu yangu ya kwanza ni kwamba kwanini kitengo cha polisi cha upelelezi cha Zanzibar kiongezewe nguvu kutoka bara? Kwani kiliomba kusaidiwa, baada ya kuzidiwa na hali? Na upande wa pili ni pale ukijadili dhana ya kuongeza nguvu inapohitajika. Kiuozoefu tunaongezea nguvu pahala palipoonesha kuzidiwa na hali iliyopo. Jee hili lishajitokeza kuwa Jeshi la polisi limeshazidiwa na ufuatiliaji wa upelelezi wa kesi hii? Nahisi bado mapema kuomba msaada wa aina hii bado.
Upande mwengine, unaposema unaliongezea nguvu jeshi, tena kwa kuleta makachero ‘waliobobea' kutoka bara, unamaanisha kuwa makachero waliopo hapa Zanzibar ni ‘vibwengo, vichamba umande, au vimasantula' tu, visivyo na uzoefu. Na kama hivi ndivyo, nalazimika kuleta tena shaka nyengine ya kwanini nguvu hii iongezwe kwa kujeruhiwa padre Mkenda tu?
Alikamatwa Sheikh Farid, lakini kwa bahati mbaya si jeshi la polisi Zanzibar wala bara lilianza upelelezi wowote. Suali la Farid liliachwa kama alietekwa ni paka au mbuzi tu, na hata baada ya kuonekana aliishia kutiwa hatiani na kufungiwa rumande badala ya kuwatafuta waliomteka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Kisa, ni Mzanzibari na muislamu.
Karibuni hivi alimwagiwa tindikali Sheikh Fadhili Soraga. Kwa sadfa ya tukio hili utaona Sheikh Soraga ni ‘mwenzao'. Kwa ufupi na lilipotokea la Soraga, kila kiongozi alipania kumuona kumjulia hali Sheikh. Kwa upande wa jeshi la polisi Zanzibar, waliapa kuanzisha upelelezi mkali dhidi ya kadhia hii. Kwa bahati mbaya tena, hatukuwasikia makachero wowote kutoka bara walioletwa kuja kupelelza kadhia ya soraga, na mpaka hii leo hatujui kesi hii ilipokomea.Au hili halikuhitaji kuongezewa nguvu?
Sambamba na haya, kuna matokeo chekea ya uhalifu nchini hapa ambayo yalipuuzwa kufuatiliwa na wala hayakuchukuliwa hatua zozote za kufaa. Cha ajabu, akijeruhiwa mtu wa kanisa hata kama alikuwa na ugomvi na watu wengine, kwa bahati mbaya au kwa maswali yao ya mipango binafsi basi hilo hufanywa kubwa. Na kuanzia hapo tunaanza kulipa ukubwa na kulizidisha mada na shadda, tukianzia na ni sisi Wazanzibari wenyewe.
Kwa mfano, mara tu baada ya tukio, taarifa ya awali ya polisi ilihusisha tukio hilo la ujambazi na uwezekano wa padre huyo kuwa na pesa alizozipata katika michango ya waumini siku hio ya krismasi. Kauli hii aliekimbilia kuitoa, inaonekana haikuwaridhisha wakubwa, na wakoloni wetu kwani haikutegemewa isukwe hivyo. Taarifa kama hii ilikuwa isukwe, kwa kuhusishwa waislamu na jumuiya ya uamsho. Hapo wenzetu na viongozi wetu wangeridhika, japo kuwa sio kweli.
Pia Balozi Seif Idd, alikuwa kiongozi wa kwanza wa Zanzibar kulikozesha tukio hili. Na ni kwa sababu ya kauli yake yeye ndie makachero ‘waliobobea' wakaletwa. Na kwa wale wajuzi wa lugha wajue kuwa hii ‘kubobea' hapa ni kuwa na ujuzi uliopindukia wa kuchonga, kuumba-umba na kuzua mambo yaliyokuwa ndiyo na yasiyokuayo. Ya kweli na ya uongo. Huo ndio ubobevu wenyewe.
Hofu yangu, kwanini iwe hivi, tena kwa matukio yawahusuyo watu Fulani tu kuwa yaonekane ndio wenye haki zaidi mbele ya sheria na akina Fulani wawe si chochote si lolote? Nakumbusha tena kuwa silioni dogo tukio la Padri Mkenda, lakini kwanini iwe kwa akina hawa tu? Nionavyo, kuna kijambo kinatafutwa hapa. Sio bure maana kama ni la upelelezi tu, hakukuwa na haja ya kulikozesha na kulitia madda na shadda kiasi hiki. Tutende haki, tukiamini watu wote wana haki sawa mbele ya sheria.

Natoa hoja
umeeleza mengi lkn ndugu yangu umechanganywa na watu wa magazeti. kupaisha sifa za hao askari waliokuja huko. ZANZIBAR kwa sasa ni moja ya maeneo yenye uhalifu wa ajabu ajabu tofauti na zamani. kwa taarifa yako tu, jeshi la polisi ni moja TZ nzima. hivyo suala lolote linapotokezea taarifa lazima ziletwe makao makuu zikiwa na mapendekezo nini kifanyike. na mara zote si ZNZ peke yake popote pale TZ jambo lolote la kiuhalifu likiwa kubwa lazima timu iundwe na kupewa maelekezo kuelekea kuliko na kadhia tumesikia hivyo. IRINGA kwa MWANGOSI, nGARA kwa wale askari na hata huko ZNZ kwa SHEIKH FARID najua unafahamu vyema mambo ya sheikh huyu na mambo yaliyomfika. huyu wafuasi wake walileta fujo kubwa kiasi cha kupelekea mauwaji wa askari polisi, timu ya mapolisi tulielezwa ilikuja huko na kubaini SHEIKH hakutekwa jibu analo mwenyewe na rafiki zake ndo maana leo hii yuko mahakamani.
 
Hawa waznz akili zao haziijui shule ndio maana ata kuandika makala hawajui,wanachoweza ni kuandika taarab..ukisoma vizuri uhandishi wa uyu mwandishi ni wazi kabisa anapumuliwa.
 
When a Christian is attacked, normally no body says anything, in contrast, when something weird happens in the religion of peace, they will act inhumane and makes someone to wonder whether that religion is from God and their demigod is a true deity.
 
Mleta maada, ulikuwa umelewa tende wakati unaandika haya uliyoyaandika? What's is your point?
 
Inawezekana una hoja na pengine umeguswa ki-aina flani na tukio hili, lakini kwa maoni yangu una wajibu wa kuzijali hisia za watu wengine pia kama vile unavyotaka wewe wengine wajali hisia zako.

Mfano wake hapa wewe una mtoto waho mahututi ambaye aweza kufa mda wowote unamlaumu daktari ambaye anaomboleza msiba wa mwanawe
 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibarimefika njia panda kutokana na matukio mabaya na ya ghafla yanayotokea hapaZanzibar, hasa yanayobeba sura ya ‘hit and run attacks' ambayo pia yanaingiakatika sura ya visasi (revenge) - kuanzia lile la Soraga hadi la huyu Padri.
Kuna nadharia nyingi hapazinazohusu uhalifu (theories on criminology) - au hata conspiracy theory.
Nadharia 1: hujuma inafanyikalakini hakuna clue/au hata alama ya namna uhalifu ulivyofanyika - hapa inakluwataabu kwa wapelelezi kugundua namna ya ualifu huo ulivyofanyika, au vipiumefanyika, na hata kuanzia pa kufanya upelelezi.
Nadharia ya 2: Uhalifuumefanyika, aliyefanyiwa uhalifu yuko hai, na kauli thabit anaweza kusema. Hapainakuwa rahisi sana sana kwa makachero kujua na kuanza upelekezi wa kina. Kesizote mbili zilizotokea Zanzibar (Soraga na Padri zinaingia hapa).
Wote wazima na wote wana kaulithabit. Padri ameweza kuzungumza na kuweza kuidhalilisha POLISI kama taasisipale alipotoa kauli yake kumpinga RPC Aziz.
Kauli ya Padri dhidi ya jeshi lapolisi inaonyesha dhahir kuwa kanisa linataka watendewe vile wanavyotaka wao;na sio hali halisi ilivyo. Ingawa hakusema wazi wazi, lakini indirectly, anamaana ya kusema kuwa ‘polisi ni muongo, au waongo'. Hii ni idhalali kubwa kwajeshi la polisi.
Kw auhakika ni kuwa padri huyualikuwa anashika pesa, whether awe mhasibu by professional or not. Kwa uhakika100% padri huyu ndiye signatory wao.
Bila yeye haitoki pesa. Je, nahili atalipinga. Naomba hao makachero wa kutajika kutoka Dar, waanzie hapa kamandio ‘lead' yao. Tumelewwana? Muanzie hapa. Je, haiwi kuwa ‘internal job'.
Angalia sequence za kihalifuzilizofanyika TZ karibuni:
i. Afisa wa kuzuia rushwa apigwa na kuuliwa na mwenzake Dar
ii. RPC Mwanza apigwa risasi na kuuliwa Mwanza.
iii. Pesa nyingi zimeibiwa duka la Dar (150m) - kitendawili mpaka leo???? Aukwa sababu hili limetokea Zanzibar. Achane kuwa bias!
iv. Kuna mauwaji mengi yametokea Dar during chrismas time, mzungu mmojaamenyongwa hotelini, na wengine kuuwawa kikatili …kimya! kimya!

Nadharia 3: Nadhani kanisa, CCMTZ na serikali zote zitafurahi sana kama report ya makachero hayo zitasema kuwaUAMSHO ndio waliofanya kosa hilo. Mimi naomba kuwasaidia kitu.
Mpaka sasa, ukweli ni kuwa,waislamu wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, hawajafikia level hiyo ya kutumiasilaha au kuhujumu. Hili linajulikana na liko wazi. Kisocholojia, bora hatasiasa Zanzibar zinaweza kuwa ni ‘problem' kuliko hata dini.
Mimi naomba serikali ya JK, Sheinna IGP Said Mwema muwe waangalifu sana na trend hii inayojitokeza. Mjaribu sanakuwa fair na wakweli – otherwise, mnaimaliza nchi hivi mnajiona. Your carelessminds - JK, Shein, Mwema and others - inaweza kuleta bad feelings kwa waislamuambayo wanaamini kuwa Zanzibar ni nchi yao na nchi ya kiislamu. Hivi JK kuonifakhari kuwa hivyo, yaani Zanzibar ndio kama kigezo kwa dunia v.s Tanzania.
Kumbuka kuwa mnapewa pesa za burena nchi za kiislamu kupeleka hajj waislamu (ni kupitia mgongo wa Uislamu waZanzibar, na sio Tabora au Singida n.k); then mnachagua wakereketwa kwenda hukoHajj na kuacha waumin wa kweli.
Chokochoko hizi za dini, na hasaukiristo - hautoijenga TZ, ila itaivunja vunja viapande vipande – angaliasecratian war - Northern Ireland, former Yugoslavia [Kosovo, Serbia n.] Iraqn.k.
Shein na JK mnakaa na kubabaishwana washauri wenu; na hamtaki kutumia akili zenu mlizojaaliwa hata 0.01%. Hebutafuteni ukweli wa mambo. Huu ndi ushauri w abure kutoka kwangu.
* Na balozi Seif Ali Iddi achakuwa bias. Mbona hujaenda kumuona Fadhil Soraga mpaka leo? umeamua kwenda wewena Mohammed Aboud kumuona Padri na aila yake na wafuasi wake.
* Naomba tena hao makacherowaliokuja Zanzibar waanzie pale benki anapokwenda kuchukua ‘hela' padri huyuambaye pia ndiye signatory mkuu, benki xxxx! nendeni hapo mkaone transactionalizokuwa anazifanya padri huyo, na kama kuna bank reconciliationzinazokubalika - au shaghla baghala tu.
* Na kama je, hali ya makusanyona matumizi ya kanisa hili yanaridhia financial regulations za Tanzania,Zanzibar na bank of Tanzania. Check …kama kuna a kind of money laundry hapo?
Kwa ufupi matukio haya badoyamebaki kuwa kitendawili (unresolved mystery

Hivi Professor Jwan Mwaikusa si alishambuliwa hivi hivi? Nini kilifuata vile?
 
tatizo waikristo awana uwakika kuwa ni waislam na wanachotaka mapadri ni waislam wakamatwe na kupigwa mabomu ikiwa ivyo tanzania aitatulia
 
Back
Top Bottom