Ushamba wa PhDs na hatma ya Tanzania

Ushamba wa PhDs na hatma ya Tanzania

Nsimbi

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2014
Posts
1,091
Reaction score
1,204
Elimu ni jambo njema sana. Linamfanya mtu kufungua ubongo wake kwa mapana.
Hata hivyo elimu tu haitoshi linapokuja suala la uongozi. Katika qualities za uongozi bora elimu ya madegree na maPhDs sio sifa namba moja.
Ni kama magadi tu lakini sio chumvi kwenye mboga tunayoita hapa kwa jina la 'uongozi'.
Uongozi unataka mtu mwenye busara, uvumilivu, subira, maono, hekima, msimamo thabiti na heshima kwa wale anaowaongoza. Vitu hivi si lazima uvipate darasani.
Daktari lazima asomee udaktari ili afanye kazi ya udaktari. Vivyo hivyo kwa mwalimu, mhasibu, lawyer, mhandisi nk.
Vilevile katibu mkuu wa wizara lazima awe graduate. Sawa. Hata hivyo kusoma pekee na kujaza mavyeti hakumfanyi mtu kuwa waziri mzuri. Si lazima sana waziri kuwa na elimu ya juu sana kuwa waziri mzuri kwani yeye ni mwanasiasa tu na hategemewi kuingia 'jikoni'
Elimu pia haimfanyi mtu kuwa mbunge mzuri. Mara nyingine hekima na busara tu zinatosha katika uongozi wa siasa.
Hivi sasa umeingia 'ushamba' wa kudhani kuwa viongozi wenye PhD ndio hamira ya maendeleo nchini.
Historia ya karibuni inatuonesha kuwa kuna viongozi walifanya vizuri katika nafasi zao bila degree. Akiwa wizara ya mambo ya ndani, Mrema alifanya kazi nzuri na hakuna aliyevunja rekodi yake mpaka sasa. Hakuwa na shahada wala kishada. Mzee Mwinyi aliongoza nchi kwa busara na hekima kubwa bila kuwa na 'degree wala nini.
Elimu sio kila kitu. SUGU wa Mbeya mjini hana shahada ya chuo kikuu lakini ndio mbunge bora na anayependwa na wapigakura wake kuliko wote nchini.
Msukuma wa Geita hana hiyo degree lakini bungeni anaongea vitu vya maana kuliko wabunge wengi wenye masters!!!
Sumaye hakuhitaji kuwa na degree kuvunja halimashauri ya jiji la Dar lillilokiwa likilalamikiwa kwa rushwa na u Uswahili katika miaka ya 2000. Alifanya kazi nzuri.
Tujiulize wabunge au mawaziri wenye degrees wamefanya nini cha maana. Wame add value gani? Au wamezikimbia tu taaluma zao kifuata maslahi bungeni?
Mamlaka ziwe makini zinapompima mtu based on elimu pekee. Waende beyond vyeti. Kwa mfano haikuwa busara kuwatoa madereva wazoefu kazini eti kwa vile tu hawakuwa na chetu cha form 4.
Sioni mantiki ya kumwamini zaidi dereva mpya kwa vile tu amemaliza kipato cha nne ukamwacha mzoefu wa miaka 20!
Hii homa homa ya shahada na PhDs inahitaji vidonge. Shahada haikufanyi kuwa nesi mzuri zaidi kama huna wito na kazi hiyo.
Wala uprofesa haukufanyi kuwa waziri bora zaidi kuliko akina Mzee Kawawa kama sio mzalendo. Vyeti havifanyi kazi. Get out of the bottle!!!
 
Angalia wenzetu walioendelea , au tuje karibu , unaweza kukuta mbunge darasa la saba Kenya? Elimu ya juu ni muhimu ila political science iongezewe . Ukisimama mbele za watu usiwe na " infirioriry comlex" kwa kuwa kuna maprofesa . Yule mwenye kipaji cha uongozi aongezee na elimu ya juu angeshangaza ulimwengu .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angalia wenzetu walioendelea , au tuje karibu , unaweza kukuta mbunge darasa la saba Kenya? Elimu ya juu ni muhimu ila political science iongezewe . Ukisimama mbele za watu usiwe na " infirioriry comlex" kwa kuwa kuna maprofesa . Yule mwenye kipaji cha uongozi aongezee na elimu ya juu angeshangaza ulimwengu .

Sent using Jamii Forums mobile app
unajua raisi wa SA(zuma)na elimu gani,achana na hao wakenya wako.
 
Back
Top Bottom