Ushairi: Ngoma yaanza Kudunda

Idd Ninga

Verified Member
Nov 18, 2012
4,936
2,000
NGOMA YAANZA KUDUNDA

Alisema hii ngoma, hii ngoma ya zamani
Ngoma isiyo na noma, akatupa tumaini
Ngoma ya watoto jama, wakubwa mcheze nini
Ngoma yaanza kudunda, manju huyo kajificha.

Wajanja waliisoma, hii ngoma ya Uswini
Ngoma hii siyo kama, inadundia hewani
Wale waloitazama, walisema ni makini
Ngoma yaanza kudunda, manju anakula nduki

Wakanena tutakoma, haidundi sikioni
Kuiona hii ngoma, inadundia puani
Ili tutoke salama, tukimbie kilingeni
Ngoma yaanza kudunda, manju kaziba sikio.

Kwani manju akisema, wazee waseme nini
Akianza kunguruma, utadhani unazini
Kweli tumerudi nyuma, leo tupo Jerumani
Ngoma yaanza kudunda, balaa ni kijijini.

Wa Bantu atawatuma, ukisema hadharani
Waje wakupige vyuma, wakuchukue nyumbani
Nyoka sumu akitema, ajabu hajulikani
Ngoma yaanza kudunda, na manju hana habari.

Mkaidi hana jema, walisema majirani
Hii ngoma inauma, ikipigwa uwanjani
Mkigeuka makima, hatutazami usoni
Ngoma yaanza kudunda, manju karuka mbuyu

Ukweli hana huruma, apendacho hekaluni
Kule maisha daima, amepanga akilini
Sisi tukiliwa nyama, yeye kimya tu kitini
Ngoma yaanza kudunda, manju abugia kuku.

MTUNZI-Idd Ninga Tengeru Arusha
+255624010160
Iddyallyninga@gmail.com
 

Choveki

JF-Expert Member
Apr 16, 2006
451
250
NGOMA YAANZA KUDUNDA

Alisema hii ngoma, hii ngoma ya zamani
Ngoma isiyo na noma, akatupa tumaini
Ngoma ya watoto jama, wakubwa mcheze nini
Ngoma yaanza kudunda, manju huyo kajificha.

Wajanja waliisoma, hii ngoma ya Uswini
Ngoma hii siyo kama, inadundia hewani
Wale waloitazama, walisema ni makini
Ngoma yaanza kudunda, manju anakula nduki
……..
MTUNZI-Idd Ninga Tengeru Arusha
+255624010160

Iddyallyninga@gmail.com

Kongole wetu Malenga;

Kongole wetu malenga, utunzi wako mahiri

Ukweli umeulonga, na fumbo hilo la siri

Wengine wamejigonga, watazama editori

Ngoma sasa inadunda, twahitaji wetu manjuKongole hii ni yako, ipokee mikononi

Heko nyingi ni za kwako, kwa kubakia fanini

Ninalitoa tamko, fumbo lako li sirini

Ngoma sasa inadunda, twaulizanoa yu wapi?Kongole wetu mtunzi, ni fumbo lililo bora

Umetumia ujuzi, utadhani umechora

Haliko ki wazi wazi, maandiko yanang’ara

Ngoma sasa inadunda, ni wapi amefichama?Kongole nasema tena, pokea wangu mkono

Kwa mbali twapungiana, mita mbili siyo tano

Tusipige danadana, tunayaona maono

Ngoma sasa inadunda, twahitaji jemedari!Kongole namalizia, tano kwangu ni tamati

Kafichama avizia? asubiria umati?

Ni manju asiye nia, haulizi watafiti?

Ngoma sasa inadunda, halafu yuko kizani!!

Choveki

Mei, 2020
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom