Fikra Angavu
JF-Expert Member
- Jul 14, 2013
- 301
- 105
KITASA
Kitasa changu kibovu, chanitesa mwenzenu.
Chaniacha na makovu, tafuteni cha kwenu.
Kucha kutwa kichovu, mwakichokonoa chenu?
Basi vyenu viwe vyenu, na changu niachieni.
Choko choko ni hazishi, mpaka kimepwaya.
Hata Ngo! ngo! hambishi, pasi soni wala haya!
Usiku ni hatarishi, tena mrefu naugwaya.

Sie tupendao chongo, tunaitaga kengeza.
Nisiwe tu muongo, mwenyewe chanipendeza.
Nisiwe tu muongo, werevu mwakilegeza.

Washenzi mwaomba maji, na mengine mna mwaga.
Upole si ukosaji, mnilalie kama chaga.
Jama hii ni dibaji, mjue kwa babu Tanga.