Ushabiki wa Simba, Yanga waua mmoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushabiki wa Simba, Yanga waua mmoja

Discussion in 'Sports' started by Ab-Titchaz, Oct 22, 2008.

 1. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #1
  Oct 22, 2008
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ushabiki wa Simba, Yanga waua mmoja​


  2008-10-22 10:07:46
  By Happy Severine, PST, Mtwara

  Shabiki wa timu ya Yanga, ambaye ni mkazi wa Magomeni mjini hapa aliyetambulika kwa jina moja la Ndava (Mtumzima) anadaiwa alimpiga ngumi shabiki wa Simba, Salum Athuman (65) na kusababisha kifo chake.

  Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 10 jioni mtaa wa magomeni mjini hapa wakati mtuhumiwa pamoja na marehemu na watu wengine walipokuwa wanacheza bao.

  Kaimu Kamanda wa polisi mkoani hapa, Alfred Mnango akielezea tukio hilo ofisini kwake jana, alisema mtuhumiwa, ambaye anadaiwa kuwa ni shabiki wa Yanga ndio anadaiwa alianza kutoa lugha ya utani dhidi ya mashabiki wa Simba kutokana na timu hiyo kufanya vibaya hasa baada ya kufungwa 4-1 na Toto African ya Mwanza, Jumamosi iliyopita.

  Shabiki huyo aliendelea kujigamba kuwa Simba itasambaratika zaidi pale itakapofungwa na Yanga, Jumapili, maneno, ambayo yanadaiwa kumchukiza marehemu na ndipo alipoanza kupigana na shabiki huyo wa Yanga.

  ``Mzee Athumani alishindwa kuvumilia maneno ya mtani wake na ndipo alipoanza kupigana..... marehemu alipigwa ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake......watu waliokuwapo waliamua ugomvi huo...bila mafanikio.

  Muda mfupi baada ya ugomvi huo, shabiki huyo wa Simba, alianza kutokwa na povu mdomoni na hatimaye kufa hapo hapo.

  Mnango alisema uchunguzi wa awali wa kidaktari umeonyesha kuwa marehemu hakuwa na uvimbe wala michubuko mwili mwake, hata hivyo, uchunguzi zaidi unaendelea ili kujua kilichosababisha kifo chake.

  Mtuhumiwa alifanikiwa kutoroka na anatafutwa na polisi ili kujibu tuhuma zinazomkabili za mauaji na kwamba ametoa wito kwa raia mwema kutoa ushirikiano kwa polisi ili kufanikisha kukamatwa kwake.

  SOURCE: Nipashe

  Comment on this article


  http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/10/22/124894.html
   
Loading...