Ushabiki hewa wa wanachadema!

Marketer

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
261
55
Nawasalimia Wakuu!

Nimelazimika kuandika haya kutokana na ukweli kuwa kazi kubwa imefanyika ndani CDM ukilinganisha tulikotoka na tuliko. Pamoja na kazi hiyo tulioifanya na zinazoendelea kufanyika katika kuhakikisha CDM inachukua madaraka 2015 inanisikitisha kugundua kuwa watanzania wengi wameathirika na uwepo wa chama kimoja kwa miaka mingi, hata wale wadogo ambao walikuta mfumo mpya wamepokea athari kutoka kwa wakubwa zao.

Athari kubwa ni kuwa waoga wa kushiriki mambo ya siasa na wakiwa sio waoga wanakuwa passive wasio na msimamo, na wakiwa na msimamo basi ujue msimamo huo ni hewa! Sio siri CDM inapendwa na kukubalika haswaaa na vijana, ila ni mashabiki wangapi wa CDM ni wanachama halali wenye kadi? wanashiriki shughuli za kichama? wanahuzuria mikutano na wanachama hai? wangapi wamewahi kushiriki maandamano?

Utakuta mtu mnazi haswaa wa CDM ila siku ya maandamano anajibanza ila moyoni anaomba watu wafurike, na wakwanza kuangalia ITV kuona ilikuwaje?! kweli tutafika!?

2015 hiyooooo inakaribia, kwa mwendo huu hatutofika, tubadilike kwa kuanzia humu JF, jiulize una kadi ya CDM, tuache woga, mtu unamkuta online ni CDM damu ila ofisini akiulizwa we chama gani, anagwaya gwaya maana kusema GAMBA roho inamsuta, kusema yeye CDM anaogopa.

Anza kushiriki shughuli za chama mapema utapata nafasi ya kujua utendaji wa watu kiuhalisia, ili 2015 ukimpitisha mgombea unamjua kiundani. Inasikitisha sana kijana umemaliza chuo au six afu unakaa nyumbani unalia ajira hakuna, jiunge na chama wewe, utapata network na conections za kutokea, na hata exposure ya kimawazo.

Ni mimi

Mwanachama hai, mwenye kadi nashabiki halali wa CDM.
 
hao waoga hawajapata mwelekeo vuta subira mambo yanaenda yakibadilika siku hadi siku:israel:
 
Heading yako inatofautiana kidogo na habari yako bt nimekusoma' mi kadi ipo bhana.
 
Imani chanzo chake ni kuana na kuona huja kwa kusikia na kusikia huja kwa kuambiwa. Itatangaze chadema bila kuchoka mabadiliko utayaona usianze kulalama we need actions.
 
Imani chanzo chake ni kuana na kuona huja kwa kusikia na kusikia huja kwa kuambiwa. Itatangaze chadema bila kuchoka mabadiliko utayaona usianze kulalama we need actions.

sio kulalama mkuu, ishu sio kuwa watu hawana imani, imani wanayo sema ndo ule usitaki, nataka ndo unawasumbua, na woga tu kuwa watu wengi hawapo msitari wa mbele, kwanini nijitoe mhanga, sasa hii ndo mnajikita wote mmbebaki nyuma. Ukijitosa wewe, mimi na yule hapo ndo inakuwa mpango mzima.
 
Wasiokuwa na kadi na wako tayari kupata kadi kama wanachama wa CHADEMA basi waambiwe taratibu ya namna ya kuzipata ili wafanye hivyo. Mie yangu iko tayari kibindoni.

Hata humu JF wako wengi tu, kelele nyingi lakini hawana kadi za chama.
 
Tatizo siyo kuwa na kadi,tatizo uwoga wa kupiga kura!

Tatizo woga wa kujulikana wanachama, watu wanaogopa enzi zile ukijulikana tu sio wa itikadi za kijani na njano basi utaletewa mizengwe ya kufa mtu, kesi juu ya kesi mpaka ukoo utakuita kikako kukuuliza mbona untaka kujipoteza ungali mdogo, wacha hizo mambo bana.

Ukiwa ninja na ukamiliki kadi kupiga kura ni vry easy, unaweza kujikuta hata unakuwa muhesabuji kura.
 
Back
Top Bottom