Usanii wa CCM, sanaa ya CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usanii wa CCM, sanaa ya CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, Nov 10, 2011.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Kinachojiri hivi sasa hasa katika Jiji la Arusha ni matunda ya usanii uliotukuka wa Chama cha Mapinduzi,CCM.Wenye chama hicho wamejisahau.

  Wamesahau kuwa wale watu wa Tanganyika si hawa wa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.Usanii wa chama hicho 'tawala' umeruhusu sanaa kwa Chama kikuu cha Upinzani nchini,Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).Mkesha wa CHADEMA pale Arusha ni kati ya sanaa kali zinazotekelezwa vilivyo na CHADEMA.

  Kupitia sanaa za majukwaani(kama alizosoma Lowassa) CHADEMA inaendelea kujiimarisha,kujijenga.Watu wanaambiwa kweli,hali na jinsi wanavyotawaliwa. Wanaelewa. Ya heri siku ile Lema atakapotolewa rumande...sanaa tosha pia.
   
Loading...