Ukipenda damu basi usiache kupenda usaa japo sio mzuri ila utakufanya kuona jema kwenye baya. Huu ni mfano tu. Daima kupendana sio kufanana moyoni, hizi ni salamu zangu kwenu wachumba na wana ndoa. Ila tukumbuke kuwa ''ubaya ukiingia mlangoni , wema utolokea dirishani''. Kumuweka msaliti moyoni ni sawa na kuweka nafsi lehani, pole sana kwani inaumiza sana.
Heri maumivu ya mwili kuliko maumivu ya moyo. Pia ni bora kulala pekeako kuliko kulala na mtu anayelala na mtu mwingine moyoni. Usemi huu “once a cheater, always a cheater” ni wa ukweli lkn kumbuka kuwa kuna funzo ndani yake ktk kila usaliti, hivyo usikate tamaa.
USHAURI WANGU; Kamwe usipoteze muda wako kwa kumuombea mabaya msaliti wako uko anakokwenda, kwani kwa kufanya hivyo itakufanya ufuatilie maisha yake, kitu ambacho kitakufanya uendelee kuumia. Daima chuki umchoma mtu anayeiifadhi.
MWISHO:
(i) Ukimuacha mtu kwasababu ya mtu mwingine, usishangae naye kukuacha kwasababu ya mtu mwingine.
(ii) Kama wewe ni mwanandoa na huwa unafuta sms ili mume au mkeo hasizione, tambua kuwa wewe tayari ni msaliti wa kiwango cha Phd
NB: kusaliti ni sawa na kuchinja ng'ombe kwa oda ya maini.