Usaliti unapotokea ndani ya uchumba

Usaliti unapotokea ndani ya uchumba

husnan jumah

Member
Joined
Mar 13, 2013
Posts
5
Reaction score
0
Wana Jf,

Nipo na mtu wangu ambae nampenda sana na naamini na yeye ananipenda. Tupo katika mahusiano ya miaka mitano. Nimegundua sasa kuwa ana mtoto wa nje ya ndoa, habari niliyoipata wakati wa kutambulishana familia. Naomba mnisaidie mawazo ni nini cha kufanya? Niendelee naye ama ndiyo atazidi kunisaliti tukifunga ndoa?

Mawazo na ushauri wenu tafadhali.
 
Nakushauri endelea nae,muda ukifika mambo yote atayaweka wazi
 
Dah!pole sana miaka 5 ya uchumba its too much,inashauriwa kwa uchumba salama ikiwa haraka sana at least Mitzi 6 ya uchumba na isizidi miaka 2 ya uchumba,kwa jinsi mwanadamu alivyo kufanya kosa la kwanza ni vigumu lakini kurudia Kosa husika huwa ni rahisi.hivyo hilo tendo alilofanya anaweza ni rahisi kurirudia tofauti Kama angekua hajafanya hivyo,pia kwa Huyo mchumba wako anaweza kuanza uchumba na mtu mwingine kwake itakuwa rahisi kukitunza kiapo hicho kuliko kwako,pia in busara zaidi kuvunja uchumba kuliko kuvunja ndoa,fikiri kwa kina dada ktk hili wakati mwingine maamuzi magumu na yanayoumiza ndio sahihi......
 
wewe umenena relationship miaka mitano jamanii!!! ila wadaa mnajishusha thamani wenyewe.
 
Wana Jf,

Nipo na mtu wangu ambae nampenda sana na naamini na yeye ananipenda. Tupo katika mahusiano ya miaka mitano. Nimegundua sasa kuwa ana mtoto wa nje ya ndoa, habari niliyoipata wakati wa kutambulishana familia. Naomba mnisaidie mawazo ni nini cha kufanya? Niendelee naye ama ndiyo atazidi kunisaliti tukifunga ndoa?

Mawazo na ushauri wenu tafadhali.

Mtoto nje ya ndoa ya nani? Ina maana wewe unataka kuwa mke wa pili au? Sa kama utakuwa mke wa pili unaogopaje usaliti!?
 
Mungu nisaidie uchumba wangu usifike miaka 5.

Dah,mnatafuta nn miaka yote hiyo?..

Miaka mitano ni mingi sana kwa watu ambao kweli mlikuwa na mipango ya kuoana ningetarajia ww mwenyewe ungekuwa

umeshang'amua kwamba kwa hali ilivyo,namna alivyopata mtoto na kwann hakukwambia na tabia zake ambazo umemuona

nazo kwa muda wote huo utajua ni mtu wakukusaliti au anafaa kuwa mtu wako.

mm ninakushauri uendelee naye kadri ya majibu utakayopata baada ya kupata majibu ya hayo maswali hapo juu!..
 
Kwa maelezo yako ni kama hamjafunga ndoa bado mko wachumba sasa mbona unasema mtoto nje ya ndoa? Mi sijaelewa nashindwa kukushauri
 
Mtoto nje ya ndoa ya nani? Ina maana wewe unataka kuwa mke wa pili au? Sa kama utakuwa mke wa pili unaogopaje usaliti!?
Na mie nimeshangaa, maybe alishakujua wewe ni mtu wa kupanic, mtu kuwa na mtoto sio dhambi, as long as alimpata wakati hayupo na wewe, hilo jambo dogo sana binti mwenzangu
 
sasa kama alimpata kabla ya kuwa na uhusiano na ww?

nyie ndo mnaosababibsha watu kukataa kutonza watoto kwa kuogopa doa katika mahusiano yanayofuata.

kwa upande mwingine unafanya wanawake/wasichana kutoa mimba au kutopa watoto kwa kuogopa uzibe wakati wa kuolewa.

so usiachane nae, ila akuhakiishie hataanza / endeleza hayo mahusiano tena
 
Back
Top Bottom