Christopher Cyrilo
Member
- Oct 5, 2015
- 90
- 482
Usalama wa taifa haufanyi kazi ya kuteka raia wema. Hii si kazi ya usalama wa taifa. Wala si sehemu ya mafunzo ya kiintelijensia.
Raia wa nchi anapokwenda kinyume na sheria, hudhibitiwa kwa kufuata utaratibu wa kisheria. Kuteka na kutesa sio utaratibu wa kisheria, wala sio utaratibu wa taaisi ya usalama wa taifa.
Kwa hiyo tuache kuituhumu idara hii adhimu ya jeshi letu zuri la polisi. Tuache kuichafua na kuipaka matope idara ya usalama wa taifa. Si vema.
Cha kufanya ni kupambana, kwa maneno na vitendo, na kwa nguvu zote dhidi ya wapuuzi wachache wenye vitambulisho vya usalama wa taifa, walioajiriwa na usalama wa taifa, wanaofanya ndani ya ofisi za idara ya usalama wa taifa na wanaotumwa na watu wenye madaraka ndani ya usalama wa taifa, kufanya utekaji wa raia na hivyo kupandikiza hofu kwa wananchi na chuki kwa vyombo vya dola.
Nawahusisha watumishi wa usalama wa taifa moja kwa moja na vitendo vya utekaji kwa sababu moja kuu, sio kwamba mimi nina akili nyingi, No; Mimi sio mtoto. Ni watoto tu ndio wanaweza wasione uhusika wa watumishi wa usalama wa taifa katika vitendo hivi.
Utamaduni huu wa utekaji, sio tu unatia wananchi hofu ya muda mrefu na kuathiri utendaji kazi wao katika kujenga taifa, bali pia unapandikiza roho chafu za uasi kwa vijana wazalendo wanaolipenda taifa lao. Na vilevile vitendo hivi vinatoa mwanya kwa watu wengine wenye nia ovu, kufanya kuwateka maadui zao kwa imani kwamba watu watajua ni usalama wa taifa. Na kwa kuwa usalama wa taifa "unaogopwa", basi watekaji wengine wanaweza kuwa salama pia.
Rai yangu kwa taasisi ya usalama wa taifa, ni vema kuchukua hatua za haraka kuwandolea watu hofu. Panapo hofu hakuna ubunifu, hakuna amani, hakuna ustadi, hakuna maendeleo. Zaidi, kunaweza kuibuka vikundi vya uasi dhidi ya dola na vikapata kuungwa mkono na wananchi wengi walioguswa na maudhi ya kutekwa kwa ndugu, rafiki, viongozi na jamaa zao.
Ni vema kuchukua hatua kabla watu wenye akili hawajafanya uasi dhidi ya majuha wenye akili ndogo na madaraka makubwa yanayowaelemea.
[HASHTAG]#UjinganiDotCom[/HASHTAG]