Habari zenu wakuu, tunakutana tena kwa awamu nyingine baada ya JF kutoka mapumziko. Kama mada inavyojieleza ni kuhusu usalama barabarani, jeshi la polisi kitengo cha barabarani linafanya kazi kubwa sana lakini bila mafanikio. Tatizo lipo katika njia ya kutatua hili tatizo.
Trafiki wao wameegemea zaidi kulipisha madereva faini na adhabu nyingine wakiamini litakuwa ni suluhisho. Kinacho takiwa ni trafiki watoe elimu ya kutosha kwa madereva na wenye vyombo vya moto. Waweke vituo maalum barabarani kwa ajili ya kutoa elimu bila kumuadhibu dereva.
Mfano kwenda mikoani kuwe na vituo vya elimu kila mpakani mwa mkoa kutoka/ kuingia mkoa mwingine.Hii inaweza kusaidia kama sio kumaliza tatizo. Huwezi kumpa mtu adhabu halafu ndio umpe elimu hawezi kukuelewa maana tayari anahasira , hawezi kukuelewa. Matrafiki wengi barabarani wanajali adhabu zaidi bila kutoa elimu. Hayo ni mawazo yangu kama mdau wa barabarani.
Wengine wanaweza kuchanga mawazo pia