Usajili wa Humud Azam…

Achraf Hakimi

JF-Expert Member
Mar 3, 2010
873
1,773
Ukiwatizama Azam msimu huu ni mojawapo ya timu ambazo zimefanya usajili makini sana, wanaye mshambuliaji hatari Kipre Tchetche ambaye naamini hataifaidi Azam kwa umahiri wake tu bali hata kiuchumi kwa sababu ana uwezo unaoweza kushawishi vilabu vikubwa nje ya nchi kumnunua japo Azam wana mafedha ya kutosha. Ila katika usajili huo kuna walakini kidogo. Mwaka jana Azam waliipiga bao Simba kwenye usajili wa Patrick Mafisango, mchezaji ambaye ni muhimu sana kwenye timu yoyote kutokana na uwezo wake wa kucheza mpira na kumudu nafasi nyingi uwanjani . Lakini msimu huu Azam wamembadili Mafisango na mchezaji toka Simba Abdulhalim Humoud. Humoud ni mchezaji mwenye kipaji halisi ambacho hakipingiki .Ila msimu uliopita haukuwa mzuri kwake akiwa Simba na kiukweli uwezo wake umeshuka kwa asilimia Fulani. Wenzetu ulaya huzingatia baadhi ya vitu kabla ya kumsajili mchezaji , vitu hivyo ni historia ya mchezaji, uwezo wake wa kucheza pasipo kuumia kwa muda mrefu na cha muhimu kabisa ni mchango wa mchezaji husika kwa timu anayotoka . Hii inamaanisha alicheza asilimia ngapi ya mechi za timu yake, kama alicheza mechi pungufu ya asilimia sabini na tano lazima uhoji mara mbili kabla ya kumsajili. Humoud alicheza mechi chache sana akiwa na Simba msimu uliopita na hilo linanipa maswali mengi kuhusu aliyefanya uamuzi wa kumsajili Azam. Ukiachana na mchango wa mchezaji kwa upande wa mechi kuna uwezo halisi wa mchezaji , Mafisango ana uwezo wa kumudu nafasi zaidi ya mbili uwanjani, humoud yeye anacheza nafasi moja tu ambayo ni kiungo wa kati , ina maana kuwa Simba wamepata faida ya kuwa na mchezaji ambaye ni sawa na wachezaji watatu ndani ya mchezaji mmoja. Kwa kutazama usajili ulivyofanyika ni dhahiri siasa zinatawala kuliko ufundi , je soka letu litapiga hatua kwa mtindo huu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom