singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
SHIRIKA la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) kwa kushirikiana na Serikali Kuu limezindua mradi wa miaka mitano kutakaotekelezwa katika halmashauri 97 za mikoa 13 Tanzania ili kuimarisha mifumo ya Sekta za Umma Nchini (PS3).
Mikoa 13 ya Tanzania Bara ambako mradi utatekelezwa ni: Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, na Shinyanga. Mradi utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania. Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zinazonufaishwa na misaada ya maendeleo chini ya USAID, tangu baada ya kupata uhuru wakati huo ikiitwa Tanganyika na hata baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964.
Miongoni mwa miradi iliyoanzishwa kwa usimamizi wa USAID ni pamoja na Chuo cha Kilimo Morogoro ambacho sasa kinajulikana kama Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Chuo cha Utumishi wa Umma na vyuo vya ualimu k atika mikoa ya Dar es Salaam na Iringa. Mwaka 1973 Marekani iliifanyia marekebisho sheria ya misaada ya nje na sasa ili kusaidia kuboresha maisha ya watu masikini. Kwa Tanzania sheria hiyo inakusudia kuwasaidia wananchi hasa wa vijijini.
USAID ipo tangu wakati wa uongozi wa Rais John Kennedy wa Marekani na inafanya kazi kwa mujibu wa Sheria ya Kusimamia Misaada ya Nje ya mwaka 1961. Mpango wa USAID nchini ulianza kutambua umuhimu wa miradi ambayo ilenga katika nyanja zote katika mikoa na taifa hasa katika utamaduni, siasa na uchumi. Hivi karibuni, Usaid imezindua mradi huo wa kuimarisha mifumo ya sekta za umma nchini (PS3) na unaanza kutekelezwa katika mikoa ya Dodoma na Morogoro.
Mkoani Dodoma uzinduzi wa mradi huo umefanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa Songwe, Chiku Galawa. Watu 180 wameshiriki katika uzinduzi huo wakiwemo wakuu wa wilaya, Katibu Tawala wa Mkoa, wenyeviti wa Halmashauri, wakurugenzi wa halmashauri, wajumbe wa sekretarieti ya mkoa, na wajumbe wa timu ya menejimenti kutoka kwenye halmashauri.
Uzinduzi katika mikoa ya Mtwara, Mbeya na Mwanza utafanywa karibuni kabla ya kuendelea mikoa mingine kadri USAID walivyojipanga. PS3 inalenga kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya sekta za umma yakiwemo masuala ya utawala bora, rasilimali watu, fedha, utoaji wa taarifa, na tafiti. Ushirikiano huo wa PS3 katika ngazi ya Serikali Kuu na Halmashauri una nia ya kuboresha utoaji na matumizi ya huduma za umma, hususani kwa jamii ambazo hazijanufaika vya kutosha.
PS3 ni mradi unaofadhiliwa na USAID na utatekelezwa na mashirika saba ya kitaifa na kimataifa. Mradi huo utaimarisha mifumo katika ngazi ya taifa, mkoa na halmashauri. Mashirika hayo yatakayotekeleza mradi huo ni pamoja na Abt Associates Inc, ambaye ndiye mtekelezaji mkuu. Watekelezaji wasaidizi ni Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo cha Mafunzo ya Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI), Taasisi ya Ushauri Tanzania (TMA), Broad Branch Institute, Intra Health International na Urban Institute.
Mkurugenzi wa mradi huo, Dk Emmanuel Malangalila, anasema wanatarajia kuwa mradi PS3 utaimarisha utawala bora na ushirikishwaji wa wananchi. “Tunataraji mwisho wa mradi huu wa PS3 kuona uimarishaji wa utawala katika ngazi ya kitaifa na ya mamlaka za serikali za mitaa, ili kuweza kutumia rasilimali kwa uwazi, kuwezesha ushiriki wa wananchi katika kupanga, kufuatilia, na kutoa matokeo katika kila sekta,” anasema Dk Malangalila.
Anasema, mafanikio mengine yanayotarajiwa ni upande wa rasilimali watu ikiwa ni pamoja na kuwepo na ongezeko kwa kuzingatia usawa katika mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji wa huduma bora kwenye maeneo yenye uhitaji zaidi. Jambo lingine ni kuimarisha mfumo wa ajira pamoja na kudumu kwa watumishi katika ajira serikalini. Masuala ya fedha ni sehemu mradi wa PS3.
Ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za jamii, kuongeza ufanisi katika matumizi ya fedha za umma, na pia kuongeza uwiano kati ya kiasi cha fedha kilichotumika na mali iliyonunuliwa. Dk Malangalila anasema, mawasiliano ni sekta muhimu na kwamba kuimarisha mifumo ya utoaji taarifa iliyopo nchini ni jambo la msingi. Anasema pia kwamba, matumizi ya takwimu kwa wadau ni jambo la muhimu na linatarajiwa kuonekana mwisho wa mradi huo.
Katika kila jambo huwa kuna changamoto na ili kuzifahamu na kupata mbinu ya kuzikabili lazima ni muhimu kufanya utafiti. Dk Malangalila anasema tafiti kuhusu utekelezaji wa mradi ni muhimu, kwa kuwa zitasaidia kujua changamoto zinazojitokeza na kupendekeza mbinu za kuondoa changamoto hizo. Tafiti hizi zitasaidia kugundua fursa zilizopo na kuzitumia kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa. Pia tafiti hizo zitasaidia kuboresha maamuzi serikalini.