Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,300
- 25,920
Waungwana wa JF,nawasalimu.
Nikiri kuwa nimesukumwa kuandika uzi huu ili kuzuia upotoshaji unaojaribu kufanywa dhidi ya Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi. Nimeusoma uzi wa Mkuu Zawadi B Lupelo unamhusu Prof. Kabudi na kubaini kuwa uzi huo una upotoshaji mkubwa. Uzi husika ni ule uliopo humu ukimsihi Prof. Kabudi ajirekebishe ili asishindwe kama Waziri Mwakyembe. Hii ilifuatia majumuisho ya Prof. Kabudi Bungeni akijibu hoja za Wabunge katika bajeti ya Wizara yake.
Ifahamike mwanzo mwanzoni kuwa namfahamu Prof. Kabudi kwa kipindi kirefu kiasi. Nimemfahamu hasa kuanzia mwaka 2005 kama Mhadhiri wangu wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UD); Amidi (Dean) wangu wa Kitivo cha Sheria UD na baadaye kama mkuu wangu wa kazi Ofisi ya Mwanasheria wa Chuo na Katibu wa Baraza hapohapo UD hadi alipoteuliwa Mbunge na Rais. Kiufupi Prof. Kabudi si mtu aliyeelezwa na Mkuu Zawadi B Lupelo.
Mosi, kuhusu Uwakili wake, si kweli hata kidogo kwamba Prof. Kabudi alifanya mitihani ya Uwakili (Bar Examinations) mara kadhaa na kufeli. Prof. Kabudi aliomba kutofanya mitihani ya Uwakili(kuwa exempted) ili kusajiliwa kuwa Wakili na akakubaliwa. Jambo hilo si la ajabu. Majaji wote wanapostaafu na kuhitaji kusajiliwa kuwa Mawakili, huwa exempted kufanya bar examinations. Hatahivyo, Prof. Kabudi alisailiwa hata baada ya kupata exemption yake. Aliyemsaili alikuwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufani, Januari Msoffe.
Pamoja na kutohudhuria siku ya kusajiliwa kwake kuwa Wakili, Prof.Kabudi alisajiliwa kuwa Wakili mwaka 2009. Alikabidhiwa Vyeti vyake vya kiwakili Ofisini kwa Msajili wa Mahakama Kuu,wakati huo alikuwa Jaji John Utamwa. Sote kama wasomi wa sheria tunajua kuwa hakuna wadhifa Wakili wa Heshima (Honorary Advocate) kama ilivyodaiwa na Ndugu Lupelo. Kwahiyo, Profesa Kabudi asingeweza kupewa wadhifa wa Honorary Advocate usiokuwepo hapa nchini. Naamini kuwa ufaulu mkubwa wa Prof. Kabudi wa GPA ya 4.8 ya Shahada ya Kwanza ya Sheria ulichangia exemption yake katika mitihani ya Uwakili.
Pia, Prof. Kabudi hakusema Bungeni kuwa Uingereza na Israel hazina katiba. Alichosema ni kuwa Uingereza na Israel hawana katiba zilizoandikwa(written Constitution). Hata Zanzibar, kati ya mwaka 1964 na 1979 haikuwa na Katiba iliyoandikwa. Waungwana husikiliza kwa makini ili kuepuka kupotosha.
Kuhusu kauli yake ya "when law was law and President was President", Prof. Kabudi alikuwa akizungumzia muktadha wa uwepo wa Sheria ya kuweka watu kizuizini ya mwaka 1962 ambayo kwasasa haipo tena. Sheria hiyo ilimpa Rais mamlaka ya kumuweka mtu kizuizini bila kutoa sababu zozote na bila ya kuwekewa ukomo wa muda wa kumuweka mtu kizuizini. Hapo,Prof. Kabudi alilenga kuonyesha uthubutu wake wa kuandika na kusimamia alichokiamini.
Kwa tuliobahatika kufundishwa na kufanya kazi naye, Prof. Kabudi hana majivuno wala kiburi (arrogance). Kinachomtofautisha na wengine, kama ilivyo katika kuongea kwa watu, Prof. Kabudi huongea kwa msisitizo-neno kwa neno. Mara kadhaa alitusimulia kuwa alipokuwa mdogo alikuwa na kugugumizi na alifundishwa jinsi ya kukabiliana nacho kwa kuvuta pumzi na kutamka maneno kama afanyavyo. Yeye ni mtu mkweli, mnyenyekevu, msikilizaji na muelewa.
Waungwana, kusikiliza kwa makini na kujua kabla ya kusema au kuandika ni jambo jema. Tujijengee utamaduni huo.