Usahihi wa kodi ya benki na simu

Malilambwiga

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
485
296
Kumekuwa na uvumi mwingi juu ya ongezeko la kodi katika huduma za kibenki pamoja na miamala ya kutuma na kupokea pesa kupitia mitandao ya simu.

Ukweli ni kwamba kabla ya bajeti hii kupitishwa awali tozo katika bank ilikuwa ni Tshs.600/= pindi unapotoa pesa kupitia ATM. Kiwango hicho kimepanda kwa Tshs.108 na kwa sasa tozo au kodi hiyo itakuwa Tshs.708/=.

Juu ya kodi ya miamala ya kutuma na kupokea pesa kupitia simu ni kwamba awali mtu aliyetuma pesa alikuwa anatozwa VAT tu na kodi alikuwa anatozwa mpokeaji. Kwa utaratibu mpya sasa mtumaji na mpokeaji wote watalipa kodi kinyume na hapo awali.

Tulipe kodi ili nchi isonge mbele. Na iwapo hatutaki kulipa kodi tusitarajie maendeleo endelevu.
 
Back
Top Bottom