Acha uoga!
Kabla daraja la Kigamboni halijakamilika, tulikuwa tunavuka na boti za mbao pale Kurasini kwenda upande wa Kigamboni.
Sasa siku hiyo kamtumbwi kakaharibika injini katikati ya bahari. Weeh, nilidata maana hata maboya hamna.
Pia kutoka Same kwenda Simanjiro kuna kuvuka mto Ruvu wenye mamba kwa kutumia mtumbwi wa kusukumwa na fimbo ndefu. Kama una roho nyepesi huvuki. Nilivukaga siku moja, sijarudi tena mpaka leo.