Usafiri Dar es Salaam

cassianiogt

New Member
Oct 19, 2012
1
0
Ndugu zangu watanzania tumekuwa tukikabiliwa na ajari nyingi za barabarani na majini. Lakini bado naona atujajifunza kitu, leo asubuhi nilipanda daladala yaani lilikuwa limejaza mno kiasi cha kwamba pakusogeza mguu hakuna. Sasa hivi karibuni tu palitokea kuungua moto kwa basi la Dar express pale Segera Mkoani Tanga ambapo basi lote liliungua, kwa bahati nzuri watu walihimizwa mapema kutoka kwenye basi hilo na traffic( baada ya kusimamisha gari na kugundua pia lilikuwa likifuka moshi kwenye matairi. Angalizo langu ni kwenye madaladala hapa Dar es Salaam huu ujazaji wa abiria kiasi hichi si kizuri kwakua litakapo tokea tatizo la kuungua moto kwa daladala itakuwa tabu sana kuepusha vifo na majeraha kwa abiria kwa namna madaladala yanavyo jaa. Sijui Traffic wapo wapi na sijui kama awalioni hili. Sijui hile sheria ya "level seat" imeishia wapi?,Shime wa usika(traffic) na wananchi wote tuliangalie hili kwa makini. Vinginevyo tutakuja kusema tungejua tungefanyaga hivi au vile, wakati huo tumeshapoteza ndugu zetu au sisi wenyewe.
 
Acha hizo ww! yaan hata swala kama hilo unasubir trafk ndo aseme bas limejaa punguen mbak levosit enh? mbaya zaid na ww upo umoumo ndan ya hilo bas lililojaa kupita kias? ww uliliona limejaa kwnn usisubir lingne? ww pia unahusika na kujaa kw hilo basi!!
 
Back
Top Bottom