kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,784
- 20,155
Maafisa wa ngazi za juu wa idara za usalama na itelinjensia za Washington wamekiri kuwa Korea Kaskazini ina uwezo wa kuwaangamiza mamilioni ya Wamarekani iwapo itafanya shambulizi moja la silaha za nyuklia dhidi ya Marekani.
James Woolsey, Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na Peter Vincent Pry, Rais wa Kamisheni ya EMP (ectromagnetic pulse) iliyotwikwa jukumu la kupambana na tishio lolote la kielektroniki dhidi ya nchi hiyo wamesema kuwa, teknolojia ya Korea Kaskazini ni ya hali ya juu yenye uwezo wa kufyatua mabomu ya atomiki ndani ya ardhi ya Marekani.
Makala iliyochapishwa na jarida la The Hill imewanukuu maafisa hao wawili wa Marekani wakikiri kuwa, serikali ya Washington imekuwa ikitoa taarifa za kuwahadaa wananchi kuhusu uwezo wa kijeshi wa Korea Kaskazini, lakini ukweli wa mambo ni kuwa, Pyongyang ina uwezo wa kutumia mfumo wa kisasa wa kurusha makombora ya balestiki wa Intercontinental Ballistic Missile (ICBM), wenye uwezo wa kuua asilimia 90 ya Wamarekani.
Hivi karibuni Korea Kaskazini sambamba na safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson katika Peninsula ya Korea, ilifanyia majaribio mfumo wa kisasa wa injini za makombora yake ya balestiki, suala ambalo limewatia tumbojoto viongozi wa Washington na Seoul.
Hadi sasa Pyongyang imewekewa vikwazo mbalimbali na Umoja wa Mataifa kutokana na miradi yake ya nyuklia na makombora hatari ya balestiki.
source:radio tehran