USA sasa iko tayari kuzungumza na North Korea ikisitisha nuclear na ballistic missile tests.

herikipaji

JF-Expert Member
Aug 23, 2016
1,198
1,364
Marekani sasa kukubali kuzungumza na Korea ya Kaskazini endapo tu nchi hiyo yenye misimamo mikali juu ya uundaji na utengenezaji wa makombora ya masafa marefu ya kujilinda ya [ICBM - Intercontinental Ballistic Missile] yenye uwezo wa kubeba nuclear ikisitisha azma yake hiyo.

Haya yakifanyika mara baada ya nchi ya Korea ya Kaskazini kufanya jaribio la kombora la masafa marefu siku ya jumapili lililofanikiwa kusafiri umbali wa altitude 2000 plus Km na kutua baada ya umbali wa 700 plus Km.
Lakini kombora hilo linaeza kusafiri umbali wa 4500 Km kama linarushwa kwenye trajectory ya kawaida.
Kombora hilo linaitwa Hwasong-12 na linauwezo mkubwa kubeba vichwa vya nuclear kwa maelezo kutoka Pyongyang.

Maoni yangu binafsi:
Awali mgogoro huu ulipoanza kushika kasi wengine tulieleza humu Marekani hawezi kuthubutu kuvamia DPRK sababu anajua kitachomfika pale tu akiingia kwenye mipaka ya nchi hiyo.
Marekani bado inakumbuka vizuri alichivuna kule Vietnam na maumivu makali aliyoambulia bado hayajamuishia.

US: Ready for N Korea talks if it halts weapons tests
 
Marekani mwenyewe mbona ana test makombora? Yaani mmarekani hataki MTU ambaye hana uhusiano nae mzuri amiliki silaha Kali. Anaogopa kubondwa
 
Hiyo ni U.S old technique under new president, N/korea alishasema hawezi kufanya kosa alilofanya Iraq, yetu ni macho tu!
Ni kweli, wakati ule US walimwambia Saddam Hussein kuwa akitaka kuepuka vita baina yake na US ateketeze silaha zote za maangamizi, akateketeza. Baada tu ya kuteketeza zile silaha, US wakaingia vitani, ndiyo maana walimpiga Saddam kirahisi sana.
 
Back
Top Bottom