US recognize Israel's sovereignty over Golan Heights

Nimewaza kama wewe na nadhani wachache sana wanaweza kukuelewa: Lakini kule Crimea na Golan Heights kuna utaofauti kidogo. Warusi walivamia Crimea na kuvunja sheria za kimataifa lakini baadae wakaitisha kura ya ambayo asilimia 80% ya wananchi wa Crimea walikuali kujiunga na shirikisho la Urusi. Upande wa pili Golan Heights ilichukuliwa kimabavu na hakuna kura yoyote iliyopigwa kuwauliza wakazi wa pale kama wanataka kujiunga na Israeli.

NB: Ila yote yanafanyika hivi, huu ni mfano mbaya sana (A bad precedent) maana muda siyo mrefu mtasikia Uchina naye kavamia bahari ya Uchina Kusini (South China Sea) maana anasema asilimia 80% yote ilikuwa ni yake. Sasa sijui kama Marekani au Urusi wanaweza kumzuia kule Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa.
Mbona mchina alisha-annex Taiwan na Hongkong,haya mambo ni mwendelezo tu. Netanyahu anasema unapoanzisha uchokozi ili kumwangamiza mwenzako,akikucharaza na kupora ardhi yako,huna budi kukaa kimya. Uliyataka mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Automatically ataonyesha kuwa upande wa syria ila kiuhalisia ni israel typically
... Mrusi ni mnafiki sana. Kwa issues za Middle East publicly hujitanabahisha kuwa upande wa waarabu na Iran ila sirini ni Israel damu! Nahisi huenda hata baadhi ya siri za waarabu na waajemi Mrusi huvujisha kwa Israel.
 
Mbona mchina alisha-annex Taiwan na Hongkong,haya mambo ni mwendelezo tu. Netanyahu anasema unapoanzisha uchokozi ili kumwangamiza mwenzako,akikucharaza na kupora ardhi yako,huna budi kukaa kimya. Uliyataka mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Uchina hajawahi kufanya annexation ya Hong-Kong wala Taiwan kwasabu yale ni majimbo yake halali.
 
Mchina kasababisha mpaka nchi zetu nyingi huku Africa kutoitambua Taiwan isipokuwa Swaziland japo Marekani anaihami Sana Taiwan kidiplomasia na kijeshi ila sina uhakika kama itatokea Taiwan ikarejea kwenye himaya ya China kama Hongkong iliporejeshwa China na Uingereza.
 
Mkuu ni suala la muda tu, maana kama tokea mwaka 1972 sera ya Marekani imekuwa ni One China Policy na hata Trump na jehuri yake ameshindwa kubadilisha anajua kabisa kwamba ipo siku Taiwani itarudi Uchina.

Uingereza miaka yote alikuwa anatambua Tibet kama eneo huru nje ya Uchina lakini mwaka 2008 alijiunga na wenzake wa Umoja wa Ulaya kutambua kama Tibet ni sehemu ya Uchina. Hii ilitokea baada ya Uingereza kutambua kwamba anahitaji sana masoko na pesa za Uchina.

Taiwani ni suala la muda tu mkuu, hasa kipindi hiki ambacho Uchina imekuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi duniani na ya kijeshi kule Pasifiki kuliko kipindi chochote cha historia yake.
 
Mbona mchina alisha-annex Taiwan na Hongkong,haya mambo ni mwendelezo tu. Netanyahu anasema unapoanzisha uchokozi ili kumwangamiza mwenzako,akikucharaza na kupora ardhi yako,huna budi kukaa kimya. Uliyataka mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mchina ka annex Taiwan ipi hiyo?Taiwan ni jipu la China na mchina anafahamu hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ni suala la muda tu, maana kama tokea mwaka 1972 sera ya Marekani imekuwa ni One China Policy na hata Trump na jehuri yake ameshindwa kubadilisha anajua kabisa kwamba ipo siku Taiwani itarudi Uchina.

Uingereza miaka yote alikuwa anatambua Tibet kama eneo huru nje ya Uchina lakini mwaka 2008 alijiunga na wenzake wa Umoja wa Ulaya kutambua kama Tibet ni sehemu ya Uchina. Hii ilitokea baada ya Uingereza kutambua kwamba anahitaji sana masoko na pesa za Uchina.

Taiwani ni suala la muda tu mkuu, hasa kipindi hiki ambacho Uchina imekuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi duniani na ya kijeshi kule Pasifiki kuliko kipindi chochote cha historia yake.
Umenikumbusha mwaka 2008 kabla ya kuanza kwa mashindano ya Olympics huko China ambayo yalitanguliwa na ghasia za kisiasa huko Tibet kudai uhuru kutoka China ambapo nchi za magharibi ziliyabebea bango yale maandamano mpaka wengine wakapendekeza waendeshe kampeni za kususia hiyo michuano lakini baadae ulivyoibuka mdororo wa kiuchumi mwaka 2008 kwa mabenki makubwa kufilisika na baadae Mama Clinton alipozuru China katikati ya 2009 alipendekeza kwanza changamoto za kiuchumi za dunia zitatuliwe kwanza ndipo hali ya Tibeti ijadiliwe baadae na mpaka leo hamna jipya tena.
 
Halafu utakuta watu wanazurura huko marekani kudai demokrasia
 
Umenikumbusha mwaka 2008 kabla ya kuanza kwa mashindano ya Olympics huko China ambayo yalitanguliwa na ghasia za kisiasa huko Tibet kudai uhuru kutoka China ambapo nchi za magharibi ziliyabebea bango yale maandamano mpaka wengine wakapendekeza waendeshe kampeni za kususia hiyo michuano lakini baadae ulivyoibuka mdororo wa kiuchumi mwaka 2008 kwa mabenki makubwa kufilisika na baadae Mama Clinton alipozuru China katikati ya 2009 alipendekeza kwanza changamoto za kiuchumi za dunia zitatuliwe kwanza ndipo hali ya Tibeti ijadiliwe baadae na mpaka leo hamna jipya tena.
Hahahaha, daaah nimecheka sana!

Ndiyo maana nikasema hivi hata huko Taiwan ni suala la muda tu, wewe subiri. Hillary Clinton kwenye kampeni alipoulizwa kuhusu Getting Tough on China alisema haya "How can you get tough on your banker ??"

Mkuu, muda tu ndiyo utaongea wenyewe.
 
Back
Top Bottom