Usilamu na Mungu vimeingiaje kwene hii thread???lol
Ukiwa fanatic kila kitu ni KIZA KINENE.
Funny enough.Hii kadhia sijui inahusiana vp na 9/11.
Sasa hao askari wa kimerekani waliokuwa brainwashed wana tofauti gani na WEWE BLIND FOLLOWER.Actually,ninakujibu baada ya kukuondoa kwa muda kutoka kwene IGNORE LIST ili usijione ktk wenye ufahamu na hikma.
Nadhani unayetakiwa kuamka ni wewe. Wewe ambaye unadhani kuwa Wamerekani wanapigana vita dhidi ya dini fulani.
Wamerekani wangekwenda hata Brazil au Australia wakijua kipo wanachokitafuta huko, it is as
simple as that. Sasa niambie wewe al Qaeda bin Hizbullah, askari wa mungu mwenye uhitaji na shida ya kupiganiwa, wamerekani wanatafuta nini kule North Korea, nchi ya watu wasio na dini? Of course utaja nipa mfano wa Iran, ila blind-following inakufumba macho kujua ni kwamba Iran kinachotafutwa sio USILAMU. Kinachofuatwa kule ni mafuta, na IRAN ni nchi tajiri yenye hifadhi za mafuta. Hii nchi inaeza kuwa target kwa Wamerekani baada ya ku-secure reserves za Iraq na Saudia Arabia.
Kumbuka Iran ipo kwene top 30 kwa GDP kwa takwimu za mwaka jana.Ni taifa ambalo halijakubali rasilimali
zake zishikiliwe na mabeberu. Hio ndio sababu ya kuandamwa na katu sio USILAMU.
Sasa nani anastahili ku-amka hapa?
Sasa tunaweza kuzungumza au ndio utajificha kwa kuweka post zangu kwenye IGNORE LIST??.
Ni vipi? Hebu fanya ustaarabu uniambie ili nisipoteze muda wangu bure pasipo kusikilizana wakati wa kuambizana. Hizi tabia nyengine sisi hatujazoea, tafadhali wafanyie hao waliokufundisha. Sisi ni waTanzania?
Na vipi scenario hii: Taaliban walishaanzisha utawala wa kiislamu Afghanistan na misingi ya kuendesha mambo ya nchi sio kijamii tu, bali kisiasa, kielimu, kidola na kiuchumi nk kiislamu. Nchi jirani kama Pakistan ilishaanza kufuata mtindo huo huo. Kama kawaida walianza hivi katika humble means, na wao sio kama wanafiki wa Northern Alliance na wengineo wenje mtazamo wa ku-capitulate na mifumo ya kimagharibi na kusaliti uislamu. Unafikiriaje watu kama hawa wajaaliwe uwezo wa kiuchumi??? Huoni kwamba:
1. waMagharibi ingewabidi kama wanataka chochote kutoka pale basi ingewabidi waingie katika mikataba ya HALALI ya kibiashara badala ya exploitations walivyozoea?
2. Nani angefaidika kwa utajiri ulio katika ardhi ya waislamu kama sio waislamu??? Kumbuka hapa hatuzungumzii Iran (Aqeeda tofauti) au akina King Abdulla (puppets). Hapa tunazungumzia Taaliban.
3. Faida za nguvu zile kiuchumi zingekuwa na consequence gani kwa wezi wa kimagharibi? politically, economically, etc. Iwe sasa hivi au karne ijayo. Wapi nguvu zile zingesimama kwa mipaka na wakati??. Kwa taarifa yako Uislamu kama mfumo wa maisha haupo kufuata mfumo wa kimagharibi uliojaa dhuluma (RIBA) na udanganyifu (exploitation) bali ni m-badala wa mfumo huo na unasimama katika kunufaisha walimwengu kwa utajiri kutoka kwa Mola wao (ZAKAAT) na SADAKA zinazotolewa kwa kutaka ridhaa yake. Inaposimama system ya ZAKAAT katika masuala ya fedha na uchumi basi system ya USURY (Riba, Interest) hufa kifo cha kawaida. Uchumi wa western capitalism unategemea nini??? ZAKAAT ndio inayokusudiwa na Mola Muumba wakati Usury (Riba, interest) inakusudua na madhalimu wa kiMagharibi chini ya himaya ya Kizayuni.
4. Je wewe huna mtazamo au uoni wa kwamba madini yale kwa Afghnistan ambayo unalinganisha na utajiri mwengine wa natural resources walizonazo nchi kama Brazil, North Korea, Iran, nk zingekuwa na faida mbili za mapana na marefu tofauti?:
i)
ECONOMIC GAIN. Hii ni faida katika vipindi/mida miwili: a)
kipindi au muda mfupi: Economic gain ya muda huu kwa taarifa yako waMagharibi hawauogopi hata ukamatwe na nani ikiwemo na Afghanistani iwe chini ya serekali yeyote ile ya kiislamu ama la, kwa maana economic gain ya muda huu wanaweza kushindana (compete) nayo. b)
Kipindi au muda mrefu: Economic gain ya muda huu vile vile hawaiogopi sana kama itakuwa imekamatwa na watu ambao hawaonekane/hawana mtazamo ambao utaleta mabadiliko ya mfumo wa fedha na uchumi. Mkamato huu ndio wanaokuja nao China na other emerging economies, kwa maana kwa kuwa misingi ni ile ile ya kidhulumati (RIBA-Usury na exploitations) basi na wao wataendelea kuwemo, kulindwa, kushindana na kuimarika bila ya kulazimika kuanza upya (alifu kwa kijiti)
ii)
ISLAMIC GAIN: Tatizo wanalolihofu, wanalojaribu kulizima na ambalo kwa idhini ya Mola Muumba hawatoweza kufanikiwa, ni: 1. ECONOMIC GAIN YA MUDA MREFU 2. INAYOONGOZWA NA MISINGI YA KIISLAMU YA ZAKAAT NA SADAKA. Hii ndio sababu ya kuitengenezea ile "pretex" ya 9/11 Taaliban na siyo Brazil au North Korea au hata Saudi Arabia ijapokuwa unajua wewe hao wanasadikiwa kufanya hivyo ni raia wa wapi. Kwa misingi hiyo hiyo ijapokuwa wanajaribu kuitengezea Iran pretex, lakini hawana uhakika sana na wanachokihofu kwamba kipo Irani kuliko lilivyokuweko na Afghanistan ya TAALIBAN. Bomu ambalo halijakamilika na katika state ni rahisi kuli-suppress once and for all lakini sio rahisi ku-suppress movement ambayo inabarikiwa na economic power. Afghanistan Taaliban haikuwa tu ni dola bali ni movement.
Ultimately wanalolihofu ni UISLAMU na kwa mtazamo wao finyu wanafikiria ni uwezo wa kiuchumi peke yake ndio unaoweza kusimamisha nchi/utawala na kuendesha movement kufikia superpower. Historia ya uislamu haina haitegemei hivyo na tayari wameshajinasa hawa. Time will tell. Unanifahamu Abdulhalim au utanitia katika ignore list. Kama utafanya hivyo basi tafadhali fanya japo nusu ustaarabu unijulishe/nitangazie.