Urusi yatakiwa kuacha kumuunga mkono Bashar al-Assad

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Viongozi wa Marekani na Uingereza wamesema kuna fursa ya kuishawishi Urusi kuacha kumuunga mkono kiongozi wa Syria, Bashar al-Assad.

Katika mazungumzo kupitia njia ya simu jana, Donald Trump na waziri mkuu wa Uingereza Theresa May, wamesema ushirika na serikali ya Syria hauna manufaa tena ya kimkakati kwa Urusi.

Ikulu ya Marekani imesema chancellor wa Ujerumani, Angela Merkel, amekubali kwamba Rais Assad sharti ashtakiwe.

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa yanayoongoza kwa viwanda duniani maarufu kama G7 wanafanya mkutano wa siku mbili nchini Italia kujaribu kuja na mkakati wa pamoja kuhusu Syria kabla ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani jijini Moscow hii leo.

Wakati huo huo, Marekani imesema imeharibu asilimia ishirini ya ndege za kivita za Syria katika shambulizi la wiki iliyopita, ambalo imeanzisha baada ya kubaini kufanyika kwa shambulizi la silaha za kemikali.

Waziri wa ulinzi wa Marekani, James Mattis amesema serikali ya Syria haina uwezo wa kuziweka mafuta ndege zake au kuziongezea silaha katika uwanja wa Shayrat.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer ametahadharisha kwamba, Marekani haitasita kufanya shambulizi iwapo itabainika kutumika kwa silaha la kemikali.

Syria imekataa kutumia silaha hizo huku Urusi ikiielezea hatua hiyo ya Marekani kuwa haina athari yoyote na ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa.

Chanzo: BBC
 
Na usa na vibaraka wake waache kuingilia masuala ya nchi zingine wabaki makwao na majeshi yao siyo kila siku kuchokonoa nchi za watu rejea Iraq Afghanistan Libya mpaka leo kunawaka moto waarabu demokrasia ni ngumu sana kwao hawa walishazoea kuongozwa kwa mkono wa chuma huoni saudia pako kimya ila pakichokonolewa mbona hapatakalika
 
Km masaa 4 wameharibu 20% ya uwezo wa kijeshi wa Syria...............Najaribu kuimagine wakitumia siku nzima Syria itakuwaje....
Achana na wamarekani.....Warusi wachumba tu
 
Nchi za kiarabu ziamke. Kama walianza na Iraq,Afghanistan, Libya na sasa Syria basi wote watakwisha. Wanapunguzwa nguvu polepole. Mwisho wakimalizwa Misri na Iran then kushinei.

Waanzishe jihad dhidi ya maharamia ya magharibi
 
Km masaa 4 wameharibu 20% ya uwezo wa kijeshi wa Syria...............Najaribu kuimagine wakitumia siku nzima Syria itakuwaje....
Achana na wamarekani.....Warusi wachumba tu
Porojo hizo! Masaa kadhaa baada ya shambulizi la marekani, syria iliushambulia tena kwa ndege ule mji iliodaiwa kuushambulia kwa kemikali! Na marekani kula kona!
 
Marikano hawezi pekeake bila msaada. Mutakuja kuniambia
Msaada wa nani?!,jiulize kwenye vita zote ambazo NATO imeshiriki US huwa anachangia asilimia ngap ya vifaa na wanajeshi. Hpo utapata jibu lako.
 
Kumwambia Mrusi aachane na syria ni sawa na kumwambia marekani aachane na Korea ya kusini! Nid kitu kisichowezekana!
Pwani ya syria ni strategic position kwa Urusi kivita! Ana meli zake za kivita hapo! Na hiyo ndo hofu ya marekani!
 
Nchi za kiarabu ziamke. Kama walianza na Iraq,Afghanistan, Libya na sasa Syria basi wote watakwisha. Wanapunguzwa nguvu polepole. Mwisho wakimalizwa Misri na Iran then kushinei.

Waanzishe jihad dhidi ya maharamia ya magharibi

Umeona eeeh?...jinsi nchi za weusi zilivyomalizwa Afrika,Haiti,Jamaica n.k............hawaoni hawa!
 
Km masaa 4 wameharibu 20% ya uwezo wa kijeshi wa Syria...............Najaribu kuimagine wakitumia siku nzima Syria itakuwaje....
Achana na wamarekani.....Warusi wachumba tu

With 220,000 active persoell, 4,950 tanks and 473 aircraft unaamini kabisa 20% ya hivyo vyote ilikuwa pale walipohit na tamahawk zao?
Lest's see the stats here;
1. 20% ya 220,000 personell = 44,000 personnel (Iliripotiwa wamekufa watu 7 tu)
2. 20% ya 4,950 tanks = 990 tanks (Hakukuripotiwa kuharibiwa kwa tank yeyote)
3. 20% ya 473 aircraft = 94 aircraft (Iliripotiwa kuwa ni ndege 6 zilizokuwa kwenye m
atengenezo ndizo zilizoharibiwa)
Tumeona picha ndege kama Nane zilizokuwepo pale uwanjani hata hazijalipuliwa. Uwanja wenyewe umeharibiwa kidogo sana, afu mtu anasema ameharibu 20% uwezo wa kijeshi wa Syria. Maana yake ameharibu 20% ya (Personnel + Tanks + Aircrafts etc) afu mtu bado unaamini kikondoo tu bila hata kureason. Hii nchi ndo maana ipo hapa ilipo sababu ya kumeza kila kitu kama kilivyo.

Nalog off.
 
Asee ndugu usipanic
Wajua tena kila watz 4 kuna 3 mabashite na vilaza.
 
Kwani huyi USA NA NATO kama wanauwezo si waamue tu kumsambaratisha ASSAD kumuomba omba urusi kuwa akubali hiki mara kile yote ni wekness tu.
Shida ya nini si wanajiamini waanze kumtoa
 
Kwani huyi USA NA NATO kama wanauwezo si waamue tu kumsambaratisha ASSAD kumuomba omba urusi kuwa akubali hiki mara kile yote ni wekness tu.
Shida ya nini si wanajiamini waanze kumtoa
Mkuu hilo jambo sio la mchezo mchezo kabisa...

Usitegemee kama tutakuja kuona wasakata kubumbu pale Old Trafford na kule Bernabeu bhanaaa
 
Back
Top Bottom