Urusi yapuuza wito wa mkutano kati ya Putin na Zelensky

Urusi yapuuza wito wa mkutano kati ya Putin na Zelensky

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Ikulu ya Urusi imepuuzilia mbali mazungumzo ya kufanyika kwa mkutano kati ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin, na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, licha ya wito uliotolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump, akihimiza viongozi hao kukutana ili kujadili kumaliza vita nchini Ukraine.

Shinikizo la kufanyika kwa mazungumzo hayo linakuja baada ya Trump kukutana na Putin mjini Alaska wiki iliyopita, na kisha kuwakaribisha viongozi saba wa Ulaya pamoja na Zelensky katika Ikulu ya White House siku ya Jumatatu.

Soma pia: Nchi za Ulaya zazindua mkutano wa kusaidia ujenzi wa Ukraine

Screenshot 2025-08-20 002641.png

Trump alikiri mzozo huo ni "vigumu" kusuluhisha, huku akionya kuwa huenda Rais Putin hakutaka kumaliza uhasama. “Tutajua kuhusu Rais Putin katika wiki kadhaa zijazo. Inawezekana kwamba hataki kufanya makubaliano,” alisema Jumanne. Aidha, aliongeza kuwa Putin anapitia “wakati mgumu” bila kutoa maelezo zaidi.

Siku ya Jumatatu, Putin alimwambia Trump kuwa yuko “sawa” na wazo la mazungumzo ya moja kwa moja na Ukraine, lakini siku iliyofuata Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, alilitupilia mbali pendekezo hilo, akisisitiza kuwa mkutano wowote lazima utayarishwe hatua kwa hatua kuanzia ngazi ya wataalam.

Dmitry Polyanskiy, Naibu Mwakilishi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, alikiambia chombo cha habari cha BBC kuwa “hakuna mtu aliyekataa” uwezekano wa mazungumzo ya moja kwa moja, lakini akaonya kuwa “haipaswi kuwa mkutano kwa ajili tu ya mkutano uwe umefanyika.”

Wakati huo huo, taarifa zilidai kwamba Putin alipendekeza kwa Trump kuwa Zelensky asafiri hadi Moscow kwa mazungumzo, pendekezo ambalo Ukraine ilikataa mara moja. Wachambuzi wanasema hatua hiyo inaweza kuwa mbinu ya Urusi kuweka sharti lisilowezekana ambalo Ukraine haiwezi kulikubali.
 
Attachments

  • Screenshot 2025-08-20 002641.png
    Screenshot 2025-08-20 002641.png
    341.1 KB · Views: 27
Putin alisema, hawezi kukutana na mtu ambaye muda wa urais wake umeisha ikulu. Akasema, mpaka uchaguzi ufanyike Rais halali apatikane kikatiba nchini Ukraine 🇺🇦 ndio atafanya mzaungumzo maana baadae Ukraine 🇺🇦 itakataa kwamba aliyefanya makubaliano hakuwa Rais kikatiba
 
Anacho kisema Putin yupo sahihi kabisa, Zelensky alikuwa anapashwa kuwa umeitisha uchaguzi mpya tangu mwezi wa tano lakini anafanya kila mbinu ili aendelee kubaki madarakani,na anajua wazi kwamba hata akiitisha upigaji kura hawezi kushinda, hivyo anendelea kutoa visingizio kwamba taifa hivi sasa bado lipo vitani kwa hiyo sheria ya Emergency ndio iendelee kutumika mpaka hapo baadae hali ikiwa shwari, mpaka lini?? Mungu ndiye anayejua!!
 
Ikulu ya Urusi imepuuzilia mbali mazungumzo ya kufanyika kwa mkutano kati ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin, na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, licha ya wito uliotolewa na Rais wa Marekani, Donald Trump, akihimiza viongozi hao kukutana ili kujadili kumaliza vita nchini Ukraine.

Shinikizo la kufanyika kwa mazungumzo hayo linakuja baada ya Trump kukutana na Putin mjini Alaska wiki iliyopita, na kisha kuwakaribisha viongozi saba wa Ulaya pamoja na Zelensky katika Ikulu ya White House siku ya Jumatatu.

Soma pia: Nchi za Ulaya zazindua mkutano wa kusaidia ujenzi wa Ukraine

View attachment 3446920

Trump alikiri mzozo huo ni "vigumu" kusuluhisha, huku akionya kuwa huenda Rais Putin hakutaka kumaliza uhasama. “Tutajua kuhusu Rais Putin katika wiki kadhaa zijazo. Inawezekana kwamba hataki kufanya makubaliano,” alisema Jumanne. Aidha, aliongeza kuwa Putin anapitia “wakati mgumu” bila kutoa maelezo zaidi.

Siku ya Jumatatu, Putin alimwambia Trump kuwa yuko “sawa” na wazo la mazungumzo ya moja kwa moja na Ukraine, lakini siku iliyofuata Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, alilitupilia mbali pendekezo hilo, akisisitiza kuwa mkutano wowote lazima utayarishwe hatua kwa hatua kuanzia ngazi ya wataalam.

Dmitry Polyanskiy, Naibu Mwakilishi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, alikiambia chombo cha habari cha BBC kuwa “hakuna mtu aliyekataa” uwezekano wa mazungumzo ya moja kwa moja, lakini akaonya kuwa “haipaswi kuwa mkutano kwa ajili tu ya mkutano uwe umefanyika.”

Wakati huo huo, taarifa zilidai kwamba Putin alipendekeza kwa Trump kuwa Zelensky asafiri hadi Moscow kwa mazungumzo, pendekezo ambalo Ukraine ilikataa mara moja. Wachambuzi wanasema hatua hiyo inaweza kuwa mbinu ya Urusi kuweka sharti lisilowezekana ambalo Ukraine haiwezi kulikubali.
Kiakili tu unaongea nini na Zelensky wenye Vita kwasasa wengine sio yeye Zelenksy mwenyewe anaogopa kuuwawa ikiwa ataenda kivingine na wenyevita yao!! Ile Vita ishakuwa kitanzi kwake mwenyewe analidwa na Jeshi la Nato ukizingua wanazingua!!!
 
Cha kuchekesha ni kwamba,

Washirika wote WA Ukraine walioshinikiza hii vita uanze,

(Tena Kwa ahadi na Tambo kedekede)

Ndo hao hao sahivi wanahangaika na suluhu ili vita hii iishe🤣

MIMI KAMA SHABIKI KINDAKI NDAKI WA RUSSIA BLOCK,

Napendekeza waendelee kupasuana, mnyonge ajulikane

TUMEPOTOSHWA SANA KHS UWEZO WA RUSSIA KIVITA.

SAHIVI KILA KITU KIKO HADHARANI.

Viongozi WA NATO an EU saivi wamegeuka Vituko,

HAWANA NURU KABISA KWENYE NYUSO. ZAO KWA KKINACHOENDELEA VITANI
 
Na update ya Jana,

Ni kwamba Ukraine na urusi wamefanya mabadilishano ya miili ya wanajeshi wao walokufa VITANI

Ukraine kakaabidhi miili 19 ya wannaajeshi wa urusi,

urusi akikabidhi miili 1031 ya wanajeshi Wa Ukraine

NADHANI KWA HALI HII,
UKRAINE NA WASHIRIKA WAKE,
WANAZO SABAABU ZA MSINGI ZA KUHANGAIKIA SULUHU YA HII VITA.
 
1000078461.jpg

🇵🇱 Poland has announced that it will not send military to Ukraine, citing the risk of weakening its own armed force and fear of Russia’s retaliation against them.
According to Politico magazine, Warsaw has the largest army in the European Union, but its authorities refuse to compromise its combat capacity. For now, Poland is limited to offering logistical assistance for missions in the east, without direct deployment of troops. 😱😱🇷🇺
 
View attachment 3447519

Sahivi eti Poland nae hataki kupeleka wanajeshi,

Wakati nakumbuka NATO nzima waliowahi peleka wanajeshi wao nchini Poland Kwa ajili ya mazoezi ya pamoja.

Kitu ambacho kiliashiria kua NATO wanajiandaa kuingiza vikosi rasmi Ukraine

Aisee, saivi Kila mNATO anaihofia Russia😄

Makubaliano na Vikao vyao sahivi Kila mtu kaamua kupambana kivyake na raia wake
 
View attachment 3447519
🇵🇱 Poland has announced that it will not send military to Ukraine, citing the risk of weakening its own armed force and fear of Russia’s retaliation against them.
According to Politico magazine, Warsaw has the largest army in the European Union, but its authorities refuse to compromise its combat capacity. For now, Poland is limited to offering logistical assistance for missions in the east, without direct deployment of troops. 😱😱🇷🇺
Poland Authority are scared of returning their fellow country men in body bags.
 
Mwanzoni kila siku alikua akiua 2000+ ila kwa sasa wanajeshi wa Ukraine wamepungua mno ndio maana idadi imeshuka 🤣🤣
Yes, kweli kabisa, pia ndio maana unaona sasa hivi zelensky antaka kula matapishi yake mwenyewe baada ya kutia saini decree ya kutokufanya mazungumzo na Russia 🇷🇺, ila sasa analilia mazungumzo
 
Yes, kweli kabisa, pia ndio maana unaona sasa hivi zelensky antaka kula matapishi yake mwenyewe baada ya kutia saini decree ya kutokufanya mazungumzo na Russia 🇷🇺, ila sasa analilia mazungumzo
Zamani Zelensky alikuwa anakalilishwa na viongozi wa EU na Uingereza specifically Uingereza na Ufatansa nini cha kusema kwenye majadiriano ya kisitisha vita baina ya Ukraine na Urusi, Viongozi hao wa Ulaya walikuwa Wanamvimbisha kichwa kweli kweli Zelensky ndio maana siku moja aliwahi kudriki kumfokea hata Trump, halafu baadae Rais wa Ufaransa (Macron)
akamsaidia Zelensky ku-draft barua ya kumuomba msamaha Trump, yote hayo yanajulikana ndio maana Trump hawawekei maanai viongozi wa Ulaya ,amekwisha wajua kwamba ni wanafiki sana na walaghai, lengo lao ni kuhujumu juhudi za Trump za kusitisha vita huko Ukraine, wanampiga vita vya chini chini Trump kwa sababu hawataki amani ya kweli nchini Ukraine ili viwanda vyao vya kuunda silaha viendelee kuneemeka. kutokana na umwagaji damu wa wanajeshi na raia nchini Ukraine na Urusi.

Juzi hapa database ya jeshi la Ukraine inayo ratibu idadi ya vifo na majeruhi ya wanajeshi wa Ukraine kwenye uwanja wa vita ilikuwa hacked na wataalamu wa tehama na kubaini kwamba mpaka hivi sasa idadi ya vifo na majeruhi nchini Ukraine imefikia million 1.5 walitoa majina na picha zao !! Wanajeshi wa Ukraine wanakufa kama kuku ndio maana Zelensky amekataa kupokea idadi kubwa ya wanajeshi wake walio fia vitani eti "anaogopa kulipa fidia kwa familia zao, huyu ni kiongozi wa aina gani hasiye na UTU??

Looking back now, nina uhakika kwamba Viongozi wa Ulaya wanao taka kulazimisha wanajeshi wao na raia eti "waende kulinda amani nchini Ukraine baada ya vita kusitishwa" naona baada ya kushuhudia idadi kubwa ya makonteina na makonteina ya maiti za wanajeshi wa Ukraine zikiletwa mpakani mwa Ukraine na Urusi ili zichukuliwe za Serikali ya Zelensky na kuzisambaza kwa familia zao, wakati
huo idadi ya wanajeshi wa Urusi waliofia vitani ikionekana ni ndogo sana ukilinganisha na Ukraine, binafsi nina imani kwamba Viongozi hao wa Ulaya hawatakuwa na hamu tena ya kutaka kuwatoa kafara wanajeshi wa mataifa yao. Mpaka sasa bado hawajakubaliana wafanye nini wahache nini, kuna wanao kubali kuchangia uwepo wa wanajeshi wao nchini Ukraine eti "kwa lengo la kuratibu amani" kuna mataifa mengine hapo hapo Ulaya yamekataa katu kwamba hawatachangia chochote kwa kile wanacho kiita kudumisha amani, now the ball is in Ukraine Authority - wasuke au wanyoe na Urusi inawasubiri wafanye upuuzi WAO wa kuwapeleka Wanajeshi eti "wa kulinda amani nchini Ukraine" bila ya ridhaa ya Urusi/Putin nawahakikisheni kwamba wanajeshi wa EU, Uingereza na mamluki wakifanya mchezo wa kuchezea shurubu za Putin watapukutishwa kweli kweli, yetu macho.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom