Urusi yajipanga kulipa kisasi Marekani

Urusi yajipanga kulipa kisasi Marekani

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Ofisa mwandamizi katika Ikulu ya Kremlin amesema Urusi inalazimika kulipiza kisasi kwa hatua ya Marekani kushikilia mali za wanadplomasia waliofukuzwa mwaka jana kwa madai ya kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani.


Konstantin Kosachev alisema jana kwamba licha ya kuwatimua wanadiplomasia mwaka jana, Marekani bado inashikilia majengo mawili ya maofisa hao.
"Katika mazingira haya, sasa inaonekana Urusi haina chaguo: ni wakati wa kulipiza kisasi. Hili halitakuwa chaguo letu na hizi zitakuwa hatua za kushurutishwa, lakini lazima zifuatwe,” alisema Kosachev.

trump.jpg

Kosachev alisisitiza kwamba kauli iliyotolewa na Ikulu ya White House ni uthibitisho wa Marekani wa kutoheshimu sheria za kimataifa na akataja kuwa ni "jaribio la kukuza dhana ya sheria za taifa kwanza dhidi ya zile za kimataifa."

Sasa kumekucha!
 
Marekani inajifanya kamungu kadunia, i wish litokee taifa liifundishe adabu Marekani ili ipate adabu.
 
Hamna kitu kama hicho, majuzi tu wamekutana uso kwa uso Trump na Putin na kukenuliana meno na ahadi kibao za kukuza ushirikiano baina yao alafu leo tamko kama hilo lifanye kazi!? Not to that extent

from Katesh using Siemens C55
 
haijashikwa nyumba hapo mama limeshikiliwa taifa kwa sababu diplomat alikua anakaa hapo...ndo sheria za kimtaifa hizoo


Nikafikiri ziliachwa nyaraka nyeti humo kama zinavyokuwa office za ubalozi, kisasi kitacholipwa, Mrusi nae anaweza kufukuza US diplomats kusawazisha mchezo.
 
Back
Top Bottom