Urusi yagoma kurejesha maeneo ya Ukraine

Urusi yagoma kurejesha maeneo ya Ukraine

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov amesema kwamba Urusi haitakubali kurejesha ardhi iliyokwisha itwaa kutoka Ukraine katika mazungumzo ya kutafuta amani yanayotarajiwa kufanyika leo katika jimbo la Alaska nchini Marekani baina ya Rais Donald Trump na Rais Vladmir Putin.

Akizungumza katika mahojiano na Kituo cha CBS, Lavrov alikataa wazo la makubaliano yoyote ya kimaeneo katika usitishaji vita unaoweza kutekelezwa na Marekani, akidokeza badala yake Urusi inaweza kukubali kusitisha vita katika mstari wa mbele iwapo silaha za Magharibi zitasitishwa kupelekwa Ukraine.

Soma pia: Urusi yafanya mashambulizi makubwa ya anga nchini Ukraine

Screenshot 2025-08-15 065225.png

Tayari Rais wa Marekani, Donald Trump ameoneshwa katika vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa akijiandaa kukutana na Rais wa Urusi, Vladmir Putin katika juhudi za kusaka amani na kusitisha vita baina ya Urusi na Ukraine.
 
Endapo Russia itaamua kukomaa kuendelea na vita basi mwisho wa siku ni yenyewe ndio itatakuja kupoteza kwani uchumi wao hautaweza kustahimili vita visivyo na mwisho.

Yale mataifa yanayonunua mafuta na gesi yao kwa bei ya chini yakibanwa vizuri Russia hatakuwa na ujanja ni lazima atafyata tu.
 
Mwisho wa hii VITA ni Kifo/Anguko la kiutawala kati ya PUTIN au Zelensky.

Kwa sababu mashart ya kusitisha mapigano, hayakubaliki kwa pande zote mbili
 
Endapo Russia itaamua kukomaa kuendelea na vita basi mwisho wa siku ni yenyewe ndio itatakuja kupoteza kwani uchumi wao hautaweza kustahimili vita visivyo na mwisho.

Yale mataifa yanayonunua mafuta na gesi yao kwa bei ya chini yakibanwa vizuri Russia hatakuwa na ujanja ni lazima atafyata tu.
Ndoto nyevu hii
 
Wewe unajuaje kwamba Uchumi wa Urusi hauwezi kustahimili vita vya muda mref?? Hivi una habari hivi sasa Uchumi wa Russia ni wa kiwango gani kulinganisha na Uchumi wa mataifa ya magharibi ambayo uana chuki binafsi na Urusi yenyewe.

Nataka nikumbushe kwa mara nyingine tena, kwamba Urusi ni Taifa kubwa lenye uwezo wa kila aina, haiwezi kutishwa au kitukishwa na Taifa lolote hapa Duniani, Urusi itaendelea tu kutetea maslahi ya jamaa zao wa Ukraine ya majimbo ya kusini mashariki mwa Ukraine ambao wamekwisha pitisha referendum ya kukubali kwa asili mia mia kuungana tena na mother Russisa kama zamani let what comes may, West na USA na media zao watasema mengi na propaganda zenye lengo la kuiponda Urusi lakini watu wenye akili timamu wanajua ukweli huko wapi na ni upi, kama suala la kuikomalia Urisi eti "irudidhe aridhi iliyo iteka vitani" basi. USA ndiyo ianze kuonyesha mfano mzuri kwa kurudisha aridhi/kisiwa cha Hawaii kwa wenyeji/wazawa, kisiwa kilicho kilicho porwa na USA kwenye miaka ya 1800s kwa kumpodua/ondoa madarakani Queen aliye kuwa anatawala kisiwa hicho jambo hilo huwa halisemwi hata kidogo, USA pia warudishe kisiwa cha Diego Garsia kwa wenyeji walio hamishwa kinguvu kutoka kisiwani humo ,warudishe pia na Costa Rica na kisiwa cha Guamu nk, sio tuna anza kuwalahumu lahumu Warusi tu bila ya kuangalia upande wa pili wa Shillingi.

Mataifa ya magharibi specifically the USA hawana moral Authority ya kuanza kuwapa somo mataifa mengine wafanye nini waache nini wakati historia ya nyuma inadhilisha kwamba wao hawana mfano mzuri wa kuigwa kwenye masuala ya Geopolitics, kama bado wanataka ku-entertain mpango wao wa siku nyingi wa kutaka kusambaratisha Urusi basi, mataifa ya magharibi pamoja na kinara wao Merikani wakae wakijua kwamba watalipa gharama kubwa kwa kutaka kuichezea Urusi Taifa ambalo lilijitayarisha kwa miaka mingi sana ku-deal/kujibu kikamilifu uchokozi au uvamizi/mashambuliza ya mataifa ya NATO na wengine - kitu cha kwanza Urusi haiogopi Taifa lolote hapa Duniani, hata west wasipo nunua mafuta na gesi kutoka nchini mwake bado Urusi itaendelea kudunda tu, kwanza Urusi imekwisha pata soko kubwa kutoka mashariki ya mbali na Asia, cha ajabu hata mataifa hayo hayo yanayo jitia kuichukia Urusi bado yanaendelea kununua kinyemela bidhaa za nishati za Urusi kwa kupitia India, wengine bado wanaendelea kununua nishati moja kwa moja kutoka Urusi, jamaa hawa wanafiki sana.
 
Endapo Russia itaamua kukomaa kuendelea na vita basi mwisho wa siku ni yenyewe ndio itatakuja kupoteza kwani uchumi wao hautaweza kustahimili vita visivyo na mwisho.

Yale mataifa yanayonunua mafuta na gesi yao kwa bei ya chini yakibanwa vizuri Russia hatakuwa na ujanja ni lazima atafyata tu.
Wewe punguani kweli wateja wakubwa wa Urusi ni China na India miaka yote karibia nusu ya watu duniani wapo hizo nchi na wameishambwambia Marekani hatuwezi kuacha kununua mafuta Urusi kwa manufaa za nchi zetu.
 
Back
Top Bottom