Urusi haitashinda hii Vita

Mtoa mada, kwasasa hakuna tena hoja kwa hoja Bali hoja kwa vioja...watu wamepanic sana kwanini Rusia na Putin wanapingwa.

Ebu fikiria Ligi yao hautambuliwi na FIFA, anga imefungwa, Mali za wafanyabiashara kwenye baadhi ya nchi zinahujumiwa na Mambo mengine mengi lakini watu wanashabikia tu kitu kikoja Rusia kushika Slaa.

Kujijenga ni kigumu sana ila kuharibu taswira ni dakika chache sana...sisi yetu macho matokeo ya huko Ukraine.
 
Yaani hizo sanctions ndizo zinamfanya Russia aiteketeze kiev
 
Kwa waliokaa US au nchi za magharibi wanajua vizuri na njia muafaka kabisa ya kummaliza adui yako, shambulia mifuko yake kwanza na ndicho anachofanyiwa Putin sasa, hii vita hatoboi soon ataomba poo, mnyamwezi akihisi una criminal au misheni zisizoeleweka anaanza kuvamia account zako and freeze them kabla hata kesi haijaanza, utakata deal tuu hata kama hujafanya kosa
 
Wewe unayeswaga ng'ombe 🐮🐮 kupeleka mnadani Kibaigwa ndio eti unajua na eti Ukraine wenyewe wasijue.

Russia inaelekea kaburini wananchi wameshaanza kupanga foleni ya vyakula ndio eti wewe unaishabikia, ujinga ni mzigo.
 
This week Kiev inatekwa na yule mpoki wao akimbie la sivyo atakamatwa na kupelekwa Moscow.

Propaganda za MSM hszitaiaidia Ukraine in the ground, Ukraine itachapwa na hakuna atakayemsaidia
 
Putin kwa sasa yupo kwenye hatari, ni kama mateka, akirudi nyuma basi Warusi nyumbani watamtafuna kwa kuitia nchi kwenye aibu, akiendelea mbele, hao hao Warusi watamtafuna Kwa kuitia nchi kwenye umaskini na ukata maana hivi vita vitaigharimu Urusi sana.
Imebaki ajitoe ufahamu na kufyatua nyuklia ila hapo ndio anasubiriwa ili atakachofanyiwa kiwe fundisho kwa Iran, Korea kwa Kim na machizi wengine ambao hufikiria nyuklia ni mchezo wa lele mama.
 
masela umeongea vizuri ila umeongelea vita vya uchumi - kichwa cha hoja husika - vita mbugani na mjini nani atamzuia mrusi
 
Mkuu umesema unaonge uhalisia lakini nimeutafuta kwenye andiko lako bila mafanikio.
Wamarekani wenyewe wanajua Ukraine lazima ianguke ni suala la muda tu. Labda ungezungumzia gharama za ushindi wa Urusi sio kushindwa kwake maana huo ndio uhalisia.
 
Aliyeleta mada ametoa hoja kuwa usa kiuchumi na kijeshi yuko vizuri, wakati Mrusi yuko kijeshi zaidi huku hali ya kiuchumi ikiendelea kuwa ngumu, ukipinga pinga kwa hoja na ukikubali uwe na hoja pia
Ukraine anapokea dozi ya kichapo wewe unakuja kusema kuwa USA ana hela kuliko Russia sasa haya yatamsaidiaje Zelensky? Nyie wenye nguvu shirikianeni na huyo laghai mwenye hela kuleta suluhu huko Ukraine kupunguza maafa siyo kuleta porojo kuwa US ana hela na jeshi kubwa kuliko Russia na wakati hadi leo biden anaendelea kulia lia kuwa hataenda kupigana ukraine na wakati huo huo akiendelea kununua energy sources from russian kwa mkono wa nyuma.

Sasa mtu yupo tandahimba anakunywa ulaka anatamba kuwa US ana hela na jeshi kuuuubwa lakini kwenye uwanja wa mapambano haonekani.
 
Mrusi kashindwa kuipiga ukraine ndani ya siku tatu na sasa ana zaidi ya siku 20 sasa hao wenye maguvu ya kijeshi na mihela wanahitaji siku ngapi ili kumzuia huyu masikini asiye na jeshi aneitesa ukraine? Au ndo yale maneno kwamba NATO wanapigana kusayansi (vikwazo) dhidi ya urusi sasa nikajiuliza Putin akirusha makombora anatumia mizizi ya mwarobaini au nini?
 
Leta source ya hizo siku 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…