Urgent: Tanzania's National reconciliation | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urgent: Tanzania's National reconciliation

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WOWOWO, Oct 18, 2012.

 1. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Take your time, let us think critically

  Wana JF ni wazi sasa Taifa liko njia panda, linaumwa, linatikiswa na udini, ukabila, ukanda, ukosefu wa uzalendo,wizi wa rasilimali za Taifa, utendaji uliokosa tija na ubunifu, kukosekana kwa utu wema, imani za kishirikina,kutokujaliana, ukiburi, majivuno na kufifia kwa nguvu za taasisi nyeti zenye nafasi ya pekee katika kutukwamua hapa tulipo.

  Mtu yeyote anayeweza kusimama na kupingana na ukweli huu hakika atakuwa halitakii mema Taifa letu, anapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote maana haya yote yanalipeleka taifa katika kuparalyze kama si kuparaganyika kabisa.Watu wengi tayari wanaliona Taifa limeshafikia kwenye hali ya kuparalyze kutokana na yale yanayotokea sasa kama nilivyojaribu kuyadokeza hapo juu lakini hakika hatujachelewa, tunaweza kusimama kama taifa tukarekebisha hali kwani tuna hazina kubwa ya wasomi,wanasiasa wenye uzoefu mkubwa na kwa umuhimu zaidi tuna visima vingi vya busara kutoka kwa watu wa kada mbalimbali. Naomba nimulike haya japo kwa uchache na nini kifanyike haraka iwezekanavyo:

  UDINI, UKABILA NA UKANDA

  Kwa muda mrefu chini ya Hayati J.K Nyerere Taifa limekuwa moja, pamoja na tofauti zetu zote tuliendela kuwa ndugu, tukishirikiana katika kila hali, hatukutupana wala kuachana.Tulisimama pamoja. Hii imekuwa ni sifa kuu duniani kote. Lakini tukubali, hili limetoweka sasa. Kisa cha kutoweka ni uroho wa madaraka. Tumekuwa na aina ya wanasiasa ambao kwao madaraka ni muhimu kuliko taifa. Hawajali.

  Kiumri ni mdogo lakini ninaweza kusema kwa kujiamini kwamba toka zimeanza Siasa za ushindani nchini propaganda ambazo zimekuwa zikitamalaki zimejikita kwenye UDINI, UKABILA na UKANDA. Nisamehewe. Naziita propaganda kwasababu ni uzushi na uongo maana hakuna udini, ukabila wala ukanda uliokuwepo. Mitaani tunaishi bila matatizo wala ubaguzi wowote. Niwatu wanataka kujihalalalisha kwa kuligawa Taifa kama si kulisambaratisha kabisa.

  Sasa tunaporuhusu viongozi wakuu wa kitaifa, watu maarufu na vyombo vya habari kuimba na kuhubiri udini,ukabila na ukanda (ambao haupo) maana yake ni kuupanda mioyoni mwa Watanzania, kuupalilia na baadaye kuvuna mazao yake. Sasa hapa ndipo tulipofikia sasa. Propaganda hizo zimeingia mioyoni, sasa zinaanza kupasua mioyo.

  Hakika Propaganda hizo zimefanikiwa. Maana zimeota, zimenawili, zimekomaa, zinatoa matunda. Mazao yake ni kukojolea misahafu,kuchoma makanisa, kudai haki na huduma kwa misingi ya dini, kufukua maiti zilizozikwa kwenye makaburi ya dini tofauti, mahubiri ya chuki za kidini, ubaguzi wa kidini, machafuko, maandamano na ama kwa hakika tutafikia kuchinjana. Maadam tayati kuna watu walikuwa wamezamilia kumchinja mtoto aliyekojolea msahafu, hili haliko mbali, uvumilivu na subira havipo tena.

  WIZI WA RASILIMALI, UFISADI NA KUFIFIA KWA TAASISI NYETI ZA KIDOLA

  Hatuhitaji maneno mengi katika haya. Taifa linabakwa na rasilimali zake. Kuanzia hazina ya fedha ya taifa,madini, misitu, wanyama pori, ardhi, nishati, maji na sasa mafuta na gesi vinasombwa kupitia mikataba mibovu, usimamizi wa kifisadi na ubinafsi uliopitiliza wa baadhi ya watanzania wenzetu. Kama taifa hakuna anayejali kizazi cha kesho. Kasi ya kuchota kila rasilimali iliyopo ni kubwa, inatisha na inaliweka taifa kwenye kiza kinene. Hakuna Tanzania ya kesho. Kila kitu kinashambuliwa.

  Ujasiri wa kifisadi umekuwa mkubwa, watu hawaogopi kuchota mabilioni ya fedha hazina. Hawaogopi kujigawia vitalu vya uwindaji. Hawaogopi kuzunguka ughaibuni kunadi utajiri wa watanzania, hawajali kuuza vitalu mafuta na gesi bila kuwa na sera wala sheria. Hawaogopi kujimilikisha migodi na mali zote za umma. Tumejenga tabaka la kirafi, limelitafuna taifa na kuliacha mifupa. Wananchi wanaogelea kwenye dimbwi zito la ufukara. Hakuna anayejali uwepo wao.

  Sasa wakati haya yakiendelea, wengi tulidhani taasisi za kidola zingesimama kiweledi na kizalendo katika kudhibiti haya. La hasha! Nazo zimegeuka makuwadi wa ujambazi na ubakaji huu. Hakuna salama ya Taifa tena. Hata bunge ambalo lingesimama na wananchi limewageuka, limebaki kuwa la wachuma fedha, wala rushwa na walinzi wa maslahi ya wabakaji wa rasilimali za taifa. Hakuna salama, tuko njia panda.

  UZALENDO NA TAIFA KUPOTEZA UTAMBULISHO

  Zamani sisi tuliokulia vijijini bila shaka na mijini tulizoea kuamshwa na mchakamchaka na wimbo wa taifa kutoka kwa watoto wa shule. Sauti zao zilijaa uzalendo, matumaini na nguvu mpya kwa watanzania. Lakini sasa ni ndoto. Watoto wengi hata wimbo wa taifa hawaujui, matumaini yamepotea, hawajui watakula nini maana karibu tu na shule yao kuna mgodi wa madini unaomilikiwa na mwanasiasa mmoja maarufu nchini na hata uwanja wa shule waliokuwa wanautumia kwa michezo na mchakamchaka umeuzwa. Wamepoteza imani na taifa lao, hawaijui kesho yao wala ya wazazi wao.

  Asubuhi na mapema bendera ilipandishwana wimbo wa taifa ulipigwa na sote tulisimama kwa utiifu, ukakamavu, uzalendo na matumaini makubwa moyoni. Baadaye wazazi wetu walienda makazini na matumaini mengi huku wakiwa na furaha tele ya kulitumikia Taifa. Yote haya sasa ni ndoto.Tumepoteza karibu vyote kuanzia utamaduni wetu, asili na utambulisho kwa ujumla wake.

  Kila mtu anawaza tumbo lake, mipango ya kulitafuna taifa inapangwa kwenye ofisi za umma. Dili za kukwapua budget ya Serikali (OCs) zimetamalaki. Wananchi wanakamuliwa kodi na michango mbalimbali lakini hakuna kinachorudi kwao. Kinachorudi kwao ni mabomu, risasi na magari ya washawasha yanayowakaba koo kila wanaposimama kudai uwajibikaji kutoka kwa watawala. Rushwa ndiyo haki kwa sasa. Kama huna uwezo wa kuitoa hakuna huduma yoyote utakayopata. Utafia mapokezi. Watendaji wamegeuka miungu watu. Ofisi za umma zimebinafsishwa, majibu wanayotoa watumishi wa umma yana harufu chafu, hayavumiliki.Tuko njia panda.

  TUNAHITAJI NATIONAL RECONCILIATION

  Pamoja na ukweli kuwa mabadiliko ya kimfumo yanahitajika, lazima utafutwe muafaka wa kitaifa.Tunahitaji kuchora mistari juu ya hatma ya taifa. Tunahitaji kuliweka mikononi mwa watanzania, kwa sasa limetekwa na wabakaji wa rasilimali.Yafuatayo lazima yafanyike sasa:

  1. Iundwe Kamati Maalumu (National Think Tank) ya kuusaka muafaka wa Kitaifa
  Hakika kama nilivyojaribu kueleza hapo juu Taifa liko njia panda na kwa kweli kuna hatari ya kuparaganyika kama hatutasimama. Ni vema rais akalihutubia taifa na kutangaza mara moja kuunda kamati ya kitaifa itakayofanya kazi ya kufuta makovu yote yaliyoko nchini kuanzia udini na ubakaji wa rasilimali za taifa (Mengi yanafahamika). Kamati hiyo ijumuhishe watu wa kada mbalimbali nchini na wenye kuheshimika katika jamii (Muhimu viongozi wa kidini wapewe nafasi). Kamati ipewe majukumu mbalimbali kuelekea kufuta makovu yote yaliyopo. (Najua michango mbalimbali inaweza kutolewa katika kuboresha wazo hili) Lakini jambo moja ni lazima kamati hii iwe ya kudumu na ipewe nguvu na mamlaka ya kisheria kuingilia na kuhoji pale jambo lolote lenye maslahi mapana kwa taifa litakapojitokeza.Viongozi wote wa Serikali lazima wawe accountable kwa kamati hii. Kwa ujumla kamati hii itakuwa ni dira katika masuala na maamuzi mbalimbali yahusuyo Taifa letu.

  2. Iundwe Mahakama maalum ya Ubakaji rasilimali

  Ukweli ni kuwa taarifa za ubakaji wa rasilimali ziko kwenye maandishi na walau watanzania wengi na hata vyombo vya dola pamoja na kushindwa kuchukua hatua stahiki vina taarifa hizo. Aidha, tuna sheria zetu mbalimbali (zingine zinahitaji marekebisho) zinazoweza kuwatia pingu mafisadi na wezi wa rasilimali za taifa. Wazo langu (Uboreshaji unakaribishwa) ni kuundwa kwa mahakama maalum ambayo kazi yake kubwa ni kushughulikia kesi zote za wizi wa rasilimali za taifa zikiwemo fedha zilizofichwa na vigogo kwenye akaunti za nje. Wananchi wenye taarifa mbalimbali wasisitizwe kutoa vielelezo na kesi hizi ziende kasi na zisijikite katika kuutafuta ukweli kwenye makampuni ya Magharibi bali kwenye uhalisia na taaifa zilizoko nchini zinazogusa ufisadi wa watanzania wenzetu tu. Maana najua tukijiingiza huko (I mean kwenye international cases) tutahitaji International intercession procedures

  3. Tukae chini tufikirie kama taifa, tumesimama kufikiri

  Mimi ni kati ya watu wanaoamini kwamba kama Taifa toka Mwalimu Nyerere abuni sera ya Ujamaa na Kujitegema hatujawahi tena kupata wasaa wa kukaa chini kwa pamoja kama taifa na kufikiri tena. Tumekuwa taifa lililogawa tenda hii ya kufikiri mikononi mwa makuwadi wa Magharibi na vyombo vyao kama IMF, World Bank, WTO nk. nk. Taifa la China (Niko tayari kukosolewa) ni moja ya nchi ambayo Baba wa Taifa letu Hayati Nyerere alikopi baadhi ya sera zake. Leo hii China iliyoanza na mawazo ya muasisi wake Mao Zedong pamoja na mapungufu yake ni taifa la pili Duniani kwa uchumi na imeendelea kuishi katika maboresho (reforms) ya Mao na warithi wake. Sisi sera ya Ujamaa na Kujitegemea tumeitupa badala ya kuendelea kuifanyia maboresho (Reforms) katika kila awamu za uongozi zilizo za zitakazofuata ili iendane na hitaji halisi la maendeleo.

  Ni kwa sababu hiyo basi, tunahitaji kwa umoja na kwa ushirikishwaji wa hali ya juu kukaa chini upya na kujadiliana juu ya njia muafaka za kulijenga taifa letu. Hatuwezi kwenda bila kufanya hivyo. Natamani jukumu hili lingekuwa pia mikononi mwa Kamati hiyo maalum hapo juu (National Think Tank) lakini ngoja niachie wadau wengine wachekeche tupate mawazo tofauti.

  Pendekezo langu katika hili mjadala wa kuanza kuifikiria Tanzania upya urudi kwenye Sera ya Ujamaa na Kujitegema (Socialism and Self Reliance), maana haijapitwa, China bado inafanya,Urusi bado inafanya, nchi za Latin America bado zinafanya na hata Marekani yenyewe inafanya hivyo, mfano hai ni Sera ya Obama ya Afya na ile ya Relief for the Poor. I am out.
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Yote hayo yalipandwa mwaka 2010 na Dr Dhaifu sasa ndio wakati wa mavuno. Na mavuno yake huwa hayaishi tutajuta kuchagua mahandsome wa bagamoyo
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ... yote haya aliyasema Kamanda Lema siku nyingi tu lakini katu hakusikilizwa kitu; serikali yetu hii ni sikio la kufa mkuu.
   
Loading...