Uraisi CCM 2015 balaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uraisi CCM 2015 balaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUMBIRI, Jan 29, 2012.

 1. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionya wanachama wake kuacha ndoto za urais wa mwaka 2015, kauli hiyo sasa imeonekana kupuuzwa na kugeuka kichocheo cha kuongeza kasi ya kujipanga kwa baadhi ya makada wenye nia ya kusaka nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa taifa.

  Hivi karibuni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye, alionya kwamba chama hicho hakiko tayari kuendelea kuwakumbatia wanachama wake wanaunda makundi ndani ya chama, kwa lengo la kusaka umaarufu wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015
  .
  Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, Nape alisisitiza kuwa endapo mwanachama yeyote atabainika kuvuruga mshikamano ndani ya chama kutokana na kigezo hicho, CCM haitasita kuchukua hatua kali dhidi yake.

  Pamoja na CCM kutoa onyo hilo kali, mbio za urais wa mwaka 2015 ndani ya chama hicho, zimeelezwa kuingia katika sura mpya baada ya mmoja wa makada anayetajwa kuwania nafasi hiyo, kufanya kikao kizito jijini Arusha, kwa lengo la kuweka mikakati ya kujipanga na kuimarisha kambi yake.

  Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya wana CCM mjini Arusha, zinaeleza kuwa, kigogo huyo alifanya kikao chake wiki chache zilizopita katika moja ya majengo ya mfanyabiashara mmoja kutoka Kanda ya Ziwa, yaliyopo nje kidogo ya jiji.
  Kikao hicho kilichohudhuriwa na baadhi ya viongozi wa CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini, wakiwamo baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa chama hicho na baadhi ya viongozi wa Serikali, pamoja na mambo mengine, kilifanya tathmini ya kina kujua maeneo ambayo mgombea huyo hakubaliki.

  Chanzo chetu kilidokeza kwamba tathmini hiyo ilionyesha kuwa kada huyo hakubaliki sana katika mikoa ya Lindi , Mtwara pamoja na maeneo ya mikoa ya Kanda ya Ziwa, ukiwemo Mkoa wa Mara.
  Kutokana na hali hiyo, ilikubaliwa kuwa fedha nyingi zitumike na watu mahiri wenye ushawishi, watumwe katika maeneo haya ili kuwalainisha baadhi ya viongozi wa CCM ambao wanaonekana kuwa mbali na mgombea huyo, na jambo hilo lifanyike haraka kabla ya kuanza kwa chaguzi mbalimbali ndani ya CCM mwaka huu.

  Kauli ya Nape
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipoliuzwa kuhusiana na kikao hicho, alisema hana taarifa zozote lakini alionya kuwa endapo itathibitika kuwa kuna makada wa chama hicho wanafanya ‘rafu’ hizo, watachukuliwa hatua za kisheria za chama kwani huu si muda wa kufanya kampeni za urais.

  Aliwataka wanachama wa CCM kuipa nafasi Serikali yao kutekeleza majukumu yake na ilani kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.
  Awali, pia Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi, aliwahi kukaririwa akisema kuwa wanaotarajia kutumia fedha kupata urais kupitia chama hicho wanajidaganya, ni bora watafute kazi nyingine za kufanya.

  Kikao cha mkakati
  Habari zaidi kutoka ndani ya kikao hicho, zililidokeza Mwananchi Jumapili kuwa makada watakaotumwa kuzunguka mikoani, baada kukamilisha kazi yao, watatakiwa kurejesha ripoti itakayofanyiwa kazi, ili kundi hilo liweke mikakati zaidi ya kufanikisha lengo lake.
  Inaelezwa kuwa hofu kuu ya kundi hilo, ni kutoka kwa baadhi ya makada wengine wa CCM, wanaotajwa kuonyesha nia ya kuwania nafasi ya urais, kukubalika zaidi ndani ya chama katika mikoa hiyo, ambapo baadhi yao wanatoka huko.

  Chanzo chetu kilidokeza pia kuwa mbali ya kuweka mikakati hiyo kabambe ya kuwania urais, pia wajumbe wa kikao hicho ‘kizito’, walifanyiwa sherehe kubwa ambapo nyama na vinywaji mbalimbali vilimwagwa kwa wingi, ndani ya majengo ya mfanyabiashara huyo, ambayo yamezungushiwa ukuta mrefu.

  “Aisee! kikao kilikuwa kizito mno mikakati mizito imewekwa , jamaa yuko serious (makini) kuutaka urais, “alidokeza kada mmoja aliyekuwa ndani ya kikao hicho kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.

  Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa tayari, makada waliotumwa kwenda mikoani ‘kumnyoshea njia’ mgombea huyo wa urais, hivi sasa wanavinjari kwenye maeneo hayo, wakiwa na fedha za kutosha na vitendea kazi vingine, yakiwemo magari ya uhakika.
  Waliotumwa kufanya kazi hiyo, ni wenyeviti wa baadhi ya mikoa ambao imeelezwa kuwa watatumia nafasi zao kufanya ushawishi huo kwa urahisi.

  Ingawa hadi sasa hakuna kada ndani ya CCM ambaye ametangaza hadharani kutaka kuwania urais, inadaiwa kwamba kuna kundi kubwa la watu ambao tayari wanapigana vikumbo chini chini kutaka nafasi hiyo, kutokana na Rais wa sasa Jakaya Kikwete, kufikia ukomo wake kikatiba mwaka 2015.
  Hatua hiyo imedaiwa kuibua makundi yanayosabisha nyufa zinazoweza kuleta mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hicho.

  Tayari CCM kimekiri kupitia Katibu Mkuu wake, Wilson Mukama kuwa harakati za kuwania urais ndani ya chama hicho, zinakivuruga.
  Taarifa ya Kamati Kuu ya CCM iliyosomwa ndani ya Kikao cha Halmashuari Kuu (NEC) ya CCM mjini Dodoma Novemba mwaka jana ,pamoja na mambo mengine, ilikiri kuwa mbio za kuwania urais mwaka 2015 ndani ya chama hicho, ndicho kiini kikuu cha mgawanyiko.
  Kamati Kuu ilionya kuwa wanaotaka kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho, wanapaswa kudhibitiwa na kwamba matumizi ya fedha katika kampeni hayatakubalika.

  Ushauri wa Kinana
  Alhamisi wiki hii, Mjumbe wa Kamati Kuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alikaririwa na gazeti la Mwananchi akieleza kuwa vigogo wa chama hicho walioanza kampeni za urais, sasa wanavuruga utendaji wa Serikali ya Rais Kikwete.
  Akiwa kwenye ziara ya kutembelea matawi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kinana alisema vigogo hao ni wabinafsi, wanaivuruga nchi na hawana lolote wanalolifanya kwa maslahi ya chama hicho tawala.

  Kinana ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Kampeni za Rais Jakaya Kikwete wakati akigombea urais kwa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, alionesha kukerwa na watu hao na kueleza kuwa si sahihi kuanza kuzungumza masuala ya urais sasa wakati Rais Kikwete bado ana miaka minne ya kutekeleza Ilani ya chama hicho.
  “Sasa hivi Rais Kikwete ana miaka mingine minne mbele kabla ya kumaliza uongozi wake na CCM ina kero nyingi za kushughulikia ili kutekeleza ilani yake, halafu wengine wanazungumzia urais sasa,” alikaririwa akisema Kinana.
  Alisema anasikitishwa na hali hiyo hasa ikizingatiwa kuwa wanaoanza kupiga kampeni za urais ni watu wazito ndani ya nchi na ni wajumbe wa vikao vikuu ndani ya CCM.

  Tishio lingine
  Mbali ya chama hicho kukabiliwa na tishio la mgawanyiko kutokana na urais wa 2015, pia kinakabiliwa na kazi ngumu ya utekelezaji wa mkakati wake, kuwavua gamba baadhi ya makada wake wanaohusishwa na kashfa za ufisadi.

  Kikao kilichopita cha NEC ambacho kilitarajiwa kuchukua maamuzi magumu ya kuwavua gamba wanachama hao, kilishindwa kufanya hivyo, badala yake kikatoa muda kwa wanachama hao kujitathmini wenyewe na kuchukua uamuzi kabla ya CCM kuwachukulia hatua

  Source:
  Urais CCM 2015 balaa
   
 2. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Mkuu what i know here we dare to talk openly! Ujasiri wa kumtaja Nape umeutoa wapi huku huyo aliyefanya mkutano unamhifadhi kama vile mkutano ulikuwa niwasiri wakati inaonekana umehudhuriwa na watu kibao au ni tetesi hii? Mwaga data za kutosha asituache na maswali. Speak it out
   
 3. M

  Mohamed Ibrahim Member

  #3
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aliefanya sherehe hizo ni Ndanda Kosovo na ana wapambe wa kutosha hasa wale wote ambao ni wahanga wa serikali ilioko madarakani wanakuwa wanamuunga mkono yeye.....ukiangalia ndani ya vijana utamkuta Bashe ambaye ana machungu ya kupambana na Dear Leader mara kadhaa....Makongoro ambaye ana uchungu wa kutopewa full minister etc
   
 4. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,075
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  tUMBIRI UMEHAMA cdm .... naona habari za CCM zinakushughulisha sana... karibu CCM kwenye siasa za kistaarabu
   
 5. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tuongee ukweli tu jamani; hivi Membe, H.Mwinyi,Sitta,Migiro na wengineo wana ubavu wa kushindana na Lowassa ndani ya CCM? Na je wana uwezo kiuongozi kuliko mthubutu Lowassa?
   
 6. M

  Mohamed Ibrahim Member

  #6
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Watanzania mil 45 anaeweza kuongoza ni lowasa tu huu ni wendawazimu kwa kweli.....mtu mwenyewe kuona mwisho mita kumi na wanasema anaendelea kudhoofu
   
 7. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mpaka 2014 kutakuwa na ccm yenye vipande siyo chini ya vinne. Na hao wanaojifanya kuitetea serikali ya sasa ikifika 2014 lazima wataikimbia na kuungana na vipande vyenye nguvu. Naamini kipande Kinachotawala haikitakuwa na nguvu tena maana kimedharaulika.
   
 8. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  inasikitiisha sana kuona viongozi badala ya kujikita katika shughuli za maendeleo na kutatua kero lukuki za wananchi, wao wanaota ndoto za urais tu, damn!
   
 9. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii habari nimeicopy na kuipaste kutoka Mwananchi Newspaper Website. Mimi siyo mwandishi wa hii habari!
   
 10. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kaka ni heri nife kuliko niwe MwanaCCM! CCM ni Janga la Taifa, tulitokomeze!

 11. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Na miongoni mwa watakaoikimbia ndiyo hawa hawa wa leo wanaoitetea mfano, Abrahamani Kinana, Lazaro Nyalandu, Nnape Nnauye, nk
   
 12. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kazi hii iliwashinda na waliiagiza CC iwachukulie hatua
   
 13. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,080
  Trophy Points: 280
  Mkuu heshima! Umenifurahisha kwa ku-acknowledge source ya uzi wako. Safi sana.
   
 14. g

  greenstar JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamaa ni kirusi anayesambaa kama HIV,gusa unase....RAI yangu kwa mawaziri wa JK fanyeni kazi kwa bidii,RAIS atatoka ndani ya baraza la MAWAZIRI ,wote muungane pamoja kupambana na KIRUSI hicho....

  JK acha kulemba ondoa kirusi kabla hakijakumaliza,wala usimtoe kafara NAPE awe ananung'unika na kutoa vitisho wakati wewe upo nyuma yake.Sasa ni muda wa vitendo.......

  Kwanza tunaomba ripoti ya DR.MWAKYEMBA itolewe na RAIS wetu bila kurushiana mpira kwa MAWAZIRI.......hakika utaonyesha wewe ni RAIS wa WATANZANIA ambaye ni SHUPAVU.Usiogope kufa kwa chama lakini ogopa nchi kukosa AMANI.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA .....RUDI HARAKA
   
 15. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Huyo lowasa anachojua kuwapa sumu wenzake shetttttani mkubwa huyo wallah mkimpa uraisi akheri nichukue uraia wa somalia ambako hakuna serikali.
   
 16. s

  sharkzulu Member

  #16
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndani ya magamba "ATAKAYE KULA NYAMA NI MWENYE KISU KIKALI"

  kuhusu kuwavua gamba hawa jamaa, magamba hawawezi kuthubutu, tangu wamekutana na mtanange ndani ya maskani ya RA igunga, Gharama waliyoitumia kulikomboa jimbo hilo ni kubwa sana, hivyo wakiyavua magamba mengine watafulia kwa kuwa plan yao kubwa iliwaweze kujiokoa ni kutumia kisu kikali kukata nyama ndiyo maana nasema ndain ya MAGAMBA MWENYE KISU KIKALI NDIYE ATAYE KWAANA NA NAFASI YA URAIS<

  Ubinafisi unaofanywa na viongozi hawa umetokana na mafunzo ndani ya chama kutumia kwa njia wanazozitumia wakati wa uchaguzi, ni za giliba.
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye​

  KIGOGO AMWAGA MAMILIONI, ATUMA MAKADA MIKOANI KUMNYOSHEA NJIA
  Na Mwandishi Wetu
  WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionya wanachama wake kuacha ndoto za urais wa mwaka 2015, kauli hiyo sasa imeonekana kupuuzwa na kugeuka kichocheo cha kuongeza kasi ya kujipanga kwa baadhi ya makada wenye nia ya kusaka nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa taifa.Hivi karibuni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye, alionya kwamba chama hicho hakiko tayari kuendelea kuwakumbatia wanachama wake wanaunda makundi ndani ya chama, kwa lengo la kusaka umaarufu wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015.

  Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, Nape alisisitiza kuwa endapo mwanachama yeyote atabainika kuvuruga mshikamano ndani ya chama kutokana na kigezo hicho, CCM haitasita kuchukua hatua kali dhidi yake.

  Pamoja na CCM kutoa onyo hilo kali, mbio za urais wa mwaka 2015 ndani ya chama hicho, zimeelezwa kuingia katika sura mpya baada ya mmoja wa makada anayetajwa kuwania nafasi hiyo, kufanya kikao kizito jijini Arusha, kwa lengo la kuweka mikakati ya kujipanga na kuimarisha kambi yake.

  Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya wana CCM mjini Arusha, zinaeleza kuwa, kigogo huyo alifanya kikao chake wiki chache zilizopita katika moja ya majengo ya mfanyabiashara mmoja kutoka Kanda ya Ziwa, yaliyopo nje kidogo ya jiji.

  Kikao hicho kilichohudhuriwa na baadhi ya viongozi wa CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini, wakiwamo baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa chama hicho na baadhi ya viongozi wa Serikali, pamoja na mambo mengine, kilifanya tathmini ya kina kujua maeneo ambayo mgombea huyo hakubaliki.

  Chanzo chetu kilidokeza kwamba tathmini hiyo ilionyesha kuwa kada huyo hakubaliki sana katika mikoa ya Lindi , Mtwara pamoja na maeneo ya mikoa ya Kanda ya Ziwa, ukiwemo Mkoa wa Mara.

  Kutokana na hali hiyo, ilikubaliwa kuwa fedha nyingi zitumike na watu mahiri wenye ushawishi, watumwe katika maeneo haya ili kuwalainisha baadhi ya viongozi wa CCM ambao wanaonekana kuwa mbali na mgombea huyo, na jambo hilo lifanyike haraka kabla ya kuanza kwa chaguzi mbalimbali ndani ya CCM mwaka huu.

  Kauli ya Nape
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipoliuzwa kuhusiana na kikao hicho, alisema hana taarifa zozote lakini alionya kuwa endapo itathibitika kuwa kuna makada wa chama hicho wanafanya ‘rafu’ hizo, watachukuliwa hatua za kisheria za chama kwani huu si muda wa kufanya kampeni za urais.

  Aliwataka wanachama wa CCM kuipa nafasi Serikali yao kutekeleza majukumu yake na ilani kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.Awali, pia Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi, aliwahi kukaririwa akisema kuwa wanaotarajia kutumia fedha kupata urais kupitia chama hicho wanajidaganya, ni bora watafute kazi nyingine za kufanya.

  Kikao cha mkakati
  Habari zaidi kutoka ndani ya kikao hicho, zililidokeza Mwananchi Jumapili kuwa makada watakaotumwa kuzunguka mikoani, baada kukamilisha kazi yao, watatakiwa kurejesha ripoti itakayofanyiwa kazi, ili kundi hilo liweke mikakati zaidi ya kufanikisha lengo lake.

  Inaelezwa kuwa hofu kuu ya kundi hilo, ni kutoka kwa baadhi ya makada wengine wa CCM, wanaotajwa kuonyesha nia ya kuwania nafasi ya urais, kukubalika zaidi ndani ya chama katika mikoa hiyo, ambapo baadhi yao wanatoka huko.
  Chanzo chetu kilidokeza pia kuwa mbali ya kuweka mikakati hiyo kabambe ya kuwania urais, pia wajumbe wa kikao hicho ‘kizito’, walifanyiwa sherehe kubwa ambapo nyama na vinywaji mbalimbali vilimwagwa kwa wingi, ndani ya majengo ya mfanyabiashara huyo, ambayo yamezungushiwa ukuta mrefu.

  “Aisee! kikao kilikuwa kizito mno mikakati mizito imewekwa , jamaa yuko serious (makini) kuutaka urais, “alidokeza kada mmoja aliyekuwa ndani ya kikao hicho kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.
  Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa tayari, makada waliotumwa kwenda mikoani ‘kumnyoshea njia’ mgombea huyo wa urais, hivi sasa wanavinjari kwenye maeneo hayo, wakiwa na fedha za kutosha na vitendea kazi vingine, yakiwemo magari ya uhakika.

  Waliotumwa kufanya kazi hiyo, ni wenyeviti wa baadhi ya mikoa ambao imeelezwa kuwa watatumia nafasi zao kufanya ushawishi huo kwa urahisi.

  Ingawa hadi sasa hakuna kada ndani ya CCM ambaye ametangaza hadharani kutaka kuwania urais, inadaiwa kwamba kuna kundi kubwa la watu ambao tayari wanapigana vikumbo chini chini kutaka nafasi hiyo, kutokana na Rais wa sasa Jakaya Kikwete, kufikia ukomo wake kikatiba mwaka 2015.

  Hatua hiyo imedaiwa kuibua makundi yanayosabisha nyufa zinazoweza kuleta mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hicho.
  Tayari CCM kimekiri kupitia Katibu Mkuu wake, Wilson Mukama kuwa harakati za kuwania urais ndani ya chama hicho, zinakivuruga.

  Taarifa ya Kamati Kuu ya CCM iliyosomwa ndani ya Kikao cha Halmashuari Kuu (NEC) ya CCM mjini Dodoma Novemba mwaka jana ,pamoja na mambo mengine, ilikiri kuwa mbio za kuwania urais mwaka 2015 ndani ya chama hicho, ndicho kiini kikuu cha mgawanyiko.

  Kamati Kuu ilionya kuwa wanaotaka kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho, wanapaswa kudhibitiwa na kwamba matumizi ya fedha katika kampeni hayatakubalika.

  Ushauri wa Kinana
  Alhamisi wiki hii, Mjumbe wa Kamati Kuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alikaririwa na gazeti la Mwananchi akieleza kuwa vigogo wa chama hicho walioanza kampeni za urais, sasa wanavuruga utendaji wa Serikali ya Rais Kikwete.
  Akiwa kwenye ziara ya kutembelea matawi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kinana alisema vigogo hao ni wabinafsi, wanaivuruga nchi na hawana lolote wanalolifanya kwa maslahi ya chama hicho tawala.

  Kinana ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Kampeni za Rais Jakaya Kikwete wakati akigombea urais kwa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, alionesha kukerwa na watu hao na kueleza kuwa si sahihi kuanza kuzungumza masuala ya urais sasa wakati Rais Kikwete bado ana miaka minne ya kutekeleza Ilani ya chama hicho.

  “Sasa hivi Rais Kikwete ana miaka mingine minne mbele kabla ya kumaliza uongozi wake na CCM ina kero nyingi za kushughulikia ili kutekeleza ilani yake, halafu wengine wanazungumzia urais sasa,” alikaririwa akisema Kinana.
  Alisema anasikitishwa na hali hiyo hasa ikizingatiwa kuwa wanaoanza kupiga kampeni za urais ni watu wazito ndani ya nchi na ni wajumbe wa vikao vikuu ndani ya CCM.

  Tishio lingine
  Mbali ya chama hicho kukabiliwa na tishio la mgawanyiko kutokana na urais wa 2015, pia kinakabiliwa na kazi ngumu ya utekelezaji wa mkakati wake, kuwavua gamba baadhi ya makada wake wanaohusishwa na kashfa za ufisadi.

  Kikao kilichopita cha NEC ambacho kilitarajiwa kuchukua maamuzi magumu ya kuwavua gamba wanachama hao, kilishindwa kufanya hivyo, badala yake kikatoa muda kwa wanachama hao kujitathmini wenyewe na kuchukua uamuzi kabla ya CCM kuwachukulia hatua.

  Urais CCM 2015 balaa
   
Loading...