Urais wa Tanzania ni madaraka makubwa sana!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,315
38,454
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mzee Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na sasa John Magufuli, kwa nyakati tofauti wamewahi kutoa mguno kuonesha nafasi waliyoishikilia ni kubwa sana na ina majukumu mazito sana. Mwalimu aliwahi kusema "Urais ni mzigo" lakini akasahau kusema kwamba mzigo wa mwenzio ni furushi la Pamba.

Tulioko nje ya urais tuna nafasi ya kusema lolote kuhusu wanaokuwa marais wetu lakini ugumu wa kuwa Rais Tanzania wanaujuwa wanaokuwa marais. Mwinyi alipoingia tu alikuja na kauli mbiu ya "fagio la chuma" lakini kadri muda ulivyokwenda ndiyo akaanza kukumbushwa kwamba ana fagio la chuma kwa nini halitumii!?

Akaja Banjamin Mkapa na kauli mbiu yake ya "uwazi na Ukweli" lakini kadri siku zilivyokuwa zinakwenda mbele uwazi na ukweli ukaanza kutiliwa shaka kwenye serikali aliyokuwa anaiongoza. Yalipokuja mambo ya Mgodi wa kiwira watu wakaanza kuhoji kama mgodi huo uliuzwa kwa uwazi na waliuuza kama walisema kweli kuwa ni nani hasa aliuziwa mgodi ule.

Jakaya Kikwete Rais mwenye bashasha nyingi sana alikuja na kauli mbiu "Ari Mpya! Nguvu mpya!Kasi Mpya!" na "Tanzania yenye neema inawezekana!" lakini na yeye aliondoka kabla ya Tanzania yenye neema kuonenkana na watu walihoji Ari, nguvu na kasi Mpya zilipoishia.

Rais wa sasa kaingia na kauli mbiu ya "Hapa kazi tu" na kwa kweli kwa dhamira na matendo yake unaona kabisa kwamba anatamani kabisa Tanzania iendeshwe kwa mtindo wa hapa kazi tu. Lakini hata yeye kwa maneno yake kwamba kuna watu wanataka "kumkwamisha" bila ya shaka kuna tatizo lipo linalozuia hamu ya kutimiza ndoto yake ya kuiona Tanzania ya viwanda kupitia kufanya kazi tu.

Kwa mtazamo wangu hii yote inatokana na Rais wa nchi yetu kupewa na Katiba pamoja na sheria zinazotokana na Katiba hiyo, madaraka makubwa sana madaraka ambayo kwa kanuni zozote zile ni lazima yamwelemee yeyote yule atayeshika madaraka hayo. Katiba yetu imempa Rais wetu madaraka ya Kifalme wakati yenyewe inataka kuitafsiri nchi yetu kuwa ni ya Kidemokrasia na ni Jamhuri.

Mfalme hahojiki pia watu pamoja na vyote vilivyomo kwenye nchi anayoongoza ni mali yake. Rais wa Jamhuri anahojika na anapingwa na wakati mwingine kuondolewa madarakani. Sasa mnapompa kikatiba Rais mamlaka ya kifalme lakini mkatengeneza mfumo wa kuendesha nchi wa kidemokrasia lazima kuwe na utata na matumizi ya maguvu na mabavu hayaepukiki!
 
Wakuu nasikitika kuona taswira hii ya mihadarati inashughulikiwa TZ bara.... wakati huko Kisiwani Zanzibar kama wao malaika hawajihusishi ma janga hili!!
na ukweli takwimu za kimataifa zinaonesha kuwa waathirika wengi na biashara hiyo ipo Zanzibar!!

Setikali ya muungano fikisheni mikono hadi Zanzibar... kunahharikika na kuzama huko!!!
 
Kwetu Tanzania ni bado sana kujua kama madaraka ya "Tanzania" huwa yana nguvu hata kule Zanzibar. Hata Sianga juzi aliongea kama vile Zanzibar ni nchi nyingine yenye mamlaka yake kamili kuhusu masuala ya kupambana na madawa ya kulevya.
 
Ndiyo maana kuna wengine hawataki hata kukosolewa, wanajiona Miungu watu wasiojaribiwa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mzee Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na sasa John Magufuli, kwa nyakati tofauti wamewahi kutoa mguno kuonesha nafasi waliyoishikilia ni kubwa sana na ina majukumu mazito sana. Mwalimu aliwahi kusema "Urais ni mzigo" lakini akasahau kusema kwamba mzigo wa mwenzio ni furushi la Pamba.

Tulioko nje ya urais tuna nafasi ya kusema lolote kuhusu wanaokuwa marais wetu lakini ugumu wa kuwa Rais Tanzania wanaujuwa wanaokuwa marais. Mwinyi alipoingia tu alikuja na kauli mbiu ya "fagio la chuma" lakini kadri muda ulivyokwenda ndiyo akaanza kukumbushwa kwamba ana fagio la chuma kwa nini halitumii!?

Akaja Banjamin Mkapa na kauli mbiu yake ya "uwazi na Ukweli" lakini kadri siku zilivyokuwa zinakwenda mbele uwazi na ukweli ukaanza kutiliwa shaka kwenye serikali aliyokuwa anaiongoza. Yalipokuja mambo ya Mgodi wa kiwira watu wakaanza kuhoji kama mgodi huo uliuzwa kwa uwazi na waliuuza kama walisema kweli kuwa ni nani hasa aliuziwa mgodi ule.

Jakaya Kikwete Rais mwenye bashasha nyingi sana alikuja na kauli mbiu "Ari Mpya! Nguvu mpya!Kasi Mpya!" na "Tanzania yenye neema inawezekana!" lakini na yeye aliondoka kabla ya Tanzania yenye neema kuonenkana na watu walihoji Ari, nguvu na kasi Mpya zilipoishia.

Rais wa sasa kaingia na kauli mbiu ya "Hapa kazi tu" na kwa kweli kwa dhamira na matendo yake unaona kabisa kwamba anatamani kabisa Tanzania iendeshwe kwa mtindo wa hapa kazi tu. Lakini hata yeye kwa maneno yake kwamba kuna watu wanataka "kumkwamisha" bila ya shaka kuna tatizo lipo linalozuia hamu ya kutimiza ndoto yake ya kuiona Tanzania ya viwanda kupitia kufanya kazi tu.

Kwa mtazamo wangu hii yote inatokana na Rais wa nchi yetu kupewa na Katiba pamoja na sheria zinazotokana na Katiba hiyo, madaraka makubwa sana madaraka ambayo kwa kanuni zozote zile ni lazima yamwelemee yeyote yule atayeshika madaraka hayo. Katiba yetu imempa Rais wetu madaraka ya Kifalme wakati yenyewe inataka kuitafsiri nchi yetu kuwa ni ya Kidemokrasia na ni Jamhuri.

Mfalme hahojiki pia watu pamoja na vyote vilivyomo kwenye nchi anayoongoza ni mali yake. Rais wa Jamhuri anahojika na anapingwa na wakati mwingine kuondolewa madarakani. Sasa mnapompa kikatiba Rais mamlaka ya kifalme lakini mkatengeneza mfumo wa kuendesha nchi wa kidemokrasia lazima kuwe na utata na matumizi ya maguvu na mabavu hayaepukiki!
ndo mana hawataki kubadili katiba kile kipengele cha kinga za raisi kiondo;ewe ili ikitoka raisi katumia madaraka vibaya akitoka madarakani tu awajibishwe kama wengine tunaowaona duniani ..........
 
Mulhat Mpunga siyo tu kinga ya kutokushitakiwa bali ana mamlaka makubwa sana ya kifalme! Hapo ndiyo tatizo lilipo. Uteuzi wa Waziri una tofauti gani na uteuzi wa Mkuu wa wilaya. Kwenye wilaya kuna Watu kibao ambao wote wanateuliwa na Rais.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Siku tukitenganisha Ikulu na walafi, tutaiona Tanzania inayo ngara kama marumaru. Lakini kuna Ikulu gani duniani hainana walafi? Labda Vatican lakini na huko pia kuna walakini.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Siku tukitenganisha Ikulu na walafi, tutaiona Tanzania inayo ngara kama marumaru. Lakini kuna Ikulu gani duniani haiadamwi na walafi? Labda Vatican lakini na huko pia kuna walakini.
Hoja siyo walafi bali kurundika kila kitu kwa mtu mmoja!! Kumbuka ulafi ni asili ya binadamu!
 
Nafurahi kama unekubali ulafi ni kitu kilicho endelezi, na kukipinga ni bora kupanda Kilimanjaro mara mbili kila mwezi. Taasisi ya urais ni taasisi pana sana, kuna watu wanahusika na maamuzi ya nchi amabao hatuwaoni kwenye taarifa ya habari. Lakini kwakuwa sisi hatuna wa kumlaumu bali ni rais, ndio maana rais anahitajika kuwa na ngozi ngumu ya kupokea lawama zote. Lakini sio kweli kama ni mtu mmoja ndio anaamua kila kitu. Hata kama ni kweli, wale wafanyakazi wote wa serikali wanaeda kazini kufanya nini.
 
Lakini sio kweli kama ni mtu mmoja ndio anaamua kila kitu. Hata kama ni kweli, wale wafanyakazi wote wa serikali wanaeda kazini kufanya nini.
Soma katiba yetu Ibara ya 35 kifungu kidogo cha Pili uone kwamba kumbe kila mfanyakazi wa serikali anafanya kazi kwa niaba ya Rais! Rais anapewa ushauri lakini si lazima aukubali ushauri huo!
 
Rais wa nchi hatakiwii kuwekewa vizngit vyovyote ili aguse kila sehemu,, ahasante Trump umetuonesha meno ya Rais
 
Trump kafanyaje kuonesha kwamba rais hatakiwi kuwekewa vikwazo? Hujui kwamba Jaji alizuia amri yake ya kuzuia baadhi ya watu toka nchi fulani fulani wasiingie Marekani?
 
Umeifatilia vizuriiii hiyo movie ilipofika,, hadii sasa?? Rais ni taasis kubwa hata ipo chin yake yeye ndiye anajua nan aisimamie kama jaji mkuu,,, mwanasheria mkuu,, ili kulinda serikali,,
 
Wakuu nasikitika kuona taswira hii ya mihadarati inashughulikiwa TZ bara.... wakati huko Kisiwani Zanzibar kama wao malaika hawajihusishi ma janga hili!!
na ukweli takwimu za kimataifa zinaonesha kuwa waathirika wengi na biashara hiyo ipo Zanzibar!!

Setikali ya muungano fikisheni mikono hadi Zanzibar... kunahharikika na kuzama huko!!!
Hakuna Tanzania bara bila Tanzania visiwani BALI
Kuna Tanganyika na Zanzibar
 
Soma katiba yetu Ibara ya 35 kifungu kidogo cha Pili uone kwamba kumbe kila mfanyakazi wa serikali anafanya kazi kwa niaba ya Rais! Rais anapewa ushauri lakini si lazima aukubali ushauri huo!
Sawa kabisa, na ndio maana watumishi wa serikali wanakula kiapo cha utii kwa nchi, serikali, na rais. Rais anaweza akashauriwa na akakataa ushauri kama hauna maslai kwa nchi. Na hapo hapo kwa upeo wake (rais) ana weza kulinganisha taarifa mbili tofauti alizo pewa ili kufikia uwamuzi huo. Kumbuka kila uamuzi lazima uandijishwe ili kuwe na ufatiliaji ni kwanini uamuzi umeamuliwa hivyo, hata kama maamuzi yalitolewa barabarani.
 
Huo ni mtazamo wako kilewella wengine wana mtazamo wa kumtumia Rais huyo huyo salamu nzito, ndio raha ya demokrasia. Ni mtazamo wako tu halafu unajinafasi.

Na washawasha!
 
Mulhat Mpunga siyo tu kinga ya kutokushitakiwa bali ana mamlaka makubwa sana ya kifalme! Hapo ndiyo tatizo lilipo. Uteuzi wa Waziri una tofauti gani na uteuzi wa Mkuu wa wilaya. Kwenye wilaya kuna Watu kibao ambao wote wanateuliwa na Rais.
Kiuhalisia, kiongozi/mtawala mbaya zaidi kuwah kutokea hapa Tanzania ni yule wa awamu ya kwanza...............

yeye ndio aliasisi katiba hii hali akijua madaraka ya Raisi ni makubwa san, sasa unajiuliza kwann hakubadili katiba wkt akiwa madarakani???

hili la katiba huko aliko anatakiwa alibebee msalaba wake, alikua mnafiki sana na ndio source ya matatizo yetu mengi sana!
 
Mulhat Mpunga siyo tu kinga ya kutokushitakiwa bali ana mamlaka makubwa sana ya kifalme! Hapo ndiyo tatizo lilipo. Uteuzi wa Waziri una tofauti gani na uteuzi wa Mkuu wa wilaya. Kwenye wilaya kuna Watu kibao ambao wote wanateuliwa na Rais.
Ndiyo maana wateule wa rais huko mikoani na wilayani ni miungu watu vile vile. Viongozi waliochaguliwa na wananchi kama madiwani, wabunge, wenyeviti n.k. wanaonekana si lolote kwa wateule wa rais. Iko kwenye record bwana mkubwa aliwaambia ma DC wasiwasikilize madiwani.
 
Back
Top Bottom