Uraia wangu

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
13,104
Reaction score
5,665
Jamani naomba msaada ili nijue uraia wangu.
Nimezaliwa mwaka 2011 mkoani Pwani.
Nimesikia baadhi ya watu wakiniita mtanzania eti nimezaliwa katika JMT.Na mimi nakubali.
Wengine wananiita mtanganyika wakisema eti nimezaliwa ndani ya Tanganyika iliyozaliwa kisiri kwa mara ya pili baada ya kuzaliwa Zanzibar miaka kama mwaka mmoja nyuma kupitia mabadiliko ya katiba ya Zanzibar.
Hivyo nami pia nakubali.Sasa je,ina maana mimi na wenzangu wengi tuna uraia wa nchi mbili ndani ya nchi moja?
Nimesikia kuwa huku ---- ma-great thinkers wanaoweza kunisaidia ndio maana nimekuja huku.URAIA WANGU UKOJE KIUHALISIA?
 
Ulishawahi kuona passport ya Tanganyika?
 
Sijaitafuta bado mkuu.
Kama nikita kwenda Zanzibar wataniuliza passport?
Kama wataniuliza,nitatoa ya nchi gani?
Ulishawahi kuona passport ya Tanganyika?
 

Waliozaliwa Bara- yaani Tanganyika dio wana uraia wa nchi moja tu ambayo ni Jamhuri ya Muungano, maana Tanganyika ilikufa mwaka 1964. Wale wa Visiwani, yaani Zanzibar ndio wana uraia wa nchi mbili; wa Jamhuri ya Muungano na ule wa Nchi ya Zanzibar.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…