BabaMorgan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 5,188
- 14,345
URAFIKI.
URAFIKI/RAFIKI. Ni uhusiano wa karibu wenye upendo, uaminifu na kujali kati ya watu wawili au zaidi. Kama binadamu tunahitaji kuwa karibu na watu ambao tunawapenda, tunawaamini na tunajisikia furaha kuwa nao karibu katika maisha yetu ya kila siku. Kwa kutambua umuhimu wa urafiki kuna baadhi ya nchi zimechagua tarehe maalum ya kuadhimisha urafiki.
Urafiki unaitaji.
Kuna aina nyingi za urafiki. Kwa mfano unaweza kuta una marafiki wengi sana lakini kila mmoja anakuwa na umuhimu wake katika maisha yako. Hizi ni baadhi ya aina za urafiki.
Sumu kwenye urafiki(vitu vinavyoweza kuvunja urafiki)
Mara nyingi hii utokea ambapo urafiki huo unaisha kwa njia ya ugomvi baina ya marafiki
Urafiki ni asili ulikuwepo vizazi vilivyopita na hadi saa hivi bado upo.kila mtu kwa jinsi alivyo anatamani kuwa na rafiki mwenye sifa anazohitaji yeye. Na hapa ndipo usemi usemao ndege wanaofanana ndo wanaruka pamoja unajidhiirisha.

- Upendo
- Uaminifu
- Kujali
- Huruma
- Uelewa
- Akuufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
- Rafiki mnafiki
- Kaka kutoka kwa mama mwingine(brother from another mother)
- Rafiki wa kweli
- Rafiki wa faida(friendship with benefit)
Kuna aina nyingi za urafiki. Kwa mfano unaweza kuta una marafiki wengi sana lakini kila mmoja anakuwa na umuhimu wake katika maisha yako. Hizi ni baadhi ya aina za urafiki.
- RAFIKI MSHAURI.
- Ukikutana na changamoto huyu ndo anakuwa kimbilio la kwanza kumueleza na unamuamini kuwa anaweza kukupa ufumbuzi wa changamoto yako.
- RAFIKI STORI TU.
- Hapa kinachowafanya muwe karibu ni stori tu zinaweza zikawa stori za kujenga au kubomoa.
- RAFIKI KAZI.
- Urafiki ndani ya eneo la kazi tu nje ya kazi panakuwa hamna urafiki
- RAFIKI MSAADA.
- Huu ni urafiki ambao mara nyingi hutokea maeneo ya shuleni, vyuoni au mtaani unakuwa na urafiki sababu unaitaji msaada tu
- RAFIKI KUFA NA KUZIKANA.
- Rafiki ambaye mnasimama pamoja bila kujali changamoto zinazowatokea na mnaweza kugombana na baada ya muda mukapatana
Sumu kwenye urafiki(vitu vinavyoweza kuvunja urafiki)
- Ubinafsi
- Chuki
- Maneno ya umbea
- Roho mbaya
- Kujikweza(majigambo yasiyo na msingi)
Mara nyingi hii utokea ambapo urafiki huo unaisha kwa njia ya ugomvi baina ya marafiki
- Kutoeleana siri mlizoambiana(mara nyingi hii utokea kwa jinsia ke, hapa utasikia mengi kama nimuathirika, ametoa mimba nyingi, anatembea na mume wa mtu, mchoyo n.k
- Kunyanganyana vitu mlivyokabiziana kwa hiyari
- Kuogopana(sababu kila mmoja anajua udhaifu wa mwenzake)
- Kuwa na chuki(hata kama ikitokea mmoja anafanya mambo yanayofurahisha jamii kutokana na ugomvi wenu huwezi furahishwa na anachofanya)
- Kujiona bora zaidi(imani ya kila mtu hapa ni kwamba yeye alikuwa bora zaidi kwenye urafiki ndo kitu kinachosababisha isiwe rahisi kuombana msamaha
Urafiki ni asili ulikuwepo vizazi vilivyopita na hadi saa hivi bado upo.kila mtu kwa jinsi alivyo anatamani kuwa na rafiki mwenye sifa anazohitaji yeye. Na hapa ndipo usemi usemao ndege wanaofanana ndo wanaruka pamoja unajidhiirisha.
- Mlevi anahitaji rafiki mlevi(ili iwe rahisi kupeana kampani katika bar)
- Msomi anahitaji rafiki msomi
- Mcha mungu anamuhitaji mcha mungu
- Mtu ambae unajisikia huru kuwa naye(ili iwe rahisi kumueleza baadhi ya mambo yako ilasio yote)
- Mtu mwenye kujali
- Asiwe mbinafsi
- Mshauri(angalau awe na uwezo wa kushauri nini cha kufanya na wakati gani wa kufanya)
- Mkweli
- Awe na Upendo
- Mwenye kukupa motisha ya kufanya makubwa
- mkarimu
- epuka kuongea kila kitu chako kwa rafiki yako
- epuku kusema ndio kwenye kila kitu
- epuka urafiki usio kufurahisha
- epuka rafiki asiyejali hisia zako
- epuka rafiki anayekufanya utumie pesa nyingi kuliko kutafuta.