Watanzania tunaendelea kujifurahisha na kujifariji kwa upuuzi wa wabunge wa CCM. Nchi ina njaa na ajira hakuna, fedha haionekani na kwa zaidi ya miaka hii karibu 25 ya Mikataba ya madini iliyopitishwa na wabunge wa CCM leo wanakuja na stihizai tena.
Eti wabunge wa CCM wanataka kumpongeza rais Magufuli kwa lipi ? Si hata mficha mwizi anaweza kulia kwa uchungu wa kuibiwa kumbe mwizi kamuhifadhi chumbani ? Mnatania watanzania.
Mikataba mlipitisha kwa wingi wenu, makofi mukapiga, wapinzani waliopinga mliwazomea na kuwazodoa leo mnakula matapishi yenu na kufanya siasa uchwara ?
By the way mmetubu kwa kelele za Rais Magufuli aliyeshiriki kupitisha mikataba mibovu na kubariki katika baraza la Mawaziri kwa awamu mbili za Mkapa na Kikwete? si nyinyi watoto wenu wana hisa za vikampuni visaidizi vya ACCASIA na BARRIC ? na jamaa zenu ndio mliwapigania kupata ajira kule na watoto wa maskini kuachwa ?
Si ndio nyinyi mlikata viuno na kusema ndioooooo baada ya kupitisha ule upuuzi wa Mikataba ?
Tanzania chini ya CCM ni janga, wanatamani kupata pepo lakini hawako tayari kufa. Maskini .
Fanyeni mfanyavyo hatutawasamehe kwa upuuzi huu wa makusudi.
Kishada.