technically
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 12,504
- 51,000
Je ni sahihi Kwa gazeti linaloishi Kwa kutumia kodi za wananchi kuandika habari za ugomvi binafisi kanisani?.
Au ndio waandishi ambao Mzee Wa upako alisema wafe?...
Hivi inakuwa Gazeti linalo survive Kwa kodi ya wananchi kushindwa kwenda Field na kuja na habari za viwanda, Afya,elimu,maji, umeme kero za wananchi wanakaa dar kanisani na kuandika umbea kama yalivyo uwazi?...
Matokeo yake yanashindwa kuuzika yanakuwa ya kufungia mandazi na matokeo yake wenye hasara ni wananchi wanalipa kodi na hayo magazeti kupewa ruzuku.....
Niwaulize wana jamii forum Kwa uandishi huu kuna mtu anaweza kununua ilo Gazeti zaidi ya waumini waliogombana huko kanisani?...
Baada muweke documentary za story za viwanda mnaangaika na story za kipuuzi .
Nape yupo Kazi kuyafungia magazeti yanayoandika habari za uhakika kiuchunguzi hivi Gazeti kama hili litauzika aje wakuu?.
Kama gazeti la serikali linaweza kuandika habari za kipumbavu kama hizi wakati serikali inajinasibu ni serikali ya viwanda basi kuna haja ya viongozi waandishi kupimwa akili kabisa...