Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,998
- 20,345
Ninakemea na kulaani upuuzi huu wa chama cha Mapinduzi kutumia mifumo ya kiserikali kufanya shughuli za kisiasa...
Ninatoa rai kwa viongozi na watumishi tajwa katika barua hii ambao ni viongozi wa kiserikali wasihudhurie shughuli za kichama zilizoitishwa kwa barua hii...hakuna sheria nchini iwe ya utumishi au vyovyote itakayowahukumu....
Viongozi wa kiserikali itikeni mkiitwa kiserikali tu lakini kivyama itikeni kwa vyama vyenu huko mkiwa na magauni yenu ya mbogamboga...
Ifike wakati ccm iheshimu miiko ya kiserikali na kichama, Bila kukemea haya upuuzi huu utaenea na kuwa ni kawaida na sheria.
Mkurugenzi unakosa maadili unatumia nyaraka za kiserikali kuitisha watumishi kwa mambo yako ya chama?
Mwalimu Nyerere alimfukuza katika cheo Marehemu Paul Sozigwa kwakosa la kutumia barua rasmi ya chama kuomba michango ya harusi ya mwanae, hilo tu lilitosha kumwachisha kazi.
Leo Mkurugenzi anayejua miiko ya kiserikali anatumia barua za kiserikali kuharasi watumi wa kiserikali kuhudhuria vigodoro vya ccm???? Hii nchi inahitaji kunyooshwa sana hasa ndani ya ccm...
Kwenye Katiba ya nchi hakuna hata kifungu kimoja kinachowapa viongozi wa chama cha siasa jukumu la kuisimamia serikali. Serikali inasimamiwa na mhimili unaoitwa Bunge lenye wawakilishi wa wananchi wa kutoka vyama mbalimbali. Nchi haiongozwi na katiba ya chama, inaongozwa na katiba ya Tanzania. Katiba hiyo inawapa heshima na haki sawa raia wa nchi hii bila kujali tofatui zao kiitikadi wala kimaumbile.
Tusipoangalia kuna siku viongozi wa chama tawala watawaita mahakimu, kuna siku watawaita wanajeshi, kuna siku watawaita waalimu na kuna siku watawaita madaktari kwa madai hayo hayo ya kipuuzi; eti ndicho chama kinachounda serikali. Ndio maana inafikia mahali mkuu wa nchi anajisahau na kudai serikali yake haiwezi kuwapa ajira wapinzani...huo ni upungufu wa ustaarabu na ulevi wa madaraka.
Serikali inaendeshwa kwa kodi za wote bila kumbagua mwanaCCM, mpinzani na asiye na chama na wote wanaolipa kodi wana haki ya kupata huduma kama wananchi bila ubaguzi. Tusipoangalia kuna siku tutaambiwa ili utumie barabara lazima uwe mwanaCCM, ili upate ulinzi lazima uwe mwana CCM, ili upate elimu lazima uwe mwana CCM, ili upate matibabu lazima uwe mwana CCM...huo ni ukosefu wa hekima na utu.
Kuna siku kitanuka na historia ilitakiwa itupe fundisho lakini tumeamua kwa makusudi, kama mbuni, kuficha vichwa vyetu mchangani. Hatari iliyo mbele yetu hawa wakurupukaji katika majibu hawawezi kuyaona; yako majibu ambayo hapo awali hungeweza kuyaona humu mitandaoni. Lakini kwa kuendelea kuongozwa na viongozi wasio na vision na wenye mihemuko taifa linazidi kuporomoka kwa kasi ya kutisha...inasikitisha sana.
Na Yericko Nyerere