Upotoshwaji juu ya mama wa kambo

Hawa mama wa Kambo wa sasa kidogo wameelimika! Wewe tuulize sisi tuliolelewa na mama wa kambo Malimbukeni....miaka ya 90,kurudi nyuma huko...
Nakubali kwa sasa haki za watoto na ustawi wa jamii vimepunguza ukatili kwa watoto ila miaka ya nyuma hali ilikuwa mbaya zaidi.
 
Umeolewa? Kama bado njooo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana , na mara nyingi watoto wao huwa mbulula tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daa pole sana, bora alimalizia maisha yake mkiwa vizuri,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati mwingine mama anakuwa mzuri ila watoto mwenyewe sasa na akijua huyu si mama yake daa kiburi dharau, kuna wengine hufundishwa na mama yake kabisa uwe unamjibu vibaya, kuna mmoja baada ya kuachana na mmewe naye kuoa mke mwingine akawa anapita pale eti wewe house girl wa watoto wangu vipi.[emoji44] sasa hapo unategemea nini watoto wako watapokea nini hapo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na ndicho kinachochafua taswira ya mama wakambo .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lipo kwenye Jamii imeshazoeleka ivyo kuwa mama wa kambo ni mtu mmbaya lakini Kuna mama wa kambo wenye mioyo yenye huruma Kama mama wa mleta mada.

Mama angu mdogo aliolewa kwenye familia ambayo tayari alikuta watoto Tena Ni wadogo mkubwa alikuwa na miaka mitano mdogo miaka mitatu..Mama yule aliwalea wale watoto Kama wake na mapenzi yote..lakini aliyoyapitia kwenye kulea wale watoto Ni mateso kutoka kwa mtoto mkubwa ambaye ni wa kike akishirikiana na mama mkubwa wa wale watoto..juzi tu hapo baada ya wale watoto kupatwa na janga yule mkubwa ndiyo kaanza elewana na kumuheshimu Mama yao wa kambo.
 
Sasa siunaona mama mzazi hapo ndio anataka kuwa chanzo cha wanawe kuteseka kisa chokochoko tu.
 
Na ndio lengo la Uzi huu. Niltaka jamii itambue mchango wa MAMA wa kambo katika malezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwaka 84 dingi alikua anaoa mke mwingine,wakati huo mlezi wangu ni bibi mkewe babu.kisha tukaanza maisha ya kifamilia mimi dingi na mkewe mpya,na muda si mrefu na sis akazaliwa.kipindi hiki ubaya na wema havikupishana sana ktk mizani sababu ya utoto.miaka kadhaa tukiwa sumbawanga mji wenye baridi njombe imesingiziwa,ndio mizani ikakaa sawa.na nikajua huyu ni mtu mwema,nakumbuka sauti yake akitufukuza tusimfate anapowasindikiza wageni lkn hatusikii.kisha wakati anarudi tunaungana nae huku akitupigia stori.nakumbuka baba akiwa hayupo alivyohangaika na mguu uliovimba kwa kuchomwa na msumari,nakumbuka ktkt kotaz za pale jangwani zilizo karibu na msitu wa wilayani huku mvua kubwa kabisa ikinyesha nimejificha bustanini namuona akiwa ameroa anapita vibaraza vya nyumba nyingine,huku akiniita,nakumbuka barazani kwetu kulikua na meza.mbovu.hilo lilikua chimbo lake la kunifichia chakula.kisha nakumbuka wakati anafariki agakhan anamwachia maagizo dada yake ,akimwambia dada wanangu.kuna mwaka nilikwenda arusha likizo nikakaa na mama mzazi mwezi tu.akilini ikaingia hisia nikiambiwa nichague namchagua wa kambo.alikua mtu mwema hata baba alipotangulia mapenzi hayakupungua.kama alikua na makosa meeeeeeengi kwa mungu,basi malezi aliyonilea yanatosha kumpa msamaha huko aliko.aliitwa mama mimi,sio mama mwanae wa kumzaa.eeh mola mlezi.mmiliki wa viumbe.muhurumie yule mama,alinihurumia sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hyo inategemea roho ya mtu, ni kweli wamama wa kambo wengine wamejaliwa roho nzuri had unaweza usijue kama sio mama mzazi.

Kuna mama aliolewa akakuta watoto wa huyo baba wakubwa kiasi, aliwalea kama watoto wake kwa kuwapa upendo wa mama hadi watoto wakawa watu wazima wanajitegemea. Bahati mbaya yule mama hakufanikiwa kupata mtoto kwa mda wote alioolewa hapo.
Last yr mwishoni yule baba alifariki, ndugu wakaanza vimbwanga na kutaka yule mama aondoke kwenye nyumba ya ndugu yao kwa kisingizo kua hawezi kurithi mali hana mtoto (yule mzee alikua tajiri so aliacha mali nyingi tu) wale watoto ndio walikua watetezi wake, walikua tayari kugombana na ndugu zao kwa ajili ya yule mama hadi mwisho wa siku ndugu ikabd wawe wapole wakamuachia yule mama kila kitu.

Nikakumbuka ule msemo wa "Wema Hauozi"
 
Duh! Story yako ipo serious kidogo ila kuna kitu chakujifunza na kikubwa ni kwamba Baba ndio chanzo cha mateso ya mama wa kambo kwa watoto. Mana kama baba kaolewa na kabeba na wanae kapeleka unahisi atakuwa na sauti apo.? Lakini pia hata mzee hakuwa fair mana kashindana na wanawake wawili ( japo mama yako hujamzungumzia huenda na yy walishindana) ko mpaka hapo mzee ndo chanzo cha yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…