Upotoshaji wa Malisa juu ya hali ya kiuchumi nchini wajibiwa kwa umahiri mkubwa

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,283
3,274
HII NDIO MAKALA YA MALISA

By Malisa GJ,

Leo gazeti la Mtanzania limeripoti kufungwa kwa Hotel kadhaa za kifahari kutokana na sababu mbalimbali, lakini SABABU KUU iliyotajwa ni hatua ya serikali kuzuia mikutano yake kufanyika hotelini, badala yake ifanyike kwenye kumbi za serikali na kudaiwa kodi (Mtanzania, Julai 14, 2016, uk.3 na 4).

Nilitamani kufanya uchambuzi wa kina kuhusiana na hali hii lakini nizungumze kwa kifupi kwa sababu niko 'field' huku kwa wanyantuzu natafuta karo ya shule ya mwanangu.

Nionavyo uamuzi huu wa serikali una faida na hasara zake.

#FAIDA_KWA_KIFUPI;

#Mosi; Mzunguko wa fedha utapungua na hivyo kusaidia sana kucontrol inflation rate (mfumko wa bei, unaotokana na monetary factor sio production factor). Sifa mojawapo ya fedha ni isiwe holela. Pesa ikiwa holela inasababisha mfumuko wa bei (inflation by monetary factor). So pesa inatakiwa ipotee kidogo, iwe adimu lakini si adimu sana (money should be scarce but not very scarce).

Kwahiyo pesa ikipotea kdg hata bei ya bidhaa na huduma itashuka. Maana yake ni kwamba bidhaa zitakuwepo lakini pesa hamna kwa hiyo itabidi zishuke bei. Hii itawaumiza wafanyabiashara lakini itawasaidia sana walaji.

Na hii ni mbinu nzuri sana ya kudhibiti uchumi. Bidhaa na huduma vitapungua bei sana. Kwa mfano Hotel ambayo ulikua ukilala kwa 400,000/= kwa usiku mmoja, muda si mrefu utaanza kulala kwa 100,000/= na zile za 100,000/= zitashuka hadi 40,000/=. Mfuko wa Cement kama unanunua 15,000/= tegemea kununua 8,000/= muda si mrefu. Hii ni habari njema kwa walaji (Consumers) lakini habari mbaya kwa wazalishaji (Producers) na wafanyabiashara.

#Pili; Njia hii itasaidia sana kuleta "nidhamu ya kazi". Kwa kuwa mzunguko wa pesa utakuwa mdogo itawalazimu watu kufanya kazi kwa bidii ili kupata pesa. Enzi za kupata pesa kiulaini zimekufa. Enzi za kumuandikia Mkuu wa Idara "minutes" na kujifanya mlikua na kikao, halafu mkuu wa Idara anasaini mjilipe posho, enzi hizo zimekwisha rasmi. Sasa ni kazi tu.

Kama unataka pesa fanya kazi, kama hutaki utakula jeuri yako. Kwahiyo kuanzia sasa watu watafanya kazi kwa bidii na uchumi wa nchi utakua kwa kasi. Utashangaa kuuziwa mfuko wa Cement 7,000/= lakini utashangaa zaidi kwamba unafanya kazi siku mbili hiyo 7,000/= huipati. Kutakuwa hakuna namna nyingine zaidi ya kuongeza bidii.!

#Tatu; Njia hii itasaidia sana kuimarisha sarafu yetu. Moja ya mambo yaliyokua yakichangia kuporomoka kwa sarafu yetu ni inflation rate kuwa kubwa sana. Sasa kwa utaratibu huu wa JPM inflation itakuwa controled kwa hiyo pesa itapotea mitaani.

Na pesa ikipotea maana yake itatafutwa. Na ikitafutwa means demand yake inaongezeka. Na demand ikiongezeka means thamani yake pia inaongezeka. Kwahiyo pesa ikipotea means demand yake inakua kubwa. (Law of demand; price falls with increase of demands, and vice versa). Kwahiyo usishangae hadi kufika mwaka 2020 Dola 1 ya kimarekani ikauzwa Shilingi 1,000/= au chini ya hapo.

Pia kwa kuwa mzunguko wa pesa utakuwa mdogo watu hawatafanya tena shopping nje ya nchi, kwa hiyo watanunua zaidi bidhaa za ndani na hivyo kusaidia kuimarisha sarafu yetu.

#Nne; Njia hii itasaidia kuleta nidhamu ya matumizi. Yani mtu akipata hela ataitunza vizuri na kufanya saving maana hajui kama kesho atapata tena. Unajua watu hawakuwa na nidhamu kabisa ya matumizi. Ulikua unakuta mtu anaenda bar weekend moja anatumia Milioni moja inaisha.

Wiki inayofuata anaenda tena na milioni bar inateketea. Ananunulia watu pombe, anahonga kila mwanamke anayemrembulia, akienda "Live band" kila jina lake likitajwa anatoa laki moja. Lakini kuanzia sasa nidhamu itakuwepo. Hakuna mtu atakayekua na ujasiri wa kufanya mbwembwe za kijinga tena kama hizo. Nidhamu ya matumizi itaongezeka sana.

#Tano; itasaidia kupunguza ombwe (gap) kati ya wenye nacho na wasiokua nacho. Ngoja nikupe mifano michache. Kuna watumishi ambao mishahara yao haizidi milioni moja lakini walikua na uhakika wa kuingiza milioni 5 hadi 6 kila mwisho wa mwezi kwa "deals" mbalimbali. Mara vikao, mara safari, mara manunuzi (procurement wanakula 10%) etc.

Kwahiyo unakuta mtu ana kipato cha milioni 7 au 8 kwa mwezi, anajiona juu kuliko wewe ambaye kipato chako ni laki 8. Anafanya shoping Nakumat wewe shoping yako Mwenge. Lakini kuanzia sasa ngoma droo. Wote mnaenda kuhemea sokoni Buguruni malapa.

#Sita; Maskini wataanza kumiliki ardhi na bei ya ardhi na viwanja itaanza kuwa "affordable" katika maeneo mengi. Unajua ardhi ilikua inapandishwa na "wapiga dili". Mtu amepata hela zake bila jasho anaenda kununua ardhi kwa mamilioni na kusababisha ardhi ya eneo hilo kupanda thamani. Kama mnakumbuka ile skendo ya boss mmoja wa shirika moja la hifadhi ya jamii aliyenunua ardhi Arusha kwa milioni 5 halafu akaiuza kwa shirika analoliongoza kwa shilingi bilioni 1.

Sasa imagine ardhi imepanda thamani kutoka Milioni 5 hadi nilioni 1 ndani ya mwaka mmoja. Kwahiyo wenye ardhi jirani na hapo wakiona mwenzao kauza Bilioni 1 nao wanapandisha bei. Lakini kuanzia sasa "discipline" itakuwepo. Mfumuko wa bei katika ardhi hautakuwepo tena kwahiyo hata maskini watakuwa na uwezo wa kununua na kumiliki ardhi.

#HASARA_KWA_KIFUPI

#Mosi; watu wengi sana watapoteza ajira kutokana na sekta nyingi za uzalishaji kufungwa. Jiulize mahoteli yote yaliyofungwa wafanyakazi wanaenda wapi? Na sio kwenye mahoteli tu, viwanda vitafungwa, makampuni na mashirika yatapunguza wafanyakazi. Wote hao wataenda kulundikana mtaani na kugeuka kuwa tegemezi.

#Pili; Taasisi nyingi za fedha zitafilisika. Mabenki yaliyozoea kukopesha wafanyabiashara kwa riba kubwa sasa hivi yatakosa wateja, na hivyo "ku-run bankrupt". Kwahiyo tutegemee mabenki mengi kufa, na machache yatakayo-survive yatapunguza wafanyakazi pamoja na kufunga baadhi ya "branches" zake.

#Tatu; Sekta nyingi za uzalishaj na fursa za ujasiriamali zitadumaa. Hii ni kwa sababu hazitakuwa na mitaji na pia wananchi hawatakuwa na purschasing power ya kuweza kumudu gharama ya baadhi ya bidhaa.

Kwamfano mtu alikua anaweza kwenda bank akakopa milioni 500 akaanzisha duka la kuuza vitu vya ndani kama furniture, mafriji, TV set, na akapata wateja wengi ndani ya mwaka mmoja akarudisha mkopo wa benki akaanza kula faida.

Lakimi kuanzia sasa hivi wajasiriamali wengi hawatathubutu kukopa. Na wakikopa hawatakuwa nacuwezo wa kulipa. Kwa hiyo mfanyabiashara akinunua bidhaa za milioni 500 akaziweka dukani, halafu baada ya mwezi mauzo ni laki 6, lazima atafute sumu ya panya atangulie akhera madukani.!

#Nne; Kuyumba kwa bei katika soko la hisa kwa sababu baadhi ya wanahisa katika makampuni mengi wanaweza kuuza hisa zao kufidia mikopo yao benki. Na kwakuwa fedha itakuwa adimu (scarce) watalazimika kuuza hata kwa bei ya hasara hali itakayosababisha soko la hisa kuyumba.

#Tano; kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu. Kwa kuwa watu wengi watapoteza kazi, wengine biashara zao, wengine watapoteza dili zao za kuwaingizia kipato, watalazimika kutafuta njia nyingine ya kuishi. Na njia Rahisi ni kujiingiza katika vitendo vya kihalifu. Ujambazi, Ukahaba, Utapeli, Wizi etc.

Kwahiyo tutegemee kusikia matukio mengi ya ujambazi na unyang'anyi wa kutumia silaha katoka maeneo kama benki, super markets, Bureau de change, na hata majumbani. Hakuna mtu atakayekua tayari kukuona unatoa milioni 1 ATM akakuacha hivihivi wakati yeye ana siku ya pili hajala.

#HITIMISHO:
Sisemi Rais aendelee kubana matumizi au aache. Nachotaka kusema ni kuwa apiime kati ya faida na hasara kisha afanye maamuzi kwa maslahi ya nchi. Zipo faida na hasara nyingi zaidi ya hizi. Hapa nimeeleza kwa kifupi tu, lakini najua Rais anao washauri wazuri wa masuala ya kiuchumi watamsaidia kumshauri vizuri kwa maslahi ya "Mama Tanzania"

Malisa G.J
=======

HAYA NDIO MAJIBU YA MAKALA HIYO

ACHENI WATU WAISOME NAMBA ILI TUPATE MAENDELEO.

Anaandika Rashid Chilumba.

Rafiki yangu Malisa Godlisten ameandika makala maridhawa leo ikigusia kile alichoita maoni yake juu ya Hali ya uchumi nchini.

Well, ni makala iliyosheheni, ambayo Malisa ameiandika kutokana na ripoti za hivi karibuni kuwa kuna kudorora kwa shughuli za uchumi kama sekta ya hoteli n.k kiasi nyingine imelazimika zigeuzwe makazi ya wanafunzi (Hostels).

Kwenye makala hiyo Malisa amejaribu kueleza kuwa hatua ambazo serikali ya Magufuli inazochukua tangu kuingia madarakani ndiyo chanzo cha yote hayo yanayotokea, na ameonya kuwa yanayojiri yanaweza kuwa na faida na hasara kwa taifa na kumtolea wito Rais na washauri wake kuchagua kati ya faida na hasara.

Lakini kupitia andiko hili namjulisha Comrade Malisa kuwa hayo anayowaza hayapo na hayawezi kutokea na katika hayo anayofanya Magufuli hakuna faida na hasara bali Kuna Uhalisia na Maendeleo.

KWANINI?

Comrade Malisa katika andiko lake anadhani kuwa hiki anachokifanya Rais Magufuli sasa (kama kuzuia safari za nje, mikutano na semina kufanyika ndani ya Kumbi za serikali badala ya hoteli, machapisho ya Serikali kupungua n.k) ni sera ya kufunga mkwiji (Austerity Measures) ambazo kimsingi ndiyo huleta hizo faida na hasara alizoorodhesha.

Lakini ukweli ni kwamba serikali ya Magufuli haijaimpose sera za kufunga mkanda (No austerity measures imposed) hivyo hisia za Malisa juu ya hasara na faida kwa hatua anazochukua Rais hazipo (Non existing gestures).

SERA ZA KUFUNGA MKANDA NI NINI ? (What are the austerity measures?)

Sera za kufunga mkwiji ni mipango ya kusudi na ya lazima inayochukuliwa na serikali ili kukabiliana na nakisi katika bajeti na uwezo wake wa kifedha. Yaani, kufunga mkanda kunatokana na serikali kuwa na ombwe kubwa kwenye bajeti yake (Huge Budget Deficit) na uwezo wake wa kupata fedha ikiwemo kukopa kwenye mabenki na masoko ya mitaji umefikia mwisho,

Hivyo ili kukabiliana na Hali hiyo, serikali inalazimika kuanzisha sera ya kubana matumizi Bila hiyari yake (Circumstances forces the Government to impose austerity measures).
Mfano mzuri wa hili ni Ugiriki na mzozo wake wa madeni kwa wale wanaofatilia.

SASA SERIKALI INAFANYA NINI KUFIDIA NAKISI YA BAJETI NA UWEZO FINYU WA KIFEDHA WAKATI WA AUSTERITY?

A. Kupunguza matumizi katika shughuli za umma (shule, hospitali, Bima ya Afya, mifuko ya Hifadhi, miundombinu n.k). Hakuna au fedha kidogo zinaelekezwa huko ili kupunguza matumizi.

B. Kupunguza wafanyakazi katika sekta ya umma, kupunguza masaa ya kazi au umri wa kustaafu (hapa lengo ni lile lile serikali kupunguza mzigo wa kutumia fedha zake zaidi)

C. Kuongeza kodi kwa viwango vikubwa hasa inayomlalia mlaji (ili serikali ijiendeshe ki maskini lazima ipate pesa, na kwa kuwa haiwezi kukopa njia pekee ni kuongeza pakubwa kodi kwa raia wake).

Hatua zote hizo juu na nyingine nyingi ambazo serikali hulazimishwa kuzichukua ndiyo huja na mkururu wa faida na hasara ambazo Comrade Malisa amezisemea.

JE SERIKALI YETU IMEANZISHA SERA ZA KUBANA MATUMIZI?

Jibu ni HAPANA.

Ukitazama maana na sifa ya Austerity Measures anazodhani ndugu Malisa kuwa zimechukuliwa na Serikali ya Magufuli hakuna uhalisia wowote kuwa Magufuli ameimpose Austerity Measures, maana serikali haijafanya chochote katika hayo yanayotajwa kuwa ishara za Austerity measures.

KIVIPI?

MOSI
, Serikali ya Magufuli haijapanga wala haina mpango wa kupunguza wafanyakazi, kuharakisha Muda wa kustaafu au kusitisha ajira bali imechukua hatua za hiari za kupambana na wafanyakazi hewa, kuajiri katika sekta za msingi na kupitia upya mfumo wa menejimenti katika utumishi wa umma ili kuondoa gharama zisizo za lazima na kuongeza ufanisi wa serikali. Huko sio kubana mkwiji ni uhalisia.

PILI, serikali ya Magufuli haijapunguza hata senti ya matumizi yake katika miradi ya umma, zaidi ndiyo bajeti yake imeongezeka maradufu, katika serikali iloyoimpose austerity measures huwa hakuna fedha za maendeleo zaidi ni fedha kiduchu tu kukamilisha miradi iliyoanzishwa zamani. Lakini bajeti ya mwaka huu serikali itatumia matrilioni katika ujenzi, shule, hospitali, madawa n.k hivyo hakuna austerity measures ni uhalisia.

TATU, serikali haijaimpose kodi za kutisha kwa watu, bajeti ya mwaka huu ndiyo yenye unafuu wa kodi kuliko zilizotangulia, kodi nyingi zimepanda kiasi na hakuna kodi kabisa kwenye bidhaa za mafuta ambazo ndizo huvuruga bei sokoni kutokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji. Hivyo hakuna austerity measures bali ni uhalisia.

Hivyo kwa kuwa hakuna sera za kubana mkwiji hakuna hasara wala faida alizoorodhesha Malisa.

SASA SERIKALI YA MAGUFULI INAFANYA NINI?

Kifupi serikali ya Awamu ya Tano inachofanya tangu kuingia madarakani ni kile tunachoweza kukiitia kwa maneno mafupi KUONDOA UHOLELA KATIKA UCHUMI.

Serikali ya Magufuli inachukua hatua ambazo serikali yoyote serious duniani inapaswa kuzichukua na unazichukua kwa hiyari ili kuleta maendeleo na si kwa lazima kama Austerity Measures. Sasa kuondoa uholela katika uchumi hakuleti faida na hasara, kunaleta uhalisia na Maendeleo.

Hiki tunachokishuhudia sasa cha mahoteli kufungwa, bar kukauka wateja, shopping kupungua, watu kuwa na nidhamu ya matumizi n.k ndiyo Hali halisi HALISI inayotakiwa katika uchumi unaosimamiwa vizuri (A well regulated market economy).

Hivyo yanayojiri na matokeo yake siyo hasara wala faida bali ndivyo uchumi imara wa soko uliosimiwa unavyopaswa kuwa.

Kwa miaka kadhaa sasa tumekuwa na mfumo holela uliosababishwa na udhaifu mkubwa wa kidola ambao ulisabisha faida kwa wachache na hasara kwa wengi. Watu wachache walikuwa na uwezo mkubwa wa kifedha kuliko wengine na kwa bahati mbaya uwezo wao haukotokana na kufanya kazi bali wizi, ufisadi na ukwapuzi wa fedha za umma na madili ya ujanja ujanja.

Hivyo watu hao ndiyo walifungua mahoteli, majumba ya kifahari, wakifanya shopping Nakumat n.k kwa hiyo kwa kuwa sasa mbinu zao zimebanwa ndiyo (hao wachache) wanatetereka maana hakuna dili tena wala hakuna pesa ya bure. Na hivyo ndivyo nchi inavyopaswa kwenda.

Sasa kwa kuwa Hali ni HALISI kwenye uchumi na sio Faida au hasara kitakachofuata ni Maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa.

1. Uchumi wa taifa kwa sababu ni halisi utabaki katika mikono salama ya wafanyabiashara Wasafi na wenye kufuata taratibu. Hiyo italeta kodi ya kutosha serikali na ajira za kutosha. Njia za panya na ujanja ujanja uliwazuia watu wengi wakweli kuwekeza kikamilifu kwa sababu walikuwa wakijiendesha kwa hasara. Wewe unalipa kodi mwenzako halipi, sasa utaongeza vipi mzigo mwingine? Lakini sasa ni shwari hence maendeleo tu.

2. Kwa sababu ya Uhalisia, serikali itakuwa na fedha za kutosha hivyo kufadhili miradi mingi ya maendeleo na kutoa nafasi nyingi za kazi na fursa mpya. Wale watakaotemwa na hatua hizi katika hoteli au shughuli zilizotokana na fedha za ujanja ujanja watapata kazi mpya katika maeneo mapya ya fursa nyingi zitakazojitokeza baada ya Serikali kuwekeza kwenye miradi mikubwa.

Mf. Serikali ikiwekeza kwenye miradi ya ujenzi kampuni nyingi za bidhaa na huduma zitafunguliwa na watu wenye fedha halali na hivyo kutoa nafasi za ajira kwa vijana wengi watakaotemwa na mfumo haramu.

3. Uchumi halisi na usio na njia za panya utavutia wawekezaji wa nje na ndani hivyo kuchangia pato la taifa, kutoa ajira na hatimaye maendeleo.

NA KADHALIKA.

Kwa ujumla hakuna hasara zozote tunazoweza kuzipata kutokana na hatua hizi za serikali ya Awamu ya TANO za kurejesha nidhamu zaidi tutapata Uhalisia katika namna nchi na uchumi unavyoendeshwa na hatimaye maendeleo endelevu.

Kwa kifupi huko yanayojiri sasa sio matokeo ya kufunga mkanda (austerity measures) bali ni KUSOMA NAMBA.

WACHA TUISOME NAMBA..

#TufanyeKazi #KaaChonjo.
 
Weka makala ya Malisa kwanza juu ya huu uzi wako ili kwa wale ambao wakuiona hiyo makala ya Malisa waisome kwanza ndipo sasa wajue kama huu ulioandika hapa ndio umahiri au la!
 
....sijaona cha maana alichoandika; km mahoteli yanakosa wateja na kulazimika kupunguza wafanyakazi unategemea nini?, uchumi gani unaokua kwa mtindo huu?

Unataja moja ya austerity measure ni kupunguza wafanyakazi wa umma, sasa mbona sekta binafsi ndio inayopunguza wafanyakazi na ndio yenye wafanyakazi wengi zaidi?, ndio kukuza uchumi huku?!
naona kajitutumua tu,hajaandika chochote cha maana!
 
Serikali kuhodhi pesa au kukusanya fedha nyingi sio ishara ya kuwa serikali inafanya vema kiuchumi. KUKUSANYA Kodi nyingi kwa kuweka viwango vikubwa sio ishara ya kukua uchumi.

Uchumi wetu kwa sasa ni kodi zitokanazo na biashara. Uchumi hukua kwa kukua biashara hizi na sio kukamua kodi kwa biashara hizi..

KUKUA Uchumi ni kukua kwa uwezo wa kununua wa raia.. Maana ya kuongezeka pato la raia.. Na Kufanya kuongezeka uwezo wa matumizi..

Kinachofanyika sasa ni kukusanya kodi kwa njia zote, biashara zina shuka na uwezo wa wananchi kimapato nao una shuka. Hivyo uchumi unashuka.. SERIKALI Inakalia mahela yake ya kodi.

HATIMAE Tusubiri recession au utapia mlo katika uchumi..
Swali la msingi hapa je hizo fedha serikali inazitumia kwa kazi gani?
 
Mimi binafsi nimesoma hiyo makala ya Malissa yooote huko fb,kiasi kikubwa hoja alizoandika hujazijibu kama alivyozianisha yeye,.....

Inawezekana ukawa na majibu mazuri sana ya kumjibu ila naona kama una haraka presha au mhemko flani hv,hebu tulia soma tena andiko la Malissa ambalo nimelipost hapo chini then umjibu kwa utulivu....

Kwa mtu aliyesoma ile makala ya Malissa na majibu uliyoyatoa hapa hayaendani.....

MAKALA YA MALISA NIMEIPOST HUMU JAMANI,KAMA INAWEZEKANA MODS MNISAIDIE KULIWEKA VIZURI AU KUIUNGANISHA NA COMMENT HII..
 
Nimeshangaa huo umahiri....wa majibu....sasa ni dhahiri hali ya uchumi wa wananchi wa kipato cha chini ni tete je...huo ni ukuaji wa uchumi ??au ndo kila mtu anakuja na kujitutumua kujibu ,vitu visivyo hapa......
 
Watanzania wanataka maendeleo, wengi wao hawaijui gharama ya maendeleo. Maendeleo ya kweli hayana maisha ya ujanja ujanja, ni kufanya kazi zaidi, kujituma zaidi, ubunifu zaidi na vipaji zaidi. Katika kipindi hiki cha kufunga uholela tegemea mahotel zaidi, bar zaidi kufungwa. Itafika ile hatua mtaani kuna supermarket moja au mbili basi, bar moja au mbili basi. Utakapoona watu wanakunywa bia weekend tu bila shurti basi ujue imekuwa!!!
 
mzee mmoja alikuwa anaota anaambiwa hivi: 'nnji' yenu inaharibiwa na 'wasomi'. kuiba wao,ufisadi wao,uongo wao,mikataba ya kifisadi wao,mipango mibaya wao,wizi mkubwa wao,ushauri mbaya wao,uandishi wa kishabiki wao,ushabiki wa siasa mbaya wao,kupigiana makofi hata wakikosea wao. hawahasaidii ila kwa maslahi'. akastuka usingizini. akaanza kuomba dua 'ee mungu wape imani 'wasomi' wetu waanze kuwa wakweli na waache unafiki,wafanye kazi kwa maslahi ya watu wote na sio vyama vyao......aaaamin'
sikujua kilichoendelee
 
Binafsi kama raia wa kawaida kabisa nnahitaji maisha yangu yaboreke hasa katika mahitaji yanayo nizunguka kama binadamu,nimeishia kusikia matamko kutoka Serikalini na wapambe wa Serikali kuwa hali ni nzuri kwa sababu tunakusanya mapato makubwa sana sasa tofauti na awali na blah blah za hapa na pale .Nimesalia nikishangaa mbona mtaani hali ndio imekuwa ngumu zaidi kila unacho kigusa kimepanda bei na chapaa hamna mifukoni ,bado niendelee kuyaamini maneno haya !!?..Walau Mama Samia (Makamu wa Raisi ) alikuwa mkweli kiasi alipotuasa tuvumilie kwa muda mambo yatakuwa sawa..

Nimkumbushe tu mama yetu huyu kuwa uvumilivu una kikomo mama ,tunaaibika ktk familia zetu .Kipato tunacho kipata ktk shughuli zetu hakitoshei matumizi yetu kiasi ukitokea ugonjwa huwa balaa tupu ....
 
Makala ni nzuri lakini uelewa unakuwa wa taabu kutokana na kutumia sana maneno ya kiingereza. Pia inampa shida msomaji kufuatilia mtiririko wa mantiki kwenye hoja zilivyowasilishwa. Kwa mfano "hajaimpose", "ameimpose", au "shopping".
 
Huu ndio ukweli sabab watanzania tulio wengi tulizowea kuishi kwa deal na ujanjajanja sasa ndio tutaishi maishi halisi .

Chukulia mfano kodi za nyumba zinavyo lipwa ni nchi peke duniani unatakiwa kulipa kodi kwa mwaka mzima.

Pili angalia bei za nyumba zinavyo uzwa hazilingani na uhalisia wa kimazingira au miondo mbini hasa Dar es salaam.

Hizo ni dalili za hela chafu zilizo kuwa zikipatikana ktk mfumo wetu wa maisha tuliouzowea.

Ongozea na ww
 
Mimi binafsi nimesoma hiyo makala ya Malissa yooote huko fb,kiasi kikubwa hoja alizoandika hujazijibu kama alivyozianisha yeye,.....

Inawezekana ukawa na majibu mazuri sana ya kumjibu ila naona kama una haraka presha au mhemko flani hv,hebu tulia soma tena andiko la Malissa then umjibu kwa utulivu....

Kwa mtu aliyesoma ile makala ya Malissa na majibu uliyoyatoa hapa hayaendani.....
KAMA NIMEKOSEA NAOMBA UNISAMEHE...
wala mkuu haujakosea alivyojibu ndivyo malisa alivyoandika kwa lugha nyingine ame copy
 
Back
Top Bottom