Upotoshaji wa DAS Mwakiposa wajibiwa kwa Majibu yaliyoshiba

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Nimesoma andiko la ajabu la Das Mwakiposa


Andiko hilo limejaa upotoshaji mkubwa,muhimu kujua majukumu ya DAS ni nini,na anawajibika wapi

1.Kuhusu posho

Madiwani huwa hawajilipi posho bali hulipwa kutokana na sheria,taratibu na mwongozo unaotolewa na Tamisemi.Mwaka 2008 baraza la madiwani wakati huo lilipitisha posho ya usafiri kuwa 40,000, ambayo imeendelea kulipwa hadi leo na iliridhiwa na waziri mwenye dhamana wakati huo! posho ambazo zipo kisheria kwa mujibu wa kanuni ya 54 ya Sheria ya serikali za mitaa ni

Posho ya madaraka

Posho ya Kikao

Posho ya usafiri

Per diem

Posho ya malazi(kwa halmashauri kubwa kama Simanjiro,Ngorongoro etc)

Posho ya madaraka(Wenyeviti wa kamati mbalimbali Meya etc)

Hakuna pahali popote wala wakati wowote madiwani wa Jiji wamejilipa nauli ya 80,000.Arusha inatumia mfumo wa malipo wa Epicor ambao ili fedha itoke lazima iwe kwenye bajeti na iwe na vote,na sote tunajua kuwa bajeti hupitishwa na bunge kisha hutungiwa sheria,

Tuna uzoefu wa kufanya kazi bila posho,mwaka 2010-2014 hakuna diwani wa CHADEMA aliyepokea posho hata senti tano,kutokana na mgogoro wa umeya wa wakati huo

Local fundi,Das amehamishiwa Arusha mwaka 2016 akitokea Sinza alikokuwa mtendaji wa kata ya Sinza.Tumeanza kutumia mafundi hawa kupitia sheria ya manunuzi ya Community participation mwaka 2015 baada tu ya kuingia madarakani.Wakati tunagombea tulikuwa na ajenda baada ya kushinda tukaanza kutekeleza.Msingi wa kutumia community participation sio tu kuokoa gharama bali kuleta sense of ownership kwa kuwa hizi ni kodi za wananchi lazima washiriki katika kuijenga Arusha yao,na Arusha waitakayo,Das,RC,DC wamekuja wameikuta Halmashauri ya mfano chini ya CHADEMA yenye ubunifu waaache kujitafutia sifa za ajabu ambazo hawastahili

.....Hata hivo tumewaruhusu wakapige picha ili warushe Fb Bwana mkubwa awaone.....

Madarasa ya sekondari ambayo ni ghorofa nne juu tuliendelea kutumia wakandarasi kutokana na ukubwa wa kazi.Ni Jiji la Arusha pekee lenye shule za sekondar za Ghorofa zenye huduma zote za kijamii,


Hayo mengine ya msibani tunampuuza kwa kuwa anastahili kupuuzwa!

Nanyaro
 
Madiwani wa CHADEMA Arusha baada ya mpango wao wa kujimilikisha maduka maeneo ya stand ndogo kukwama wanamchukia sana Gambo................hawa madiwani wamekula sana pesa za wafanyabiashara Arusha kwa ahadi ya kuwapa maduka pale stand.
 
Madiwani wa CHADEMA Arusha baada ya mpango wao wa kujimilikisha maduka maeneo ya stand ndogo kukwama wanamchukia sana Gambo................hawa madiwani wamekula sana pesa za wafanyabiashara Arusha kwa ahadi ya kuwapa maduka pale stand.
Choko-raa Mzigoni
 
madiwani Arusha wanakwamishwa kutekeleza majukumu yao. kama hakuna dhamira ya kweli ya mfumo wa vyama vingi turudi kwenye zama za chama kushika hatamu.!
 
Jenerali Ulimwengu alisema baada ya Nyerere kulazimisha multiparty politics kumekuwa na rearguard action kukwamisha mfumo huo usifanye kazi na ikiwezekana kuua kabisa. Tumeshuhudia kwa macho yetu tangu 2010. Kadri ushindani unavyopata nguvu ndivyo rear guard action nayo inavyoshika kasi na wahusika kuwa more and more desperate and irrational. Wanyarwanda tuliwashanga kwa kupigana kwa misingi ya ukabila. Nasi tusipopata watu wa Mungu wa kutunusuru, tutafika huko eti kutetea ccm, cdm, cuf.
 
Back
Top Bottom