Upotevu wa mapato stendi ya Ubungo

cassanjr

Member
Aug 13, 2010
37
8
Habari zenu wanajamvi,

Kuna jambo ambalo nimeligundua jana pale Ubungo terminal (stand ya mabasi ya mkoa). Ukiwa unaingia pale getini wanatoza ushuru na risiti yako wanakupatia na wakati unatoka unaiacha risiti yako pale katika geti la kutokea.

Nimeona hawako sahihi kwakuwa upo uwezekano wa kuzitumia risiti hizo hizo kwa wateja wengine kuuziwa kwa mara ya pili. Nashauri wahusika waweke utaratibu kama risiti ikitumiwa kwa kuingia nayo getini basi lazima utoke nayo.

Asanteni
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom