chukua vyote NIACHIE Uporoto01.:angel:
Kwa hiyo yake saini, Cheusi kanisaliti,
Nimeshindwa ushindani, Uporoto ni smati,
Mangala wake mwandani, si yangu hiyo bahati,
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.
Afrodenzi jamani, nawe mfariji Mati,
Preta ukiwa kundini, nijuzeni mikakati,
Cheusi mkuwadini, Poroto apigwe buti,
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.
Uporoto huna dini, si kiumbe ni ngongoti,
Iweje unifitini, unipore langu titi?
Nitalala mang'amuni, labda nile vitoti,
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.
Wapendwa nawaageni, nimeshapigwa kibuti,
Uporoto amewini, leo anafanya pati,
Cheusi kanipiga pini, nakoma simfuati,
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.
Kaditama niahuni, nimekwaa kizingiti,
Cheusi kenda mitini, na kivulanache njiti,
JF nishaurini, nilizushe valangati?
Nimeshindwa mkakati, Uporoto amewini.
Kashaija ndugu yangu, nakugea zangu pole,
Ulienda wanguwangu, ukajikwaa kidole,
Alichokipanga Mungu, kiwezi kuwa kipele,
Jaribu tena kwingine, Cheusi kwako haramu.
Ila onyo nakugea, Siguse jukuu wangu,
Usije tena kulia, Nikiwarudisha kwangu,
Wajukuu nimelea, wanitunze peke yangu,
Jaribu tena kwingine, Cheusi kwako haramu.
Afrodenzi angalia, simuweke mawindoni,
Maty wala Roselia, na mwanajamiiwani,
Waisiledi achia, na wengineo sebuleni,
Jaribu tena kwingine, Cheusi haramu kwako.
Dada zangu nakwachia, ukiwaweza chukua.
Preta nakuzawadia, Nyamayao naye pia,
LD kiwezea, Lili Flawa Fukuzia,
Mahari ulete kwanza, Babu ninazipokea