Uporaji dar mchana kweupee! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uporaji dar mchana kweupee!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shadow, Mar 6, 2009.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Nimekutana na hii habari kwenye Blog ya Michuzi nikaona ni bora niilete hapa kwa mjadala zaidi. Nimeunganisha na baadhi ya maoni na matukio yanaoendelea katika jiji la Dar Es Salaam.


  uporaji dar mchana kweupeeeeee

  Leo asubuhi, nikiwa kwenye foleni maeneo ya jangwani, saa 1.20 asubuhi, gari la tatu kutoka gari langu kwa nyuma lilivamiwa na vibaka, wakafungua milango, ndani ya kama dakika 3 wakapora kila walichoweza kupora.
  Ilikuwa ni kwenye foleni, jamaa wana visu, na kila mtu akawa anaangalia kama sinema hivi. HAKUNA MSAADA!
  Watu kwenye daladala la karibu, wakawa wametulia kimyaaaaa. Na walio kwenye saloon cars wakawa wanafunga vizuri vioo ili wasiwe next target. Siku zote hizi WARNING nilikuwa sizipi uzito unaostahili, leo nimekubali. Naomba munielewe, Sizungumzii mtu kupora cheni au simu dirishani.
  Jamaa wamefungua milango, na kunyang’anya kila walichokifikia.
  Tafadhali sio tu ufunge vioo, lakini hakikisha milango imefungwa ( LOCKED) BONGO TAMBARAREEE!
  Mdau OCTAVIAN ‘OC’

  source :MICHUZI

  Tarehe March 06, 2009 10:48 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Jamani, zile difender zimeishia wapi, Tukubaliane kitu kimoja, mambo mengi yanayofanyika Tanzania yanasababisha madhaama sehemu nyingine, mfano, tukimuuliza Muheshimiwa IGP- Mwema, atasema hana askari na vitendea kazi, kang'ang'ania community policing weee mpaka basi, mabilioni yanayopotea kila siku kwenye, Radar, Richmond, Dowans, EPA na nyingine nyingi, zingetosha kabisa kumpa IGP uwezo wa kudhibiti hawa wahuni wachache. Hili tatizo halipo tu Jangwani jamani, lipo Salander Bridge pia, nimeshashuhudia mwenyewe mara mbili mtu akiporwa side mirrors na Handbag. Watanzania tushikamane kuishinikiza serikali kuthibiti hii hali.


  Tarehe March 06, 2009 10:50 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Mdau bora umelitoa hili wadau waweze kuchangia. Hili jambo lipo sana hapa Bongo sielewi ndio life style ya wabongo au vipi. Unaweza ukawa unaibiwa na hata kupigwa mchana peupeee lakini hakuna anayejitokeza kukusaidia hata kama kunawatu wanaopita karibu tena mwenye gari kama yupo karibu ndio anafunga vioo kabisaaa. Kwakweli wabongo tunakosa upendo kabisa kwa wenzetu.

  Nao vibaka siku hizi kutokana na tabia hiyo ya kuachwa wakimuibia mtu hakuna basi ndio wamezidisha hasa. Hayo maeneo ya hapo Magomeni ni kama kawa kwa kitendo hicho kwa wewe ndio mara ya kwanza kuona mimi nilishaona tena vitendo kama hivyo. Inakuwa kama watu wa Magomeni wanawajua vibaka hao na nijamaa zao.

  Hii polisi jamii sijui itaimarika lini ikiwa sisi wenyewe tunaangalia tu hatushiriki kusaidia kupunguza hivi vitendo viovu vikiendelea. Hii inaonyesha wazi huko tunapoelekea tutakuja kuchinjana hivi njiani hakuna pia atakayesaidia.

  Kwa maoni yangu naona pia vibaka wamejiamini sana kutokana na wakimwibia mtu hakuna anayeingilia kumkamata pia hata wanapokamatwa wakienda polisi wanafungwa tu hauzidi mwaka wanatoka msamaha wa Rais ukipita. Hii imepelekea kufanya uporaji kuwa ndio ajira yao. (Mimi nitaiba nikikamatwa poa nitafungwa kwanza gerezani nitakuwa napata chakula cha bure kutofautisha na uraiani na pia muda si mrefu nitatoka kwa msamaa wa Rais au nikikamatwa nitatoa chochote nitaachiwa)

  Pia Kinondoni yani msamaa wa Rais ulipopita yani vibaka wote unawaona uraiani bora maeneo ya studio sio mabaya sana lakini maeneo ya manyanya na Mkwajuni ukipita tu katika mitaa mida ya asubuhi basi wewe ujue utabananishwa na vibaka wakupore vitu vyote.

  Nilinyanganywa simu mchana kweupee, nilipita mtaa mmoja nitokee Kinondoni Stereo nikakutana na kibaka ikawa tunapambana nikijiamini kwani niliona watu kwa mbali kidogo wananiona kuwa watanisaidia huku napiga kelele lakini hakuna aliyekuja zaidi ya kunishangaa hadi kibaka akaning’ata na kuchukua simu.

  NAOMBA WATANZANIA TUBADILIKE..NCHI YETU NI NCHI YENYE AMANI..TUPENDANE, TUSHIRIKIANE, UKIONA MWENZAKO ANAPATA TATIZO KAMA HILO BASI ASIJITOKEZE MMOJA KUMSAIDIA TUJITOKEZE KWA WINGI TUMSAIDIE NDIVYO TUTAKAVYO TOKOMEZA MAOVU HAYA...TUITUNZE AMANI YETU YA NCHI SASAHIVI TUNAPOELEKEA PABAYA...MWENZIO AKIFANYIWA KITU KIBAYA JIHISI KAMA NI WEWE AU NDUGU YAKO KWANI IPO SIKU YATAKUFIKA NA WEWE..

  Mdau H


  Tarehe March 06, 2009 10:52 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

  du sasa bongo kunatisha naogopa hata kurudi kama mambo yamefikia hivo ndugu zetu huko watapona ndo mana mdogo wangu anataka kununua bunduki nikamkataza ya nini bongo kumbe ni muhimu kuwa nayo kwa mambo kama haya nchi inaenda kubaya


  Tarehe March 06, 2009 11:01 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Hii michuzi ni kweli au kamba kali tu kwa bongo yetu hii mambo kama hayo wapi na wapi kwanza sio tamaduni zetu au ulikuwa unaota donto ya mchana kaka


  Tarehe March 06, 2009 11:34 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

  tuache utani bwana serikali inaweza kushughulikia hili


  tunaomba serikali ifannye kazi yake


  Tarehe March 06, 2009 11:56 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Ahsante kwa kutuhabarisha. Naelewa usingeweza kufanya chochote maana wao walikuwa na silaha na wewe huna. Pia ungetoka wangekuvamia na wewe.
  Cha msingi tukumbuke ku lock milango ya magari yetu


  Tarehe March 06, 2009 12:06 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Nimekusoma OC .inabidi wanausalama wa yaangilie sana haya maeneo ya Jangwani ,Salender bridge pia maeneo ya Daraja la Ubungo yamekuwa na matukio mengi sana ya uharifu.

  Afande Kova changamoto hiyo


  Tarehe March 06, 2009 12:06 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Nimekusoma OC .inabidi wanausalama wa yaangilie sana haya maeneo ya Jangwani ,Salender bridge pia maeneo ya Daraja la Ubungo yamekuwa na matukio mengi sana ya uharifu.

  Afande Kova changamoto hiyo


  Tarehe March 06, 2009 12:13 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  mbona na wewe hukusaidia kitu?


  Tarehe March 06, 2009 12:20 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Hii mimi inanishangaza, walikuwepo watu kwenye daladala, na maeneo mengine wameona, halafu wote wameuchuna, kwakuogopa visu na mapanga, hamjui munawapa vichwa hawa watu. Ilibidi watu wajitose, kwasababu na wao walikuwa wanawapima, kwa kujua wengi ni waoga.
  Tusidanganyike, kama hatutajitolea wenyewe tusitegemee polisi watakuwepo kila mahali. Inabidi kujitolea muhanga ili kuinusuru hii hali. Hayeni wachekeeni, kwani leo kwa yule kesho kwako.
  M3


  Tarehe March 06, 2009 1:50 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Hii ni dalili ya baadhi ya wananchi (na hasa wananchi wa chini kabisa kimapato) kukata tamaa na kufikia hali ya kusema, "liwalo na liwe". Hii inatokana na Upumbavu, Ujinga, na Uzembe wa Serikali na watendaji wake (pamoja na Rais) kutumia mida wote wa uongozi wao katika kujinufaisha wao na familia zao binafsi bila ya kujali nchi na wananchi wake.

  Sitetei wezi, na ningependa sana kama hawa vibaka wangeelekeza uharamia huu kwa watendaji wa serikali, na familia zao.


  Tarehe March 06, 2009 2:26 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  wewe unaetaka kumumwagisha mtu ubongo naomba nikuulize swali ulishamwaga wangapi??
  angalia utaishia kunyongwa na ufisadi wenu..
  mnataka wenzenu wafe na njaa?? na ufisadi wenu

  hii ni trela bado picha kamili mtaiona


  Tarehe March 06, 2009 2:29 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  hakuna msaada wa story ukitaka kutoa msaada wape hela hiyo ni njaa tu inawasumbuwa ni ndugu zetu wanahitaji kuishi na kuishi ni kula sasa mnataka wao wafe na njaa.

  waende na nyumbani kwa mkapa watapata hela ya kula mwaka mzima.


  Tarehe March 06, 2009 2:34 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  je ungelikuwa wewe unanjaa na nyumbani kwenu mzazi wako yuko hosp na hakuna hela ya matibabu je ungefanyanini???
  au utamwacha ndugu yako afe na njaa kwa ajili ya mafisadi au utawakaba ili umtibie mzazi wako???
  mimi naona hawanakosa ni kosa la selikali ya mafisadi kuifisadi nchi na kuleta ungumu wa maisha kwa walio wengi.


  Tarehe March 06, 2009 2:37 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  bora mtu ufe kwa kutafuta ridhiki kuliko kufa na njaa poa tu tumieni hizo bastora zenu kama mnaona kuuwa watu ni ufahari wenu mafisadi

  ila azabu zenu za kuibia walala hoi zinaongezeka.


  Tarehe March 06, 2009 2:42 PM, Mtoa Maoni: Mzee wa Zeze

  Hayo yaliwahi kunikuta mwaka 2001 pale kwenye taa za barabarani za Ubungo. Walifanikiwa kunikomba kila kitu nilichokuwa nacho garini na kunijeruhi kwenye bega la upande wa kulia.
  Kwa bahati nzuri mmoja alikamatwa nanatumikia kifungo chake cha miaka 30


  Tarehe March 06, 2009 2:55 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Wadau, anachosema huyu Mdau mwenzetu ni kweeeeeeli kabisa. Wiki iliyopita wameninyang'anya hereni zangu ivi ivi hapo hapo jangwani maeneo ya Kwa Macheni!! Ilikuwa ni saa moja dakika ishirini na tatu (07:23am) nikiwa kwe foleni. Watu walikuwa wameshangaa na kunipa pole tu. Vijana wako Smart huwezi amini wala kudhania. Nawahimiza watu wote mlock milango ya magari yenu na kufunga vioo. Na kwa wale watembea kwa miguu umezuka wizi wa waendesha pikipiki kukwapua pochi za kina dada na kutokomea nazo. Hilo lilitokea mwishonimwa mwezi wa pili maeneo ya Ubungo. Jeshi letu la polisi tunaomba litusaidie kucheki katka maeneo tajwa ili kutunusruru maana itafika mahali sasa wataanza kuchinja watu wakienda Kulijenga Taifa!!!! Sharly


  Tarehe March 06, 2009 2:56 PM, Mtoa Maoni: narsis mboya

  hi wadau
  this is just the beginning
  ngoja watu waanze kupungwa makazini kutokana na hili lirecession linalokuja
  watoto wanamaliza mashule ajiri haba
  sekta binafsi nazo zitajibu mapigo kwa kutokuajiri
  bidhaa haziuziki labda za china!
  nakwambia ni kasheshe tupu
  askari wa doria wapo siku hizi?
  Mdau


  Tarehe March 06, 2009 3:13 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Ni juzi tu niliona katika blog moja ya MR. BOBOS CLASS imetolewa tahadhari baada ya dada mmmoja kuvamiwa hapo jangwani majira ya saa3. Ninachojiuliza mimi ni kwamba, nikiwakama mtumiaji wa njia hiyo kilasiku, huwa naona askari wanapatrol katika eneo hilo. Je, wanakuwa wapi au ndo vibaka wanawa-time?Inatia hofu hofu sana. Je, ukimfyatua na bastola mtu kama huyo inasimama vipi?


  Tarehe March 06, 2009 3:16 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  SAFI SANA.
  Hao jamaa mi nawafagilia sana, maana ni kielelezo kizuri cha hali tuliyiofika najua naweza kueleweka vibaya lakini aliye na macho haambiwi tazama. Hata MUNGIKI waliianza hivi leo wanakaribia kuwa insurgence


  Tarehe March 06, 2009 3:23 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Watanzania wengi ni wagumu sana kuwasaidia wenzao wanapopatwa na matatizo. hivi ni kweli uwingi ule wa magari katika foleni na daladala zote hizo watu wanashindwa kuwa na umoja na kushuka na kukabiliana na majambazi ama wahuni? si pati jibu. hivi kama watu wangeshuka katika madaladala kama matatu hao vibaka wengeweza kufanya unyama huo?
  Tuache uoga wa kihindi wa kujifungia ndani.


  Tarehe March 06, 2009 3:38 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  waacheni jamaa nao wajilipe washaburuzwa sana na mafisadi hao


  Tarehe March 06, 2009 4:17 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  hayo mambo ni kweli kabisa na yanatokea maeneo ya jangwani wakati wa foleni. wiki iliyopita pia dada wawili wafanyakazi wa muhimbili(nurses)waliporwa kwa staili hiyo hiyo. hakuna aliyewasaidia, kwa kuwa vibaka walikuwa na mapanga na visu. walichukua simu, pochi na kila walichoweza kubeba, asubuhi kweupeee


  Tarehe March 06, 2009 4:17 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  hayo mambo ni kweli kabisa na yanatokea maeneo ya jangwani wakati wa foleni. wiki iliyopita pia dada wawili wafanyakazi wa muhimbili(nurses)waliporwa kwa staili hiyo hiyo. hakuna aliyewasaidia, kwa kuwa vibaka walikuwa na mapanga na visu. walichukua simu, pochi na kila walichoweza kubeba, asubuhi kweupeee


  Tarehe March 06, 2009 4:17 PM, Mtoa Maoni: Waefeso

  Nadhani ndo kilichobakia, kuwa na bastola, nadhani serikali ilegeze masharti ya watu kununua silaha, itaongeza discipline.


  Tarehe March 06, 2009 4:42 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

  Duh e bwanaeeeee...Kova atakuwa anayo habari hii na lazima kutakuwa na askari wa doria walipangwa eneo hili!! Mara kibao huwa inatokea pale Jangwani nyakati za foleni haswa asubuhi!Huwa wanafuatilia kilichomo na aina ya abiria waliomo kuanzia magomeni! wakishaona kwamba milango haitawapa shida kufunguka na abiria si mapande ya watu/mabaunsa basi wanali-mark hilo gari na ku-set ambush pale chini Darajani, sehemu ambayo wao kukimbia bila kufukuzwa na umati wa watu wenye hasira inakuwa rahisi!Sasa sijui tufanyeje?maanake pale hakuna ujanja na ni lazima mtu uende kazini saa hizo...KOVA SAIDIA BANA!!
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Askari wa doria kazi yao ni kutafuta wenye makosa ili wawatoe upepo,trafiki nao hawaangalii hata sababu ya foleni zenyewe.Viongozi ni wezi hivyo askari wengi wanatumika kuwalinda wao,raia hawana askari wa kutosha wa kuwalinda.Watanzania tujilinde wenyewe kwa kusaidiana anapovamiwa mwenzetu.Serikali iruhu raia kutembea na vitu vya kujilinda kama visu,sime na chochote kingine au iwahakikishie ulinzi raia katika shughuli zao za kujenga nchi.
   
 3. Sasha Fierce

  Sasha Fierce JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Utamu ina faida na hasara yake.
  Faida- imeweza kuwapa faida wafanya biashara,kuna msichana mmoja walimtoa huko kwenye utamu ana duka lake pale bongo.Na kuna watu walikuwa wanasoma data zake na wakataka kumjua huyo demu wakaenda kutembelea hilo duka lake na kuona vitu anavyouza matokeo yake waka end up kununua.Ni kwamba alianza kupata wateja kwa kwenda mbele.

  Hasara-inaharibia statu za watu,kuna wengine na heshima zao na vitu vinayoandikwa mle ndai.lakini 300% ya maneno yanayoandikwa sometime niyana ukweli na 70% ni uongo mtupu.
   
 4. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Sasha,

  naona umekosea na kupost hapa hiyo issue ya Ze Utamu. Hapa tunaangalia suala la uporaji unaofanyika kwenye foleni za magari hasa katika barabara kubwa za jijini Dar es salaam.
   
Loading...