Uponyaji wa moyo uliovunjika by Denis Lyamuya(Principal Focus)

Principal Focus

JF-Expert Member
Jan 4, 2013
925
550
UPONYAJI WA MOYO ULIOVUNJIKA
Yesu Kristo karibu katika mafundisho haya Roho mtakatifu aniongoze nifundifundishe kwa kadri ulivyonielekeza ili kusudi lako litimie watu wapate uponyaji. Eeh! Yesu Kristo katika jina lako roho mtakatifu karibu katika mafundisho haya. Amina
Uponyaji wa moyo uliovunjika. Isaya 61:1 “Roho ya Bwana I juu yangu: kwa sababu amenituma niwahubiri wanyenyekevu habari njema: amenituma ili kuwa ganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.” Zaburi 34:18 “BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, na waliopondeka kuwaokoa.” Hosea 6:1 “Njoni, tumrudie Bwana maana yeye amerarua na yeye amepiga, na yeye atatufungua jeraha zetu.”
Moyo wa mtu kwa tafsiri nyingine wawez sema nafsi ya mtu au roho ya mtu. Anaposema kuwaponya waliovunjiika moyo hana maana anatibu nje tu kwa jicho la kawaida kama lionavyo but anatibu yale ya roho ili mwili upate afya. Mungu anataka uponyaji wa ndani si wa juu juu tu na kusema amani amani wakati hakuna amani.
Katika uumbaji kuna vitu Mungu hakuumba moyo ubebe na wala dhambi haikuwepo kabisa. Mwanzo 3:1-24 nitakuonyesha mistari baadhi hiyo mingine itakua home work yako ili ujifunze zaidi. “1 Basi nyoka alikua mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, msile matunda ya miti yote ya bustani? 3lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.4 Nyoka akamwambia mwanamke, hakika hamtakufa kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. 22 Bwana Mungu akasema, basi huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na baya: na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima akala, akaishi milele: 23 kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwalia. 24 Basi akamfukuza huyo mtu…”
Kumbe tangu mwanzo magonjwa hayakuwepo wala vita havikuwepo, wala kuachana hakukuepo wala taabu na dhiki za dunia katika uumbaji hazikuwepo, wala katika uumbaji dhambi haikuwepo kabisa sijui kama utakua umepata nafasi ya kusoma biblia yako vizuri utakua umeona dhambi ililetwa na mtu mmoja na dhambi imeondolewa na mtu mmoja ambaye ni Yesu Kristo.wala mauti haikuwepo hakika, moyo wakati wa uumbaji ulipewa uhai ambao ni furaha sio moyo kuvunjika. Au pengine ngoja nirudie hivi nirudie hivi, kabla ya Adamu na Hawa kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya kulikuwa hakuna vita wala moyo kuvunjika, kulikuwa hakuna laumu, masengenyenyo, visasi, mauti, magonjwa, taabu. Mwanzo waliishi kwa fellowship na Mungu kwasababu Mungu alikuwa anawatembelea wala hata hapakuwa na maombi kama sasa. Kwa maana Adamu na Hawa waliishi kwa neon lake pia walimjua Mungu. Lakini kila kitu kilibadilika baada ya Hawa kumshawishi Adamu kula tunda la ujuzi na kulila, Mungu alilaani akalaani ardhi,akwafukuza katika bustani. Akaweka uadui kati ya mwanamke na nyoka etc etc. hivyo ukishajua taabu zote zilianzia wapi ni lazima umrudie Mungu kwasababu anakuita anasema njoni kwangu nyinyi mliolemewa na mizigo kwa maana nyira zangu ni nyepesi na mzigo wangu ni mwepesi. Zamani mtu alikua anaishi miaka mingi sana wengine miaka mia nane nakuendelea. Ngoja tuone kitu hapa huku tukienda taratibu kwenye somo. Mwanzo 6:3,5-6 “3 Bwana akasema, roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.5 Bwana akaona ya kuwa maovu ya wanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.” Sijui kama ulishasoma agano jipya vizuri ukaona mstari umeandikwa au una maana kama hii “na ashukuriwe Mungu kwa maana siku zilifupishwa kwa ajili ya watakatifu, ili wapate kuurithi ufalme wa mbinguni au wapate uzima wa milele.” Siku zilifupishwa ili tuishinde dhambi. Kabla ya agano jipya Mungu aliweka torati tuwe chini ya sheria lakini Yesu alipokuja alitutoa chini ya sheria ilituwe wana wa Mungu. Unasema naongea kitu gani klasome biblia yako katika Wagalatia uone. Torati iliwekwa kabla ya kuja imani ilituishi chini ya sheria. Lakini imani ilipokuja ambayo ni Yesu Kristo tuliwekwa kama watoto wa Mungu ndiyo maana anasema mtu anaye fata sheria lakini halifati jina langu hataingia katika ufalme wa mbinguni. Alifufuka siku ya tatu ili tuishinde mauti na dhambi zake zote, tupone magonjwa yote n.k
Embu tuangalie vipi vinavunja moyo:
1 DHAMBI
Dhambi iliingia baada ya moyo kuumbwa hivyo tangu mwanzo Mungu hakuweka mauti ndani yenu lakini Adamu na mkewe walipotenda dhambi, mauti ikaingia.
2 HASIRA
“Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; wala msimpe Ibilisi nafasi.” Waefeso 4:26-27. “…Basi kila mtu nawe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kunena, wala kukasirika. Kwa maana hasira ya mwanadamu haiitendei haki ya Mungu. Kwa hiyo wekeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu.” Yakobo 1:19-21. Mwe na hasira ila msitende dhambi.
3 MAUTI
Dhambi ni uasi, dhambi uzaa mauti. Mtu akifa leo lile jeraha la mtu kutoweka ghafla linauma sana kwa kuwa ameondoka bado unamhitaji ndiyo maana utengano haukuwepo kabisa tangu mwanzo.
4 LAUMU/ LAWAMA
Moyo haukuumbiwa kubeba lawama ndio maana moyo ukibeba jeraha huenda kuua nguvu za mifupa au tumbo. Laumu ni kitu kizito kabisa hakikuwepo tangu mwanzo.
Tangu mwanzo Mungu hakuumba moyo kubeba uoga, ugomvi ndio maana Mungu anasema vita si vyetu ni vyake. Sisi binadamu hatujui kupigana, kuachana Mungu hakuweka mpango wa kuachana tangu mwanzo ndiyo maana familia zikitengana jeraha zinabaki kwenye watoto. Moyo wa mtu haukuumbiwa kubeba visasi, chuki, usaliti kwa maana toka mwanzo havikuwepo kabisa.
Ngoja tuangalie mifano ilituone moyo ukijeruhiwa matokeo yake yanavyokuja….
Mfano 1Mithali 17:22 “Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.” Mimi sijui wangapi mnashida ya mifupa mpaka leo lakini hamjui chanzo. Umeenda kwa daktari katibu kwa nje huenda ukawa na nafuu miezi kadhaa au miaka kadhaa tatizo likarudi tena. Umetibu matokeo but hujatibu chanzo.
Mfano 2 Mithali 14:30 “Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa.” Kumbe tafsiri nyingine ya vitu viletavyo uhai ni ukiacha pumzi ya Mungu, neon la Mungu, damu n.k pia moyo wenye furaha ni uhai wa mwili.
Mfano 3 Mithali 14:29 “Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.” Kumbe ukiwa mwepesi wa hasira maarifa yote hupotea.
Mfano 3 Mithali 26:20-28 “Moto hufa kwa kukosa kuni; na bila mchongezi fitina hukoma. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni juu ya moto; Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui. Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo. Nayo hushukia za [HASHTAG]#tumbo[/HASHTAG]. Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbaya ni kama kigae c kilichofunikizwa taka za fedha. Auchukuiaye huficha chuki kwa midomo yake; Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake. Anenapo maneno mazuri usimsadiki; kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake. Ingawa chuki hufunikizwa kwa hila. Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko. Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; naye abiringishaye jiwe litamrudia. Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.” Tunaona jinsi ambavyo mioyo yetu ikiumia na ikishindwa kubeba maneno ya machochezi na kupeleka shida kwenye tumbo ndipo mtu anakua anaugua tumbo au madonda ya tumbo kwa maana muda mwingi anakuwa anawaza juu ya yale maneno.
Ayubu 34:6 “Nijapokuwa ni mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo; jeraha yangu haiponyeki, nijapokuwa sina makosa.”
Mfano 4 Zaburi 38:4-10 “ Maana dhambi zangu zimenifunikiza kichwa, kama mzigo mzito zimenilemea mno. Jeraha zangu zinanuka, zimeoza, kwa sababu ya upumbavu wangu. Nimepindika na kuinama sana, mchana kutwa nimekwenda nikihuzunika. Maana viuno vyangu vimejaa homa, wala hamna uzima katika mwil wangu. Nimedhoofika na kuchubuka sana, nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu. Bwana, haja zangu zote ziko mbele yako. Kuugua kwangu hakukusitirika kwako. Moyo wangu unapwita-pwita, nguvu zangu zimeniacha; nuru ya macho yangu nayo imeondoka.” Moyo unapobeba dhambi uhai unaondoka, uhai ukiondoka mwili unadhoofika. Kama unakumbuka katika mwanzo 6:5-6 ambapo Mungu alihuzunika moyoni mwake akatoa roho yake kwa maana sisi binadamu moyoni mwetu tunawaza machukizo tu wala hakuna jema.
Mfano wa 5 Zaburi 69:20 “ Laumu imenivunja moyo name ninaugua sana. Nika ngoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; na wa kunifariji, wala sikumwona.”
Mfano 6 Mithali 15:13-14 “ Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka. Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; Bali kinywa cha wapumbavu hula upumbavu.”
Iko mifano mingi natamani niiandike yote lakini kwa muda wako pitia MITHALI sura ya 14-16.
Tuangalie sasa uponyaji au njia za uponyaji wa moyo uliovunjika.
Marko 16:17-18 “ Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watesema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakita wadhurukabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.” Ngoja nirudie hivi Luka 9:1 “Akawaita wale thenashari, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.”
Haja zetu na zijulikane mbele za Mungu ngoja tuone mifano: Wafilipi 4:6-7 “Msijisumbukie kwa neon lo lote; bali katika kila neon kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.” Usisumbukie tiba nyingine kwa jambo lo lote maana Mungu hujishughulisha na mambo yetundio maana anatwambia haja zetu zijulikane mbele zake na amani yake ipitayo kuliko akili zote atatuweka chini ya mkono wa Kristo Yesu. Katika Zaburi 69 Daudi alipeleka haja zake mbele ya Mungu kwa maana alijua ukuu wke wala hata hakuyumbisha maneno alienda kwenye point kuwa Bwana kwa maana maji yalikuwa yanamfikia katika nafsi yake na kumwambia tazama ninazama kwenye matope mengi, nisipoweza kusimama. Kwa kuwa alichoka kulia na koo lake lilikauka akamwambia Bwana tazama adui zangu ni wengi zaidi ya nywele zangu niokoe… vivyo hivyo tena alifanya katika Zaburi ya 38 alienda mbele yake na kumwambia Mungu jeraha zake haziponi na zinanuka so wewe ni nani unakataa kumwambia haja zako unajipa matumaini pasipokuamini kuwa yeye yupo. Nenda kwa bwana na haja zako zijulikane sisi bianadamu njia zetu si za haki lakini ni kwa neema tu ya Mungu anatuongoza kwa maana Mithali 16:25 inasema njia njia ionekayo kuwa sawa machoni pa mtu; lakini mwishoni ni nia ya mauti. Nenda mbele zake kwa maana anakuita kama anavyosema katika Mathayo 11:28-30 anasema “ Njoni kwangu, nyinyi nyote msumbukao na wenye kulemwewa na mizigo, name nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.” Ametuita tulio lemewa na mzigo cheki kitu anachotuambia ‘nikabidhini fadhaa zenu’ angalia katika 1PETRO 5:6-7 anasema “ Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.” Unamkabidhi yeye vifungo vyenu, taabu zenu, mioyo yenu kwa maana yeye hujishughulisha na mambo ya kwetu. Mkisha mpa mizigo yenu mshitaki akija anaambiwa hawa wamelipiwa cash kwa damu ya Yesu hivyo magonjwa yao, taabu zao zote nimezifutilia mbali. Kwa maana mwanzo walikaa chini ya sheria ukawateka lakini sasa nimewafanya kuwa watoto wangu sikupi nafasi hata ya kuwajaribu kwa maana tulilipiwa cash msalabani ili tupate wokovu.
Jua Mungu anataka upone kabisa hivyo ongeza imani yako mbele zake ili upate uhakika wa mamlaka ulizopewa kwa maana Yesu alitupa mamlaka na kuponya na kutukabidhi funguo za mbinguni na duniani. Embu tuangalie Yeremia 6:14 anasema “Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani Amani, wala hapana amani.” Jeraha zako ni kubwa yupo Yesu Kristo mwana wa Mungu anataka upone kabisa ndio maana anakuita uje kwake uchukue nira zake kwa maana ni laini na mzigo wake ni nyepesi. Anakuita uje umpe fadhaa zako zote ili akuponye na si kumwambia vitu nusu nusu tu na kuambiana juu juu tu kuwa amani amani wakati hapana amani. Anataka uwe na uhakika wa kupona kabisa, uwe na imani kwake wakla usione shaka moyoni mwako na ukishaenda na kumtwika fadhaa zako zote na kuchukua nira yake na mzigo wake ankufanya kuwa mtoto wa Mungu. Haijalishi uko wapi au uko na umri gani njoni kwa Yesu. Mkiri Yesu Kristo kuwa ni mwana wa Mungu alifufuka siku ya tau unakuwa umeokoka na kuwa mwana wa Mungu. Wala hata hana masharti just kukiri tu kwa kinywa chako ankuja, anataka uwe na imani uache uovu uwe mwana wa pendo lake. Hataki usumbukie kwa akili zako mwenyewe zikupe majibu ya haja zako. Kuwa na Imani Waebrania 11:1 “Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.”
Warumi 10:17 “Basi imani, chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neon la Kristo.” Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neon la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendekeza Mungu. Kwa maana pasipo imani haiwezekani kumuendea Mungu lazima aamini yeye yuko na kwamba huwapa thawabu wale wamfuatao.
Kwa ajili ya kuongeza imani yako soma Waebrania 11:1-40. Maana usipokuwa na imani moyo wako utaendelea kuvunjika na majeraha yako hayatapona kabisa. Amini leo na uvae silaha za Mungu tunazipata katika Waefeso 6:11-18. Kwa maana mamlaka tuliyopewa ni kubwa na haifanyi kazi tu kinyebila imani. Mwe na imani kwa maana mkishakombolewa mshitaki wenu anazunguka kuwatafuta nafsi zenu hivyo vaeni silaha zote huku mkikesha na kuomba kwa imani na matendo yenu yakatawale na upendo kwa maana pasipo upendo imani ni bure kabisa, hata ukiomba kwa imani ukapona pasipo upendo wewe si kitu kabisa hata ukatoe msaada kwa wahitaji pasipo upendo ni bure kabisa.. jilindeni kwa maana mshitaki wenu yuko anazunguka ili awashtaki. 1 Petro 5:8-11 anasema “Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, ni kama samba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani; na Mungu wa neema yote; aliyewaita kuingia katika utukufu wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu. Uweza una yeye hata milele. Amina.”
Kuweni na matendo mema huku upendo ukitawala vyote maana ukiwa na imani na matendo mema pasipo upendo ni kazi bure kwa maana Mungu ni upendo hata akamtoa mwanae wa pekee afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Pendaneni kama yeye alivyotupenda sisi. Kwa maana huwezi mchukia ndugu yako alafu unasema unampenda Mungu huo ni unafiki hakika.
Jenga imani yako ikatibu magonjwa yote yaliyopo kwenye moyo maana pasipo imani hata uende wapi hautapona labda anaye kuhudumia akuombee kwa imani yake ili upate uponyaji. Imani ni Yesu, ndiyo kwa maana imani huja kwa neno lake.
Kwa imani naomba upate uponyaji katika jina la Yesu kristo maana kwa damu yake alitununua cash msalabani na kutufanya kuwa makuhani wa Mungu. Katika jina lake pokea uponyaji. Amina
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom