UPO WAPI MUHESHIMIWA KATIBU KINANA
Kama haupo humu JF basi una jicho lako.(zitakufikia)
Ingawa kwa mujibu wa katiba yetu kazi ya kuteua watendaji serikalini kwenye uongozi wa ngazi za wilaya,mikoa na mawaziri ni kazi ya Rais wa JMT kwa mashauriano na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, viongozi wetu hawa nao ni binaadamu na wanaweza kukosea katika uteuzi au kuna watu wazuri tu lakini jicho la Rais haliwezi kuwaona . Je, chama ( CCM) hakina wajibu jukumu au nafasi ya kusaidia?
Katika safu ya uongozi wa awamu hii,kuna viongozi ambao ni wazuri katika kazi zao wengine wapo tu ili mradi siku zinasonga mbele . Wengine wanakipa chama mzigo mkubwa wa kuwasafisha kwa Wananchi.
Kwa kumsaidia Rais asiendelee kubeba mizigo hadi 2020, ipo haja chama ( CCM) kusikiliza maoni ya wananchi kwa ukaribu zaidi na kumshauri, kwani chama hakitakiwi kuogopa ukali wa mwanachama wake
Kama kweli Rais ambaye ni mtumishi wetu, kupitia kura zetu na ndio tunaomlipa mshahara wake kupitia kodi zetu, anapenda siasa zisifanyike hadi 2020 (kama alivyowahi kusema) atazingatia maoni na ushauri wetu kwa jinsi ile ile anavyozihitaji kura zetu.
Nina imani kuwa Mheshimiwa Katibu utaliangalia hili na kulitendea haki.