Upo uhalali wa kutozwa processing fee kwenye mkopo?

Upo uhalali wa kutozwa processing fee kwenye mkopo?

Sheikh23

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Posts
1,202
Reaction score
2,001
Wakuu habari ya muda huu, niende moja kwa moja kwenye tafakuri yangu, hizi bank za kibiashara zimekuwa zikitoza viwango tofauti vya gharama za kuchakata mkopo kwa wateja wake, gharama hizi hutofautiana kulingana na kiasi mteja anachokopa na muda wa mkopo huo (niko tayari kusahihishwa).

Sina uzoefu na mikopo ya kibiashara,au mikopo ya wajasiliamali, mathalani kwa mkopo wa watumishi wa umma ambao mtumishi huchakata yeye mkopo kupitia mfumo wa Ess, Afisa utumishi/Rasilimali watu huchakata tena taarifa na kuridhia mtumishi huyo akopeshwe, Bank humalizia jukumu la kumpatia mkopo mteja wao (mtumishi) baada ya utatu huo kukamilisha protocol zote, kama mchakato ni huo,processing fee ni sharti la kisheria toka BOT? Au ni sharti la kimkataba wa mkopo?

Nini mantiki haswa ya uwepo wa takwa hili/gharama hizi ilhali hakuna mizunguko ya upitishaji wa mkopo kama ilivyokuwa kabla ya mfumo wa Ess?

Kuna namna mikopo au kukopa kunakuwa kugumu na pengine jamii kuona kukopa ni jambo la hatari kwa sababu ya milolongo mingi, riba kubwa na kukosekana kwa elimu sahihi kwa jamii.

Nawasilisha,mwenye ufahamu anijuze.

Mbarikiwe.....wabillah tawfiq
 
Nini mantiki haswa ya uwepo wa takwa hili/gharama hizi ilhali hakuna mizunguko ya upitishaji wa mkopo kama ilivyokuwa kabla ya mfumo wa Ess?
Mkuu, Nchi yetu kuna namna vitu vinaenda kwa mazoea, hivyo hata mfumo ukibadilika bado kuna baadhi ya vitu wataendelea as if hakuna kilicho badilika.

Hili ni tatizo kwa taasisi nyingi sana, BUT kwenye swala la Mikopo ile inayohusisha ASSET kama Collateral, nadhani Processing Fee iliwekwa kwakua kuna michakato kadhaa hupitia hadi Mkopo upitishwe.

Otherwise kwenye hilo la kwenu WATUMISHI, nafikiri ni muendelezo ule ule wa kukumbatia mifumo ya zamani.
 
Back
Top Bottom