MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Wakati tunalia na ya Sukari, Bunge live na ya kina Lugumi wenzetu huko Kenya kila jumatatu wanaandamana kuishinikiza serikali kubadili maafisa wa tume ya taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo kabla ya uchaguzi mkuu ujao lakini sisi tunabaki kulalamika tu wakati wa matukio.
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba kwa Katiba iliyopo mtawala anaweza kua Dikteta, anaweza kuyatumia mamlaka aliyopewa kikatiba kuamua chochote atakachojisikia. Hatuna budi kuendelea kuidai katiba mpya ili kubadili mfumo na taratibu zote za kuliendesha taifa na sio kung'ang'ana na taratibu zilizopitwa na wakati!
Hakuna mwanaCCM atakayesimama kuidai katiba mpya, hakuna atakayeridhika kubadili mfumo ambao unajua kabisa ananufaika nao! Hata kwa mchakato ulikokua umefikia ilikua ni kwa sababu za wapinzani na sio Chama tawala,hivyo wapinzani hawana budi kuendelea kupampana na hili, ndio tegemeo la wananchi.
Kuna watakaosema na kuponda kua katiba sio kipaumbele kwa sasa kwa sababu tu ya kukosa uelewa au ni makusudi tu, Taifa bora ni lazima kua na katiba bora na imara itakayoweka misingi imara ya kimaendeleo. Ni wazi kabisa kua katiba iliyopo ni mbovu, mchakato wa katiba mpya umewekwa kando, makabwela hatujui hatima yake.