Salvatory Mkami
Senior Member
- Apr 17, 2013
- 146
- 244
Yani wewe ucheze mpira umeshika panga kali kabisa halafu ufunge magoli useme wewe ndiyo mshindi? Vichekesho...
Mwenyekiti wa CCM taifa ambaye pia ni mkuu wa nchi, alipiga marufuku kufanya siasa hadi 2020. Lakini wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi katika maeneo mbalimbali nchini,baadhi ya wabunge wa CCM waliendelea na siasa. Wapinzani tukanywea, tukaogopa, tukakaa kimya, uchaguzi umefika aliyekuwa anafanya siasa akaendelea na siasa aliyekuwa kimya akaanza siasa, wewe unafikiri patatokea nini?!
Wapinzani nasi tusijipe moyo kwamba tumetetea nafasi zetu, Je, hii ina maana hatukuwa na mipango ya kushinda zaidi, au tunajipa moyo?! Huu si wakati wa huruma, wakati wa JK tulikuwa tukipiga kelele tunasikika lakini kwenye utawala huu hilo halipo. Ni wakati wa kufanya utafiti na kufanya siasa mpya zinazoendana na zama za sasa, ukisema unaogopa polisi basi acha siasa. Hakuna siasa nyepesi Afrika. Tuvute pumzi tuanze upya. Ikiwa hali ya kukaa kimya itaendelea hadi 2020 bila mikakati hakika nawaambia Upinzani utakuwa ndio byebye.
Kuungana ni sehemu moja wapo ya mkakati wa kuishinda CCM. Ndivyo kenya walifanya, Gambia, Ghana. Lakini Changamoto kubwa kwa wapinzani ni kuaminiana na hii inaleta picha mbaya kwa wanachama, inawagawa wanachama. Mgogoro wa CUF umeigharimu sana UKAWA, hili la CUF litapita na kuiacha CUF vipande, mkakati mwingine utakuwa ni kuihujumu CHADEMA, ni wakati sasa wa kuacha siasa za kuhurumiwa, kukimbilia kwenye Media kila mara. Wapinzani tunahitaji kujifungia sehemu hata kwa miezi miiwili ili kuja na mfumo mpya wenye akili wa kufanya siasa za upinzani katika mazingira ya sasa.
Binafsi nataka kuona vyama vya upinzani vinavyoipa CCM misukosuko ili kufanya nchi ipate maendeleo, nchi za Afrika zinahitaji wapinzani Imara kuvipa changamoto vyama tawala ili kuleta maendeleo yanayoshirikisha makundi katika sura ya kitaifa.